robstunner
JF-Expert Member
- Apr 26, 2017
- 225
- 196
Wanawake 4,000 wakutana Ruvuma kula na kufurahi kwa kumpata Tundu Lissu kuweza kuzungumza ukweli wa kile kinachoendelea nchini. Wanawake hao wameshangaa kuona wanaume wote wamekuwa waoga kiasi cha kumuachia Tundu Lissu tu kuweza kupambana na goliathi. Wameapa watazunguka nchi nzima kuhakikisha wanahimiza wanaume na wanawake wa nchi nzima kuaacha kuogopa kukemea ukiukwaji mkubwa wa sheria za nchi kwa kisingizio cha kuleta maendeleoa. Pia wametaka wakulima nchini kusimama kidete kwani wakulima ambao ndio wananchi walio wengi wanaendelea kuwa masikini kwa kitendo cha serekali kutokujali sekta hiyo inayobeba wananchi wengi. Wemesema wanashangazwa sana wanaposikia kuna kiongozi anayepigania wanyonge huku akipunguza bajeti ya kilimo kwa kiwango kikubwa na kulipa jeshi hela nyingi kupambana na upinzani. Hawakuishia hapo bali walisema wanashangaa kiongozi wa wote kutumia nafasi ya kufungua miradi ya maendeleo ya kodi toka wananchi wote kufanyia chama chake siasa za wazi huku akigomea vyama vingine kufanya kazi zao za kisiasa kwa mujibu wa katiba. Wanawake hao watagawanyika katika makundi sita kuzunguka nchi nzima kueneza ujumbe usemao "madai ya maendeleo isiwe kisingizio cha uonevu na kunyima uhuru wa kujieleza kwa wenye mitazamo tofauti"
NB: Hapa tunakosoa kistaarabu bila kejeli wala matusi.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji111]️[emoji1479][emoji1479][emoji1479]
