Heshima yenu humu ndani wakuu.
Wanawake kwa nini mnakuwa na roho mbaya hivyo?
Inakuwaje unamletea visa mtu ambaye mlikuwa mnapendana ambaye mlipanga mambo mbalimbali ya kimaisha?
Mtu ambaye amekusaidia mbalimbali leo hii unamuona hafai. Kweli Wanawake ni viumbe ajabu sana.
Huwa wanaficha makucha wanapokuwa wanahitaji kitu fulani kwa wakati fulani.Pindi apatapo hicho kitu ghafla utaona anabadilika mpaka unajikuta na wewe unajishangaa mara mbili mbili.
Miezi kama miwili iliyopita nilikutana na mrembo na ana kila sifa ya kuitwa mwanamke. Mwenye umbo namba 8 umbo hatari sana.
Basi tukawa tumependana na kuwa na mipango mingi tu ingawa yeye alikuwa hana kazi yoyote. Kitu cha kwanza nikamsaidia akapata kazi kwenye kampuni moja hapa mjini kwa mshahara wa laki 4 tu.
Baada ya kupata hiyo kazi nimeshangaa ghafla amebadilika sana. Simu nikipiga hapokei na akipokea anatoa sababu za kijinga sana. Kama mjuavyo huwezi ukaacha kujipa matumaini kimtindo kuwa umpendae atakuwa poa tu huenda kuna kitu kinamsumbua.
Leo nmeangalia kwenye whatsApp ameniblock na nikipiga simu haipatikani so nashindwa sijui nifanyeje. Nikajaribu kumcheki kwa namba mpya hakupokea ikabidi nimtumie Meseji ya kumuuliza kama amepata hela niliyomtumia kiasi cha laki moja.
Baada ya dakika mbili akipiga akinieleza kuwa hajapokea hapo hapo nikamchana ukweli kuwa una ongea na Fulani( nikataja jina langu) kabla sijamaliza kutaja jina simu ikakatwa.
Mpaka muda huu hakuna simu inayopokelewa tena wala sijibiwa Meseji.Hivyo nimelidhika na matokeo maisha yanasonga kimtindo.
Mfariji wangu wa karibu kwa sasa ni movie. Hakuna namna nyingine.
Nawashauri Wanawake kama haumtaki mtu mwambie ukweli ajue siyo kuigiza kuwa unapenda kumbe uko pale tu kwa manufaa yako binafsi.
Ahsanteni.