Wanawake wanamaliza sana hela Kwa bodaboda

Wanawake wanamaliza sana hela Kwa bodaboda

Unakuta mtu anataka aende sokoni, umbali hauzidi hata dakika 15 anampigia bodaboda aje amfuate na baadae amrudishe

Kutoka kituo cha daladala Hadi home dakika kadhaa tu, wikiend anakuja ghetto kufua nguo, unashangaa anakupigia simu 'nimeshafika getini njoo ufungue'..unachungulia dirishani unaona bodaboda anamshusha kisha anachukua buku lake anasepa

Siku hizi Wamekuja na staili ya 'bodaboda wangu'. Anampigia muuza chipsi anamwambia niwekee chipsi Yai kisha funga kuna mtu atafuata,mara bodaboda huyoo analeta mzigo home kisha anachukua chake anaishia zake, Wengine Hadi sokoni hawaendi tena siku hizi.Wanatuma bodaboda wanamaliza kila kitu kisha anafikisha mzigo home

Ukitembea nae mwendo mdogo tu anaweza kukuharibia siku Kwa jinsi atakavyokupandisha hasira.Utasikia 'me nimechoka kutembea bana tupande boda'..unamjibu mbona tumefika Tyr si pale tu,ananuna! Bodaboda wanakula hela za wanawake kama wachungaji wa mwendo kasi.

Kwa nini hamna huruma na hela?

Huku tunakoelekea mtakuja kutuambia tuache na bajeti ya bodaboda mezani Kwa mwendo huu mnaoenda nao.

Mmekuwa wavivu mno!!
Kama mnawahonga pesa za bure ulitaka wasitumie? Acha wale maisha
 
Mwanamke anakunywa uji wa ulezi wenye "blueband",mtori au supu halafu anashushia na juisi nzito ya embe na parachichi na hataki kutembea afanyishe mwili zoezi na mmeng'enyo upate nafasi.Matokeo yake ni kupata vitambi na magonjwa yatokanayo na aendeshavyo maisha yake.
Unfortunately wanawake wengi pamoja na kula hivyo nk huwa hawanenepeani Sana kama wanaume na mazoezi hawafanyi.
 
Wewe ndio Unawaza hivyo,Hivi kweli Mdada atoe Buku lake la Vikoba Kirahisi hivyo...Ungesema Tuwahurumie Bodaboda Ningekuelewa sana.
 
Ogopa saana akikwambia nina "bodaboda wangu"
Bodaboda wanakojolea mademu wazur hauwez amini

171698433_299370455008032_6991473953088324024_n.jpg
 
Mchunguze sana mwanamke anaependa kupanda boda boda,

hatokosa Tabia za Uvivu
hatokosa Tabia za Ufujaji Pesa
hana future plans (chunguza)

Boda Boda zipo "incase" na si kwasababu ya kutumia kila unapoenda n kwa dharura tu lakini wengi wao wameshazifanya miguu yao.

Mwanamke mpenda bodaboda ana hidden feuture nyingi ambazo ukizifahamu zitakupa majibu kuwa huyu Sio Mke wa Kuoa. (fanya tafiti) utagundua.

Wakati mwingine napenda huu utandawazi unakusaidia kujua who is the right person and who is not,Kadhalika kwenye simu Uktaka umjue Tabia zake Mnunulie Smart Phone tena anza kwa kumuuliza anapenda Brand gani,atakutajia then mengine yote utayajua kuptia hyo Smart anayotumia.

Asante Mzungu Asante Mchina,kuoa/kuolewa na gume gume sasa ivi n utake tu mwenyewe tabia zao zipo kweupeee ushndwe tu mwenyewe kutumia akili kuchambua.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom