Wanawake tuache kujioa, maisha mengine yanawezekana pia

Hivi ni rahisi kujifunza kupenda?

Sasa mkuu, kama hawezi kujifunza kupenda amewezaje kufanya unyama wa aina hii? Kama anaweza kudiriki kuacha mtoto na mwanamke mjamzito aliyempenda na kujitoa kwake akaenda kwa mtu mwingine na kumjengea nyumba anashindwaje kutumia ujasiri huo kujifunza kumpenda huyo mwanamke?

Sie wengine unaweza usimpende mwananmke kabisa, lakini matendo yake yakakugusa mkuu. Nguvu aliyotumia kufanya huo ukatili ni kubwa kuliko nguvu ambayo angeitumia kujifunza kumpenda huyo mke wake, mtazamo wangu tu!
 
Alichokosea huyo mwanaume ni kukubali kumuoa huyo mwanamke wakati hampendi au hajawa tayari.
 
Huyu dada mwenye mtoto mmoja na mimba ya miezi 6... Dada huyu kabla hawajafunga ndoa mmewe alikuwa hayupo vizuri kipesa, kutokana na hilo suala la ndoa lilikuwa linapigwa danadana siku hadi siku.

Kwakuwa bidada alikuwa anafanya kazi akaamua kuchukua mkopo kazini kwake, akampa kiasi bwana yule akamlipie mahari, na nyingine yakuanzishia vikao, kweli mambo ya yakaenda bidada akajigharamia kila kitu hadi pete alinunua yeye.

Baada ya ndoa, bidada akabeba mimba ya kwanza akazaa, na mwaka huo ndio mbwembwe zilianza, bidada akikosea kidogo tu, mwanaume anamwambia "Kwanza wewe ulinilazimisha kukuoa ndio maana ulijitolea mahari".

Mwanaume harudi nyumbani hata siku tatu, bidada anavumilia tu, akashika mimba nyingine ina miezi 6 sasa, mwezi uliopita bidada kagundua mwanaume amejenga Mbezi Mwisho baada yakupekua msg za mmewe, hapo wao wamepanga. Akamuuliza mwanaume akamwambia "kweli nimemjengea yule ndio chaguo langu. Bwana ndani ya wiki kabeba nguo zake kahamia huko makao mapya.

Mwanamke kaachwa nna mtoto na mimba na deni juu la mkopo, analia anatamani kujiua, anahangaika basi atoe mimba ili abaki na mtoto mmoja.

RAI YANGU:
Wadada usikimbilie kuolewa tu kwasababu mtaani watu wanaolewa, olewa kwasababu umepata mtu sahihi wa kuishi nae, ambaye anafurahi uwepo wako moyoni mwake.

Aisee hatari sana inasikitisha
 
Kufanya hilo jambo inahitaji nguvu nyingi zaidi kuliko ile inayohitajika kujifunza kupenda.

Hapana. Hiyo ni tofauti sana.
Huwezi kukubali kumuoa mtu wakati hujampenda kwa dhati au hujawa tayari kuwa naye.
Kujifunza kupenda ni ngumu sana labda kwako tu.
 
Inaumiza mamito, kama akikuwa hana mpango nae basi angemwambia tu, kamuacha mwenzie na matatizo kwenye nyumba ya kupanga. Hawa watu hawa. Mmmh!!

Mwanaume suruali tu akafie mbele kwan hajui maana ya. Kupendwa anatangatanga tu hajui anataka nini katika mapenz shetwaniiiiiii kabisa huyo.ila na wadada tujifunze kitu hapa
 
Duh hili huwa linanijiakichwani kila nisomapo mada za aina hii. Sijui kwwanini...!
nami nimewahi kujiuliza swali hili. Majibu niliyopata ni

1. Kuna watu ambao wamepewa karama (gift) ya kusaidia wengine kwenye maswala hayo kwa hiyo ni wepesi kuona tatizo na kulipatia ufumbuzi ila na wenyewe huhitaji msaada wa watu wengine kama wafanyavyo watu wote waliofanikiwa.

2. Kuna ambao wamepitia mambo magumu/mitihani migumu kwenye mahusiano na wakashinda au kushindwa kwa hiyo wakikutana na wengine wenye matatizo kama waliyokwishapitia inakuwa rahisi kutoa suluhisho kwa kuwa kwao ni marudio tu.

3. Kuna ambao hawajajitambua wao ni nani na wanataka nini kwenye mahusiano kwa hiyo hujikuta wakitumia muda mwingi wakijitafuta. Katika kujitafuta huko hugundua mambo mengi kuhusu mahusiano hivyo ni rahisi kuelewa wengine wanapitia nini.

4. Kuna ambao wangekuwa wazuri sana katika mahusiano na wangependa sana kuwepo kwenye mahusiano lakini kwa sababu fulani wanashindwa. Hivyo kisaikolojia anajaribu kuishi mahusiano ya ndoto yake kuwasaidia wengine waishi kama vile ambavyo angetamani kuishi.

