Jamii ya sasa kwa ujumla kizazi cha wakati huu chote kimekua na uvivu, sio kwenye boda boda tu hata kwenye dala dala
Kituo hapa hadi pale mtu yupo radhi atoe 300 apande daladala,wakazi wa Dar mtu anapanda daladala Kimara Mwisho
anaenda kushukia Stop Over, au Mtu anapanda Kimara suka Anaenda shukia Temboni sehemu ambazo ukisema unatembea
hata dk 10 humalizi, sishangai watu kuumwa magonjwa yasio na kichwa wala miguu kwasababu ya kutotaka ishughulisha miguu yetu.
Ila nimeandika yoteeee, mimi ni nambari 1 kupanda hiz boda sehemu ya kwenda kwa miguu,mjue sazngine boda inawahisha mambo,dala dala kadhalika Ki ufupi ulimwengu wa sasa watu tunajali MUDA bana eboooo..
Halafu nyie wadada wapanda boda boda mimi nawashukuru maana heri yenu,kuna wale majini wana aleji na boda boda wao ni UBER tu..
Mkuuu usiombe ukutane na majini UBER bwana bwana bwana , ana App zote za online transport mzeee kuanzia UBER,BOLT hao viumbe ukikutana naoooooooo Mkuu hao wanaenda sokoni kwa uber TU..
Anakaa Makumbusho sokoni anaenda manzese chezea wewe.. anakwambia anarahisisha mizunguko ataptia kabisa na saloon kuosha nywele kubandka kucha kwa Athanas mambo kede kedeee.
Sema nini Mkuu, Mtafutie mpenzi/mke wako biashara ili hela ya boda awe anaitoa mwenyewe kupitia biashara yake Hata akitaka kwenda kariakoo na Ndege shauri lake si hela yake mwenyewe. Hela yako jibaneeeeeee Mfungulie kitu apendacho cha kumpa hizo hela za Boda Boda. Mengine achana nayo maana hawachungiki hao wala hawazuiliki n waamue tu wenyewe kubadilika.