mkada
JF-Expert Member
- Nov 14, 2011
- 1,200
- 903
Wanawake mlioolewa acheni hii tabia isiyo ya kistaraabu ya kudokoa hela kwenye mifuko ya suruali na mashati ya waume zenu,,,haiwezekani unadokoa mpaka elfu kumi ,,ukiulizwa unasema eti aah nimechukua chenjichenji tu mme wangu
chenji chenji elfu kumi?? sasa leo nimegundua elfu hamsini anasema aaah nilikuwa nikuambie kuwa nimechukua hela kwenye suruali yako
samahani baba watoto wangu nitakurudishia.Hii tabia sio nzuri,,mbaya zaidi ukiwa umelewa siku hiyo na umetoka kufunga mahesabu,,inaweza kuchomolewa mpaka laki moja.Inakera sana,,this is not fair kabsa.Hela zenu ninyi mnakuwa wakali kama pilipili,,,haiguswi.Badilikeni.