5. Kuna ambao naturally wako vizuri kwenye reasoning kwa hiyo hutoa ushauri wa kujenga.
 
Hapana. Hiyo ni tofauti sana.
Huwezi kukubali kumuoa mtu wakati hujampenda kwa dhati au hujawa tayari kuwa naye.
Kujifunza kupenda ni ngumu sana labda kwako tu.

Nakubaliana na wewe mkuu, kama ambavyo ni kazi sana kula au kutumia vitu vya mwanamke nnaedai simpendi kisha kumtelekeza yeye, mtoto na ujauzito juu.
 
Kweli aisee, bora nisiwe mshauri mzuri lakini niweze kuimudu ndoa yangu. Sasa kuna manufaa gani kuwapa watu ushauri, tena mzuri wakati ndoa yangu mwenyewe ni mtihani...
Wengine wana-derive pleasure kwenye kushauri kuliko kwenye mahusiano. Halafu mitihani ndo inatupa experince. Halafu ndoa nzima ni mtihani kwa hiyo ukiona mtu yuko kwenye mtihani wa ndoa na anamshauri mwingine basi ujue maswali yao ni tofauti - hilo la mwenzie kwake rahisi, na lile la kwake gumu. Manufaa anayopata mtu kuwapa ushauri wengine ni kuwa hamfi wote. Huoni faida kuokoa ndoa mbili tatu nne labda kuna siku na wewe Mungu atakumbuka fadhila zako naye akaokoa ya kwako.
 
nami nimewahi kujiuliza swali hili. Majibu niliyopata ni

1. Kuna watu ambao wamepewa karama (gift) ya kusaidia wengine kwenye maswala hayo kwa hiyo ni wepesi kuona tatizo na kulipatia ufumbuzi ila na wenyewe huhitaji msaada wa watu wengine kama wafanyavyo watu wote waliofanikiwa.

2. Kuna ambao wamepitia mambo magumu/mitihani migumu kwenye mahusiano na wakashinda au kushindwa kwa hiyo wakikutana na wengine wenye matatizo kama waliyokwishapitia inakuwa rahisi kutoa suluhisho kwa kuwa kwao ni marudio tu.

3. Kuna ambao hawajajitambua wao ni nani na wanataka nini kwenye mahusiano kwa hiyo hujikuta wakitumia muda mwingi wakijitafuta. Katika kujitafuta huko hugundua mambo mengi kuhusu mahusiano hivyo ni rahisi kuelewa wengine wanapitia nini.

4. Kuna ambao wangekuwa wazuri sana katika mahusiano na wangependa sana kuwepo kwenye mahusiano lakini kwa sababu fulani wanashindwa. Hivyo kisaikolojia anajaribu kuishi mahusiano ya ndoto yake kuwasaidia wengine waishi kama vile ambavyo angetamani kuishi.

5. Kuna ambao naturally wako vizuri kwenye reasoning kwa hiyo hutoa ushauri wa kujenga.

Sisy....you are too smart......
 
Aise! Naomba Nikatae Kauli Za Mleta Mada Kwanza: Hakuna Mtu Anayeweza Kujioa.
Pili Naomba Nimpongeze Huyo Bidada, Ana Akili, Ana Mahesabu, Ana Mapenzi Ya Kweli, Anajua Kuyathamanisha Maisha Yake Pamoja Na Maisha Ya Mpenzi Wake Kabwera.
Tatu, Naomba Nimpe Pole Kwa Kukimbiwa Japo Amediriki Kuonesha Mapenzi Yake Kwa Uvumilivu Wake.
Nne, Nimpe Hongera Kwa Juhudi Yote Aliyofanya Bidada, Alichokusudia Alifanikiwa Na Mungu Amembariki Mtoto Lakini Pia Bidada Ni Mama Kijacho. Mungu Hatamwacha Kwa Neema Iliyoko Ndani Ya Kristo Yesu, Hiyo Mimba Atazaa Salama, Huo Mkopo Ajipe Moyo Waliomkopa Wanaona Hali Yake Na Afanye Kazi Kwa Utulivu Kama Hakumpenda Yule Kaka Kwa Mali Fulani Nadhani Hakumtegemea.
Tano, Ajaribu Kuwashirikisha Ndugu Wa Mume Jambo Hilo, Watalitatua Kwa Ufanisi Kama Labda Kuna Mali Mume Anataka Kuvusha Na Sheria Itamlinda Bidada.
Sita, Bidada Asiache Kumtembelea Mumewe Mbezi Huko Kama Atashindwa Ajaribu Kinamna Hata Kumpeleka Mtoto Akutane Na Baba,,
UJUMBE: Kwa Dada Zangu, Maisha Ni Mapenzi Tu.
 
Nakubaliana na wewe mkuu, kama ambavyo ni kazi sana kula au kutumia vitu vya mwanamke nnaedai simpendi kisha kumtelekeza yeye, mtoto na ujauzito juu.

