Wanawake, oneeni huruma watoto wenu basi!!!!

Wanawake, oneeni huruma watoto wenu basi!!!!

Huna dada...!!?
Mama, baba yako?
Shangazi yako au mama mdogo?
Bibi na babu hawa wawe wa mwisho.

Kuliko mtu asiyekufahamu akuhifadhi kwa miezi 3 borq hao ndugu zako wa damu na masimango juu hawatakukula ukakwisha.

Acha watoto kwa hao ndugu mmoja wapo wote kwa pamoja, nenda kasake tonge uwe unakuja kuwaona wanao kila wiki. Miezi mitatu ikifika uwe na kwako kwa kudumu uendelee kulea wanao.
Madama Kasie. Ukikosa moja hukosi na 2. Wakati mwingine na maoni ya watu huwa mchango mkubwa wa kuchukua maamzi. Binafsi, siamini katika mtu kumbebesha majukumu. Unafight na hili, likigoma unaattack lingine, na mwisho wa siku, kutoboa lazima.

Ni challenge tu za muda, na siko down kivileeee, kiasi kwamba kina mama walee, mimi ambae sikupata nguvu ya kutekekeza nishindwe! Hapana.

Labda nimetumia kauli isiyo sahihi, na lengo langu tu ni kwamba mwezi ukute bado kuna kitu. Kwa hiyo, si kwamba ni zero kabisa. Hapana
 
Duuh pole mkuu kwa changamoto yako sijawahi kusikia single faza analalamika ndo kwanza nasikia kwako.

Anyway pambana tu mzee
Single faza wapo wengi sana, nina mshkaji wangu kamlea binti yake tangu akiwa na miaka miwili sasa hivi yupo darasa la 7 ana miaka 13 kama sikosei. mama mtoto alikua mtu wa bata sana sasa hivi hatujui yuko wapi na hajawahi hata kupiga simu kuulizia kuhusu mwanae.

Mimi mwenyewe kaka angu alivyofariki niliachiwa jukumu la kumlea mwanae. Gharama ninazoingia ni kama vile dogo hana mama. Kila kitu nalipa mimi, mpaka kodi ya nyumba wanapoishi yaani wakati mama mtoto anafanya biashara zake na hela anapata

Sema ndio vile tu sisi wanaume sio watu wa kulalamika ndio maana yanayotukuta hayasikiki sana
 
Jibu na maamuzi unayo hapa, uzi ufungwe.
Hapana. Kwanza hapa ni kama tupo sebuleni. Mi ni binadamu, si mkamilifu. Na huenda naloliona tatizo, kwa wenzangu ikawa tofauti. Na ndo maana ya majibu yenu, yapo ya ushali na mengine yamekaa kiaina. Sema tu, ile kwamba ungefanya hivi na hivi, pengine wazo langu lisiwe solution, ila nina imani katika maoni ya wengi ntapata muongozo. Kama wapo kina mama wanalea, wengine watoto zaidi ya kwangu, na wanachokipata ni chini ya nachokipata mimi, si huenda akatokea mtu, akanipa muongozo tena ukanifaa!? Msiufunge tafadhali.
 
Mkuu, umenena vema kwenye comment yako hapo juu. Unadhani, niliweza walipokua na mwaka mmoja, leo wamefikisha 3 ndo nifeli? Yaani wakose mama, wakose baba? Sijazaa mtu anilelee, japo labda bahati mbaya ni kuzaa na mtu asie na upendo, hata hao ndugu huenda nilichukua maamzi hayo kuepusha hizo lawama. Stranger ni binadamu kama wengine, kwa kidogo nikipatacho hata nikienda Kibiti watakua tu. Mzigo wangu, ntakomaa nao mkuu.
Mkuu unapatikana wapi?
 
Tunaendelea kupata fundisho kupitia JF na maisha kwa ujumla

Zaeni mkiwa na uwezo wa kutunza watoto wenu tofauti na hapo sisiemu wataendelea kulaumiwa bure
Afrika tunazaa experience ,kule Japan wameacha Kutokana na maisha ya sasa; ugumu wa malezi hasa kipat ,kufanya kazi ,kukosa muda wa kutunza familia.
 
Huku wanakwambia kila mtoto anakuja na sahani yake
😂😂Haifanyi kazi kwa sasa ,maisha yanasumbua sana ...Wale vijana watatu waliojinyonga kule Mbeya ,wote wana watoto..Maisha yamekuwa magumu sana..
 
Haya single maza sasa hivi dawa ya hawa viumbe ni kuwaachia watoto walee wenyewe..!! Hii kuwasaidia kulea watoto matokeo yake yanakuja huku kutukana single maza.

Na wewe single faza pole komaa tu mkuu, ni watoto wako hao.. !!
 
Haya single maza sasa hivi dawa ya hawa viumbe ni kuwaachia watoto walee wenyewe..!! Hii kuwasaidia kulea watoto matokeo yake yanakuja huku kutukana single maza.

Na wewe single faza pole komaa tu mkuu, ni watoto wako hao.. !!
Wala,

Nikila watakula, nikikosa watapoa, kama wamama wanalea, iweje mi nishindwe!

Wala usiwaze hivo, kwamba dawa yao ni kuwasusia. Wengine bado wanahitaji kula bata na kutoka kila aina ya demu, hivyo kama mama unaejitambua, utamtesa mtoto tu.
Mtu yeyote anaeweza kutelekeza damu yake, huyo ni mnyama, jihadhali nae. Siku zote ukimuona mtu anamtukana single mother, IQ yake weka 0.
 
Daycare uwiano wa gharama na matunzo kwa kweli vimechengana. Kuhusu kuwatafutia, nina kazi nayoifanya nikiwa home. Changamoto tu ni ile kukauka kabla ya tarehe.
Hapo kazi ipo
Inabidi upeleke wattoto WA bibi yako Ili ujipinde zaidi kutafuta riziki
 
Kupata sehemu tena kwa mtu baki ety ukae ww na wanao wawili tena kwa miezi mitatu huo ni uongo aisee, tumia akili kwa mara nyingine tena mkuu
 
Kupata sehemu tena kwa mtu baki ety ukae ww na wanao wawili tena kwa miezi mitatu huo ni uongo aisee, tumia akili kwa mara nyingine tena mkuu
Umenielewa vibaya mkuu. Japo sipo vibaya kihivo,kiasi cha kutegemea mtu na wanangu, ninaingiza chochote.

Nimemaanisha kwa mtu anayeweza kuwa na nyumba ambayo ni vacant(iliyo wazi). Na hiyo miezi mitatu, huenda isifike.
 
Tunaendelea kupata fundisho kupitia JF na maisha kwa ujumla

Zaeni mkiwa na uwezo wa kutunza watoto wenu tofauti na hapo sisiemu wataendelea kulaumiwa bure
Hakika, inaumiza sana
 
Back
Top Bottom