ITR
JF-Expert Member
- Sep 22, 2022
- 7,070
- 19,195
Jana hapa mtaani kwetu tumemzika mmama mmoja mwenye miaka 35 baada ya kujaribu kutoa mimba.
Ni hivi huyu mama alikuwa na mme wake ambaye ni raia wa uganda sasa mme wa huyo dada akaondoka kwenda nyumbani kwao Uganda nadhani kuna miradi yao waliyo kuwa wamewekeza huko hivyo alienda kuisimamia akamaliza miezi mitano.
Kumbe huku nyuma baada ya baba mwenye nyumba kuondoka mwana mke akaanza kukitembeza mwisho wa siku akabeba mimba,na kwa mujibu wa mme wake anadai miezi 4 iliyo pita mke wake alimpigia simu akitaka amfuate huko uganda maana alikuwa amemsi sana nadhani alikuwa anatengeneza mazingira ya kumbambikizia mimba mme wake lakini jamaa akagoma kata kata.
Mwisho wa siku siku za mme wake kurudi zikafika mke si akaenda kuichoropoa hiyo mimba ya unzinzi sasa sijui waliitoa vibaya akawa ameenda nayo kuzimu tumemzika jana ameacha watoto wawili.
Lakini hili tukio limeniacha na maswali mengi sana bila majibu yake.
Swali la msingi ni hivi kama huyu mwanamke alikuwa amesha beba mimba ya mchepuko na zoezi la kumbambikizia mme wake limeshindikana kwa nini hakuitoa mapema badala yake akailea na akaja kuitoa ikiwa imesha komaa?