Wengine wanatumia kama mteremko wa kufikia mafanikio yao.
Huyo mwanaume alikuwa anahitaji sehemu ya kutulia ili awe stable.
 
Aise! Naomba Nikatae Kauli Za Mleta Mada Kwanza: Hakuna Mtu Anayeweza Kujioa. Huyu amejioa kwa sababu gharama za mahari na sherehe katoa yeye pamoja na kulisha familia.

Pili Naomba Nimpongeze Huyo Bidada, Ana Akili, Ana Mahesabu, Ana Mapenzi Ya Kweli, Anajua Kuyathamanisha Maisha Yake Pamoja Na Maisha Ya Mpenzi Wake Kabwera. Ni kweli hizi sifa anazo ila kazipeleka sehemu zisikotakiwa matokeo yake zinataka kumtoa roho.

Tatu, Naomba Nimpe Pole Kwa Kukimbiwa Japo Amediriki Kuonesha Mapenzi Yake Kwa Uvumilivu Wake. Ni sawa kumpa pole ila mimi nashukuru amekimbiwa maana yule jamaa hamsatahili na ningekuwa namjua huyu dada ningemfata nimwambie akamshukuru Mungu na amuombe amtie nguvu maana wokovu wake ndo unakaribia. Na asijaribu kumrudisha huyu bwana. Kuna matatizo ya kisaikolojia usipoumia sana huwezi kupona. Ni kama dhahabu au chuma kinavyopitishwa kwenye moto ili kuvipatia ubora zaidi. wachache tunaweza kuelewa hii.

Nne, Nimpe Hongera Kwa Juhudi Yote Aliyofanya Bidada, Alichokusudia Alifanikiwa Na Mungu Amembariki Mtoto Lakini Pia Bidada Ni Mama Kijacho. Mungu Hatamwacha Kwa Neema Iliyoko Ndani Ya Kristo Yesu, Hiyo Mimba Atazaa Salama, Huo Mkopo Ajipe Moyo Waliomkopa Wanaona Hali Yake Na Afanye Kazi Kwa Utulivu Kama Hakumpenda Yule Kaka Kwa Mali Fulani Nadhani Hakumtegemea. Kwa kuwa ni sala nami naungana nawe kumuombea ila wenye mkopo hali yake haiwahusu.

Tano, Ajaribu Kuwashirikisha Ndugu Wa Mume Jambo Hilo, Watalitatua Kwa Ufanisi Kama Labda Kuna Mali Mume Anataka Kuvusha Na Sheria Itamlinda Bidada. hapa sijaweza kufikiri

Sita, Bidada Asiache Kumtembelea Mumewe Mbezi Huko Kama Atashindwa Ajaribu Kinamna Hata Kumpeleka Mtoto Akutane Na Baba,, NI sawa na kusema mwimba ukikuchoma ukishatibu jeraha ukautafute ukochome tena, au kama bado hujatibu jeraha ukautafute uongeze jeraha ili utamu wa maumivu ukolee zaidi.
UJUMBE: Kwa Dada Zangu, Maisha Ni Mapenzi Tu.
Starehe ya mapenzi uwe na akili zako zote timamu na si mahaba niue
 
Huyu dada mwenye mtoto mmoja na mimba ya miezi 6... Dada huyu kabla hawajafunga ndoa mmewe alikuwa hayupo vizuri kipesa, kutokana na hilo suala la ndoa lilikuwa linapigwa danadana siku hadi siku.

Kwakuwa bidada alikuwa anafanya kazi akaamua kuchukua mkopo kazini kwake, akampa kiasi bwana yule akamlipie mahari, na nyingine yakuanzishia vikao, kweli mambo ya yakaenda bidada akajigharamia kila kitu hadi pete alinunua yeye.

Baada ya ndoa, bidada akabeba mimba ya kwanza akazaa, na mwaka huo ndio mbwembwe zilianza, bidada akikosea kidogo tu, mwanaume anamwambia "Kwanza wewe ulinilazimisha kukuoa ndio maana ulijitolea mahari".

Mwanaume harudi nyumbani hata siku tatu, bidada anavumilia tu, akashika mimba nyingine ina miezi 6 sasa, mwezi uliopita bidada kagundua mwanaume amejenga Mbezi Mwisho baada yakupekua msg za mmewe, hapo wao wamepanga. Akamuuliza mwanaume akamwambia "kweli nimemjengea yule ndio chaguo langu. Bwana ndani ya wiki kabeba nguo zake kahamia huko makao mapya.

Mwanamke kaachwa nna mtoto na mimba na deni juu la mkopo, analia anatamani kujiua, anahangaika basi atoe mimba ili abaki na mtoto mmoja.

RAI YANGU:
Wadada usikimbilie kuolewa tu kwasababu mtaani watu wanaolewa, olewa kwasababu umepata mtu sahihi wa kuishi nae, ambaye anafurahi uwepo wako moyoni mwake.

Inaumiza sana....lol! Pole yake bidada, sio peke yake wapo wengi tu wanaojitolea mahari
 
Back
Top Bottom