Wanawake tuache kujioa, maisha mengine yanawezekana pia

Apologise lady

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2013
Posts
5,980
Reaction score
3,115
Huyu dada mwenye mtoto mmoja na mimba ya miezi 6... Dada huyu kabla hawajafunga ndoa mmewe alikuwa hayupo vizuri kipesa, kutokana na hilo suala la ndoa lilikuwa linapigwa danadana siku hadi siku.

Kwakuwa bidada alikuwa anafanya kazi akaamua kuchukua mkopo kazini kwake, akampa kiasi bwana yule akamlipie mahari, na nyingine yakuanzishia vikao, kweli mambo ya yakaenda bidada akajigharamia kila kitu hadi pete alinunua yeye.

Baada ya ndoa, bidada akabeba mimba ya kwanza akazaa, na mwaka huo ndio mbwembwe zilianza, bidada akikosea kidogo tu, mwanaume anamwambia "Kwanza wewe ulinilazimisha kukuoa ndio maana ulijitolea mahari".

Mwanaume harudi nyumbani hata siku tatu, bidada anavumilia tu, akashika mimba nyingine ina miezi 6 sasa, mwezi uliopita bidada kagundua mwanaume amejenga Mbezi Mwisho baada yakupekua msg za mmewe, hapo wao wamepanga. Akamuuliza mwanaume akamwambia "kweli nimemjengea yule ndio chaguo langu. Bwana ndani ya wiki kabeba nguo zake kahamia huko makao mapya.

Mwanamke kaachwa nna mtoto na mimba na deni juu la mkopo, analia anatamani kujiua, anahangaika basi atoe mimba ili abaki na mtoto mmoja.

RAI YANGU:
Wadada usikimbilie kuolewa tu kwasababu mtaani watu wanaolewa, olewa kwasababu umepata mtu sahihi wa kuishi nae, ambaye anafurahi uwepo wako moyoni mwake.
 
Ni kweli kabisa lazima unapokuwa unafanya maamuzi ya kuoa au kuolewa lazima umpime vya kutosha anaetaka kukuoa,

Kufanya maamuzi kwa ajili ya presha za umri au mashinikizo mwisho wake ni mbaya mnoo...

Lakini kosa la huyo dada sio kujioa, ila anajioa na mtu wa aina gani....hapo ndipo tatizo lilipo...

Mungu atubariki wanaume tusipende saana wadada wanaojioa..
 
c.c atoto,
mito Ulisema kweli kaka angu, mwanaume atakuheshimu tu akiwa hana hela. Akishapata vijicent basi ndo utamjua tabia yake vizuri. "Pata pesa tujue tabia yako ".

Nimekuja kujifunza kitu kimoja (thanks to Irene mbowe). Mwanaume mspoil kadri utakavyoweza dinner, sijui vizawadi vidogo sawa kabisa, but never kumuhudumia. Wanaume wengi atakuwa anakutumia kukwambia hakutaki hawezi as wewe ndo Kisima chake cha fedha, ila mkewe wa moyo yupo mahali pengine. Mwanaume ameambiwa "atakula kwa jasho". Muache azoee kutokwa jasho, ukimlemaza sasa hivi tegemea kucheka kitalebani kwa sababu huyo atakuwa tu irresponsible man kwenye ndoa na hivyo unatengeneza bomu litakalokuja kukulipukia. Au laah akikuacha sasa hivi utakuwa na sababu million za kulia. Kwanza umeachwa, umetumika kimwili na hela zako zimekwenda mwee

Yote tisa, kumpa mwanaume hela eti akakutolee mahari koma ukomazike. Ndo haya kila siku utaambiwa "me nilikutolea mahari? tobaa. Muache atafute yeye mwenyewe hiyo hela ya mahari. Nyie mpangieni tu mahari kidogo but as long ametokwa jasho kuitafuta atakuheshimu maana kahenyeka kukutoa kwa wazazi wako

Huyo dada hana haja ya kumkufuru Mungu, wala huu si muda wa kuanza kujilaumu, yameshatokea. I hope familia yake itakuwa karibu naye sana kwa wakati huu, wamsaidie kwa Vyovyote watakavyoweza. Msaada wa maneno ya faraja (hakawii kunywa sumu) hata wa kifedha ili apunguze mkopo wake. Alee tu mimba yake, Mungu atamfungulia njia hadi yeye mwenyewe hatoamini. Karma is a bitch and fate is a hoe Tutaona mwisho wa huyo mume.
 
Last edited by a moderator:
...akaamua kuchukua mkop kazini kwake, akampa kiasi bwana yule akamlipie mahari, na nyingine yakuanzishia vikao, kweli mambo ya yakaenda bidada akajigharamia kila kitu hadi pete alinunua yeye.

