Najiona maisha Yangu yakikosa nuru kabisa na kuelekea ukingoni

FORTUNE JR

Member
Mar 20, 2021
69
350
Wakuu habari, poleni na majukumu ya kila siku.

Ni hivi wadau kila nikishika simu yangu nakuiona app ya JF napata hasira natamani kupigiza simu yangu chini, Maana bila platform hii huwenda maisha yangu yangekua na amani na matumaini.

Mimi sio mdau saana wakuandika nyuzi humu JF lakini hupenda sana kupitia nyuzi mbalimbali za wadau zenye kujenga, kufunza na kuelimisha. Niliipenda platform hii kutokana nakuwa na watu wengi matured na haina vishawishi ukilinganisha na platform nyingine.

Miezi 3 iliyopita niliandika uzi kwa mara ya kwanza kutokana na changamoto fulani iliyonisibu hivo nikatamani mawazo kutoka kwa wadau mbali mbali.

Kuna baadhi ya wadau wali reply private(DM) ikiwemo bi dada mmoja ambae alinijenga sana finally akanipa namba yake nimcheki whatsapp, In short nikazaoeana nae kirafiki tu, so ana view status zangu na view zake utani wa hapa na pale maisha yakasonga.

Honestly sikuwaza kumtongoza na sikuwa na intention yoyote kwake, alinambia anasoma chuo X Dodoma.

Hivi karibuni bidada alini call anadai anasafari ya Dar, kuna ofisi Fulani aliomba nimwelekeze kwakua yeye si mwenyeji sana Dar na hana m2 wa karibu sana anaeweza kumwomba ampeleke, uzuri ni kwamba hizo ofisi hazipo mbali sana na ninapo ishi so nikamwambia afike then nitampa maelekezo vema.

Siku inayofwata asubuhi aliniarifu anasafiri kutoka Dodoma, alifika majira ya mchana na tukafanikiwa kukutana, hio ndo ilikua mara ya kwanza kukutana live baada ya urafiki wa miezi kama mitatu hivi.

Marshallah bidada ni mzuri kuliko nilivyomkusudia ana rangi ya chocolate fulani ivi iliyopoa.

Nilimsindikiza had hio ofisi na uzuri tuliwahi kabla muda wa kazi haujaisha alifaniwa kilichompeleka na akadai kesho yake angeludi Dodoma asichelewe masomo chuo.

Aliomba nimtafutie lodge yenye utulivu then kesho asafiri kurudi Dom nkamwambia haina neno.

Binafsi naishi na Wazazi wangu Tegeta ila pia na Gheto langu Kinondoni ambalo lipo karibu na sehem ninapofanya kazi ya kujishikiza niliyopata baada ya kumaliza chuo.

So huwa nikiwa nataka utulivu binasi huwa napoa apo pia kazi zikizidi sana ofisini huwa natumia muda mwingi kupoa hapo.

Kabla sijampeleka bidada lodge akapumzike na mimi niendelee na majukumu yangu, nilimwomba tupitie kwangu kwakua hatukua mbali kuna issue nilihitaji kufanya, so tulifika hadi kwangu (Kinondoni) nikamkaribisha bidada ndani stori zikatunogea na baadae kuna wazo likanijia kwanini asilale 2 pale kwasababu mm nilipanga kurudi hom Tegeta.

Na Fact ni kwamba ilikua ndo siku ya kwanza kukutana na binti live, ila tulizoena sana kama watu tuliojuana muda mrefu.

Nadhani hii ilichagizwa nachatting zetu before kwenye simu kwa takribani miezi mi 3 nyuma, alikua mcheshi, mstaarabu kifupi sikupata mashaka sana kumwacha pale na vi2tu vyangu.

Baada ya kutoa wazo la kuwa nimwachie room apumzike alilipokea na akadai nitakua nmemsaidia sana, stori hazikuisha baina yetu mbaka majira ya saa 4 kasoro baada ya kuhakikisha amekula nikataka kuondoka lakini bidada aliomba nisiondoke she was like " Sitakua Comfortable kabisa kubaki peke yangu naogopa then kesho nataka nitoke mapema sana.

We lala Zako kitandani me hata apa kwenye sofa patatosha sana, kikubwa tuheshimiane we ni rafiki ang,".

Ikumbukwe hadi kufika point hii sio kama binafsi sikuvutiwa na binti ni mzuri kiukweli ila binafsi nilikua na mtu wang ambae sikutaka kumvunjia uamifu kwakua daima amekua moja ya nguzo muhimu sana kwangu.

Ananiheshimu na ananisikiliza na tushapanga mengi, hivyo nilikua rai kufumbia macho hili.

Kosa langu linaanzia hapa, kukubali kulala na Huyu dada room, tamaa zikazidi mwili nkajikuta namtaka kimapenzi, alikataa sana nikama alikua na hofu fulani.

Woga na hofu niliyoiona usoni kwa binti ilinifanya niamini huwenda ni mtu mwenye principles na mipika yake, kijana mm niliyepandwa na tamaa za mwili ambae kichwa kinawaza tu jinsi ya kuzikidhi nikazidi kulazimisha finally binti akaona isiwe tabu taratibu kwa unyonge na hofu kubwa akaanza kuvisusa viwalo vyake hadi akawa mtupu.

Hapa kidogo nikapata mashaka baada ya kumwona na bonge la tattoo nyuma kiunoni, juu kidogo ya makalio, hii ilionyesha dhahiri pindi anachorwa alikua uchi, lakin akili inayosindikizwa na hisia inanambia i'ts none of your business we kizi haja yako.

Ndani sina kinga kwakua nilikua sio mtu wa michezo hio. Kifupi nililuka na binti usiku kucha ad siku ya pili anaaga na kuondoka lakini kuna jinsi kawa mnyonge, jioni akanichek kafika.

