Wanawake wa maofisini punguzeni kuombaomba

Wanawake wa maofisini punguzeni kuombaomba

101 East

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2015
Posts
1,057
Reaction score
2,256
Wanawake wa maofisini punguzeni kuwaombaomba hela vijana(wanaume) jua kwamba wanafamilia (mke, watoto, dada, mjomba, Baba, mama, shangazi) ndugu na wapenzi wanawategemea.

Imekuwa Kero sana mtu sio mpenzi wako mara anataka umnunulie chai, mara lunch na dinner wengine hadi nauli. Tena kimbembe ikifika kuanzia tarehe 20 na kuendelea vizinga vinazidi mpaka Kero yaani.

Jamani waoneeni huruma wengine wanategemewa na jamii zao ie. kanisani au msikitini
 
Uzuri wa kuombwa unakuwa na hiari ya kukataa.

Sasa na wewe kwa kupenda kwako kujionyesha unazo na wao wanakutumia kama fursa tu. Maana mpaka kuanzisha uzi inamaanisha huwa unatoa ukiombwa halafu unaenda kunung'unikia chooni.

Mwanamke daima hamuombi ombi ovyo mtu mwenye malengo nae. Wewe umefanywa hondo hondo mlezi wa wana. Pengine hizo chai unazonunua anaenda kupewa msela mwingine anywe.
 
8
Usipompa mtu ananuna salam haitikii Ukiwa na kazi ya kuprint anakwambia printer haina wino [emoji23][emoji23]
Kwani akinuna wewe unapungukiwa na nini? Kwani Computer yako haijaunganishwa via wifi na printer? Kama una kazi si unacomand inaprint, wewe unafuata printed documents tu. Hii sababu zako hazina mashiko.
 
Wanawake wa maofisini punguzeni kuwaombaomba hela vijana(wanaume) jua kwamba wanafamilia (mke, watoto,dada,mjomba,Baba,mama, shangazi) ndugu na wapenzi wanawategemea.

Imekuwa Kero sana mtu sio mpenzi wako mara anataka umnunulie chai,mara lunch na dinner wengine hadi nauli.
Jamani waoneeni huruma wengine wanategemewa na jamii zao ie.kanisani au msikitini
Kwani ukiombwa huwezi kukataa? Huna misimamo yako? Hujui mpango wako wa pesa. Mambo mengine mwanaume hutakiwi kuongea huo ni udhaifu mbaya sana
 
Back
Top Bottom