Ati akafanyaje? ila na sie wanaume dhambi nyingine ni za kujitakia tu. Hata kama mtu haumpendi , kwa juhudi yote hiyo aliyoonyesha mama wa watu hauwezi kujifunza kumpenda? Laana zingine zinaepukika!
 
c.c atoto,
mito Ulisema kweli kaka angu, mwanaume atakuheshimu tu akiwa hana hela. Akishapata vijicent basi ndo utamjua tabia yake vizuri. "Pata pesa tujue tabia yako ".

Nimekuja kujifunza kitu kimoja (thanks to Irene mbowe). Mwanaume mspoil kadri utakavyoweza dinner, sijui vizawadi vidogo sawa kabisa, but never kumuhudumia. Wanaume wengi atakuwa anakutumia kukwambia hakutaki hawezi as wewe ndo Kisima chake cha fedha, ila mkewe wa moyo yupo mahali pengine. Mwanaume ameambiwa "atakula kwa jasho". Muache azoee kutokwa jasho, ukimlemaza sasa hivi tegemea kucheka kitalebani kwa sababu huyo atakuwa tu irresponsible man kwenye ndoa na hivyo unatengeneza bomu litakalokuja kukulipukia. Au laah akikuacha sasa hivi utakuwa na sababu million za kulia. Kwanza umeachwa, umetumika kimwili na hela zako zimekwenda mwee

Yote tisa, kumpa mwanaume hela eti akakutolee mahari koma ukomazike. Ndo haya kila siku utaambiwa "me nilikutolea mahari? tobaa. Muache atafute yeye mwenyewe hiyo hela ya mahari. Nyie mpangieni tu mahari kidogo but as long ametokwa jasho kuitafuta atakuheshimu maana kahenyeka kukutoa kwa wazazi wako

Huyo dada hana haja ya kumkufuru Mungu, wala huu si muda wa kuanza kujilaumu, yameshatokea. I hope familia yake itakuwa karibu naye sana kwa wakati huu, wamsaidie kwa Vyovyote watakavyoweza. Msaada wa maneno ya faraja (hakawii kunywa sumu) hata wa kifedha ili apunguze mkopo wake. Alee tu mimba yake, Mungu atamfungulia njia hadi yeye mwenyewe hatoamini. Karma is a bitch and fate is a hoe Tutaona mwisho wa huyo mume.

Inaumiza mamito, kama akikuwa hana mpango nae basi angemwambia tu, kamuacha mwenzie na matatizo kwenye nyumba ya kupanga. Hawa watu hawa. Mmmh!!
 
Last edited by a moderator:
Ati akafanyaje? ila na sie wanaume dhambi nyingine ni za kujitakia tu. Hata kama mtu haumpendi , kwa juhudi yote hiyo aliyoonyesha mama wa watu hauwezi kujifunza kumpenda? Laana zingine zinaepukika!

Mambo mengine laana tu, kwanin asingemjengea akamuacha salama ndio akaondoka.
 
Inaumiza mamito, kama akikuwa hana mpango nae basi angemwambia tu, kamuacha mwenzie na matatizo kwenye nyumba ya kupanga. Hawa watu hawa. Mmmh!!
Hapo analia na mengi ujue. Unawaza una limkopo, kodi, chakula + ulee watoto wawili. Bora hata asingekuwa na hilo deni maskini, ila Mungu yupo tu.

Sasa unadhani huyo mkaka angeweza kusema kuwa hamtaki? Thubutuu si anajua anahudumiwa bure, alikuwa anamtumia tu ili hadi asimame amtose dada wa watu. Mungu ampiganie tu huyo dada maskini
 
hata huyo mwanamke mwingine ajiangalie sana, kama huyu jamaa ameweza kumfanyia hivi huyu dada licha ya fadhila zote hizi unafikiri kitu gani kitamzuia kumuacha huyo mpya?

Umeamini wanaume hamna akili, utu, na mna roho mbaya sana??
 
Jaman, ukimuona mwanamke analia jua analia na mengi moyoni. Hata huvyo machoz ni sehemu ya sala, Mungu atamsikia
 
Umeamini wanaume hamna akili, utu, na mna roho mbaya sana??

Japo sio wote lakini ndio tabia zetu....hauoni hata huyo mwanamke mwingine nae inabidi alaumiwe? Sitaki kuamini kua alikua hajui yote hayo kuhusu hali ya huyo mwanaume japo huenda hakuambiwa ukweli.

Hapo kwenye tabia za ajabuajabu ni kwa pande zote mbili, na inategemea mtu na mtu. Mwanamke anaweza kufanya kituko ukabaki kinywa wazi hali kadhalika na sisi wanaume kwa matukio kama hili la jamaa yetu nako hatujambo, kwa hiyo sio suala la upande mmoja.
 
Heaven Sent mie msimamo wangu kuhusu pesa yangu uko pale pale, na hautokaa ubadilike.