Baada ya siku kama 4 hivi kupita nikawa najisikia maumivu wakati wa kukojoa na finally naona usaa unanitoka, nikajua tayari, muda wa mavuno ya tamaa zangu umefika, nikaenda zangu hospital.

Baada ya vipimo naambiwa nina UTI sana, ila Gono nikaambiwa sina.

Nikashauriwa ni vyema nichome sindano 5 na Dawa nikapewa, nimemaliza sindano nadawa nikapata ahueni kidogo.

Baada ya muda kidogo tena najickia maumivu makali ndani ya mlija wa uume na saa hii usaa zaidi.

Nikamtafuta kaka ang hivi yeye ni Daktari pia baada ya kumpa dalili akadai ni Gono niende akanipime, baada ya vipimo akadai ni Gono na limeshamili sana na akadai ile dozi ya awari na sindano inaonekana zimewatibua hawa wadudu wako very active, akanipangia sindano 7 na dozi nyingine.

Linalo nichanganya zaidi ya yote ni kwamba huyu dada kuna Ujumbe aliniandika ni mrefu kiasi lakini kifupi anadai amefurahi kuniju mm ni m2 mwema , na pia anasikitikia maisha yangu na anajihisi mkosaji sana kuangamiza maisha yangu mtu mwema.

Napiga simu yake haipatikani namba zote, Whatsapp pia simpati, cna hakika kama kani block maana nikimchek hata kwa namba tofaut simpati, all social media alizokua anatumia ni kuko kimya no response.

Nime recover sasa naendelea vizuri but akili yangu haiachi kuwaza kama huenda huyu binti kuna kingine kaniachia zaidi ya hivi ninavyoviona.

Napata woga kwenda kuchukua HIV test na pia huyu daktari anasema ni mapema sana kufanya test maana ni week kadhaa tu .

Nina mawazo sana hasa nikirejea kusoma text ya huyu dada ina mafumbo ndani yake ila haiashirii mema kabsa. Cna hata rafiki au m2 mwingine ninae mjua anaefahamiana na uyu binti.

Na katika urafki wetu nilifanikiwa kujua jina lake 1 tu na Chuo chake x na alidai n mzaliwa wa Tanga full stop.

Wakuu katika hali hii niliyonayo ya msongo wa mawazo nikifikiri ni kipi nitaenda kukutana nacho naomba kusema Afya ndo utajiri wa kwanza kabisa kwa mwanadamu, ile mentality ya kutambua unakitu mwilini na kina athiri afya yako ina haribu sana utendajikazi wa ufahamu wako na inatowesha kabisa mwangaza wa maisha . Tuishi tukitanguliza nyendo zetu kwa Mungu , kuna makosa hayakupi nafasi ya pili.

BROTHERS, kulala na kuwa na wanawake wengi it's not manhood ila kuna time hufikaga lazima ulipie madhambi yako, kuna mistake moja 2, it will totally change your life. Sometimes tunashindwa kutimiza malengo na ndoto za mafanikio kwasababu ya humu tunamopita ni mikosi na laana tunapata. Tujali afya zetu, tule vizuri, tufanye mazoezi, tuombe Mungu na kutunza vipato vyetu tunamajukumu makubwa sana ya kuendeleza na kuandaa vizazi vyetu bora.

LADIES wakati ni ukuta, u slay queen unaukomo tena hauchukui round "Walk the right way you will meet the right people" . Kuna heshima fulani mwanamke unaipata automatic ukitambua misingi yako na ukijiheshimu kwenye ndoa yako.

Asanteni kwa time yenu. Ushauri wenu, mawazo yenu na neno lolote litanijenga sana katika hali hii, napia huenda itakua msaada hata kwa wengine since we still live so kuna leo na kesho. 🙏
 
Mkuu subiri muda ukapime ili uwe huru kimawazo kwa sababu kwa sasa utaendelea kuwa na hofu sana...

Kitu kingine kwa kuwa umeandika una mchuchu wako, kabla hujahakikisha afya yako hakikisha unamkwepa usije naye ukamletea shida kama ipo...
 
Andika Vizuri, Panga Kazi Yako
Wasomaji Tuelewe, Sasa Undishi Wa Kurundika Hivyo Unaondoa Mvuto

Summary:

Jamaa anahisi kaambukizwa HIV na mdada waliyefahamiana kupitia JF...

Sababu ya kuamini hivyo inatokana na mosi, kaambukizwa gono, pili kuna maneno ambayo aliandikiwa na huyo bi dada yanayoonesha kama hatma ya afya yake ina walakini...

Kwa sasa hajapima afya yake kuondoa hiyo hofu, hivyo anaomba ushauri wa wadau kuweza ku-move on
 
Ningekuwa mimi wewe..kwanza namuanika humu ili kilicho kupata wewe kisiwapate wengine.

Ondoa uoga... pambana na hizo dozi ulizo pewa halafu ukapime.

Kaa mbali kwa muda na ulie kuwa nae mwanzo kwenye uhusiano mpaka ukae sawa.

Usijilaumu wote tunafanya makosa
Mungu akutangulie....kila la kheri
 
Sasa Mkuu Huna Elimu Yeyote kuhusu PEP? JF haijakusaidia kujua kuhusu PEP?

Ushauri ulioutoa Kwa wanawake wawe na msimamo mwisho waishie kubakwa na wewe?

Pole Kwa Maambukizi.

Hapa naamini ukiangalia vijana wenzako wakkipita na afya zao unawaonea wivu. Si ndiyo? Hayo ni mashaka. Kaka Yako kama alitwaa damu Yako atakuwa na majibu tayari.

Pima upate ushauri.
 
Back
Top Bottom