Wanawake tujikumbushie vituko vya leba

Mwingine eti unakuta akipata ujauzito haishi nongwa!
Nakwambia mara anachukia watu, wengine anamchukia mumewe jamani[emoji87][emoji87][emoji87]
Na tabia ya kula maudongo, mikaa, sabuni, unga n.k yote hayo ni mapokeo!
Hahaha kula sabuni!!??
 
Kikawaida siingiagi thread za mambo ya wanawake zaidi.
Ila leo hapa nikiwa napata moja moto ya tano kwenye kistuli, maluweluwe yakanituma em angalia kuna lipi la ajabu wakifika leba.

Aisee, kabla ya kusoma nilikuwa nimeingiwa na shetani wa kumu-harass binti aliyekuwepo karibu yangu;
lakini baada ya kusoma comment mbili tu za Mama Sabrina na Mzigua90, nimepoa hapa, nimeagiza chupa nyingine kwa adabu zote kwa dada mhudumu, nimemwambia keep the change huku nikitamani hata kumuongezea, acha nimalizie hii moja nikalale tu. Kiufupi hata zile mood za kum-harass yule binti zimekata. Nimewaona wanawake wote 'special beings'. Nimejiona mwenye dhambi pale navyowa-overlook.
.
.
.
.
Ila najua, baadae ntasahau af ntaendelea tu na insticts za kiwindaji.
 
Barikiwa kwa kutufikiria hivyo hata kama ni kwa muda mfupi
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwa uchungu ulivyo naupitaga huu uzi km ukoma

Hii ni laana kwa hakika

Hapo kwenye ukali huyo mkeo kama mimi tu nakuwaga kama simba au chui jike hadi kuunguruma huku nikiuma vyuma vya kitanda

Kuna stage manesi wanasema lalia ubavu na pumulia mdomoni wakati huo ukinywa chai ya moto......ebwana ndio
 
Mpaka nimetokwa chozi uzi ulinishindaga huu sijui nimeufufua wa nini

Nawaombea wanawake wenzangu mlioko leba malaika wa bwana akawe nanyi popote mlipo, naishia hapa kwanza
Kwa heshma na taadhima naomba niwape hongera na salute kubwa kabisa kwenu wanawake mnaojielewa.

Leba kunafurahisha na kuudhunisha pia sometimes.
Asanteni sana.

View attachment 715000
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…