Mwanaume lazima awe mwanaume tu, hivyo viherehere vinipite mbaliii.
Love is blind only if you let it blinds you, maisha ni darasa lisiloisha twajifunza mapya kila siku, japo pia kuna wanawake bit.ches ambao hufanya kama hayo hayo pia.
So tufumbue macho tu na tumtumaini sana Mungu atupe watu sahihi na kamwe tusiache kumtumainia yeye.

Hii dunia sasa ni tafrani, bila rehema na neema za Mungu sijui kwakweli tunakoelekea, hata kama ndio umempata mtu sahihi muache asimame kwa miguu yake kama mwanaume, let him play his part n you just play yo part of being a woman.
 
Last edited by a moderator:
hata huyo mwanamke mwingine ajiangalie sana, kama huyu jamaa ameweza kumfanyia hivi huyu dada licha ya fadhila zote hizi unafikiri kitu gani kitamzuia kumuacha huyo mpya?

Hakika umenena hakuna jinsi atalikwepa hilo,kwa sababu kama anaweza kujenga nyumba ni wapi kuwa hata mahari isingemshinda.Wanaume tunajitakia laana sana kwetu n.a. hata vizazi yetu.

Kwa sasa Nashauri huyu mama kwa vyovyote alivyojitoa asiweke focus yake kwenye tatizo ambalo limeshatokea kwa sababu hatoweza kufanya au kuamua chochote kwa haraka,afarijiwe kwa kile atakachohitaji.
Let her focus be on God,that whoever call the name of the God shall be saved.

Haijalishi huyo mume amemuacha kwenye nyumba n.a. kuondoka.Atarudi kwa magoti kunyenyekea tena Mara Saba .Asimama n.a. kuomba kwa mungu aliye juu,mwanadamu si chochote mbele ya uweza wa mungu .
Wafilipi 4:13
 
Pole yake masikini weeee.....

Hivi unaanzaje kumpa mwanaume pesa.......

Kuna raha mwanaume kustruggle kupata pesa ya kukulipia mahari hata kama ni kidogo........

Mwanaume pekee unayeweza mpa pesa ninmuneo tu... (tena kama sio gumegume)
 
Mwache mwanaume awe mwanaume......... acheze nafasi yake kama mwanaume

Kuna wale wanaowahonga wanaume.... wakishajioa kama hivi ndani ya nyumba anabeba majukumu yoooooye mwenyewe...miezi sita tu utamwona anaomba ushauri kwenye group whatsapp au fb???? Mpaka unajiuliza alikuwa na matarajio gani...

Ila inahitaji moyo na roho kumhonga mwanaume mtu mzima alokamilika viungo mwenye nguvu na kipato....

Heaven Sent mie msimamo wangu kuhusu pesa yangu uko pale pale, na hautokaa ubadilike.

Mwanaume lazima awe mwanaume tu, hivyo viherehere vinipite mbaliii.
Love is blind only if you let it blinds you, maisha ni darasa lisiloisha twajifunza mapya kila siku, japo pia kuna wanawake bit.ches ambao hufanya kama hayo hayo pia.
So tufumbue macho tu na tumtumaini sana Mungu atupe watu sahihi na kamwe tusiache kumtumainia yeye.

Hii dunia sasa ni tafrani, bila rehema na neema za Mungu sijui kwakweli tunakoelekea, hata kama ndio umempata mtu sahihi muache asimame kwa miguu yake kama mwanaume, let him play his part n you just play yo part of being a woman.
 
Last edited by a moderator:
Yaan wadada na suala la kuolewa sijui mpewe dawa gani ili muelewe.

Mtu yuko radhi kufanya chochote ilimradi aingie kwenye ndoa au afunge ndoa.

Utafiti wangu umegundua kuwa, wengi wanafanya ivo ili wajulikane mtaani, kwa marafiki na hata kwa ndg kuwa flani kaolewa, lakini hana aidea yeyote ya maisha baada ya ndoa ya ndoa yatakuwaje.

Badilikeni kina dada for sure, muwe na mawazo chanya, dont force things please na mwisho wa siku unaumia mara 98%.
 
Mwache mwanaume awe mwanaume......... acheze nafasi yake kama mwanaume

Kuna wale wanaowahonga wanaume.... wakishajioa kama hivi ndani ya nyumba anabeba majukumu yoooooye mwenyewe...miezi sita tu utamwona anaomba ushauri kwenye group whatsapp au fb???? Mpaka unajiuliza alikuwa na matarajio gani...

Ila inahitaji moyo na roho kumhonga mwanaume mtu mzima alokamilika viungo mwenye nguvu na kipato....

Mwanamme halisi hulali kwa mkweo,huajiriwi kwa mkeo,hulishwi n.a. mkeo,ndio wale unaishia kudandia wadada wenye hela mjini.Usubiri mke achune up one hapo.

NDIO mpaka mnapata dhihaka za kutunziwa wake,watoto na wanaume wenzenu,ni kujishushia heshima.

Hakuna dharau mbaya km mwanamme mwenzio anajua uko hai & kukufanya uncircumcised deiwaka
 
Back
Top Bottom