Wanaume: Zama zimebadilika

Kauli za uoga hizi, kumbuka hata ukiwa na range watu wenye rolls royce watamchukua tu mtu wako. Bil gate katarakiana na mpenzi wake na anapesa, unajua sababu.

Sikia maisha hayana formula moja japo kuna sheria ndogondogo unawez kuzifuata ili usiishi kwa presha. Jipende na kula kwa size yako ila uisiache kula kisa hauna.
 
Hii injili ina ukweli mwingi. Wasipokuelewa achana nao. Wanawake wamegeuka ombaomba, ukiwanyima tu watakupa majina mabaya mabaya halafu kuna wanaume wenzako watawapa support. Maisha ni kuchagua
Binafsi hata sijali kuhusu wao kuwa omba omba watajua wao, kikubwa nisiwe mtu wa kusemwa, at the end of the day, kila mtu atashinda mechi zake
 
Sijasema kuwa wenye pesa hawaachwi ila naongea ukweli wa mahusiano ya kuwa kama wewe ni kapuku utaishia kunyanyasika na kujieleza sana
 
Mimi naona ukiwa na mahusiano na mwanamke mwenye utu na ambaye ata add value kwenye maisha ndio issues kwa mahusiano serious.
Mwanamke asiye na value kiuchumi au angle nyingine ya maisha haina maana ikiwa umelenga mahusiano. Uzuri hautoshi, malezi, utu( namna anavyo chukulia watu wengine hasa walio chini yake) akikosa hili basi anaweza kukushushia hadhi hata mbele ya watu.
Anyway kuna watu wanapenda kuteseka maana kuna mtu anaweza kukomba ushauri juu ya binti fulani aneyetaka kuwa naye alafu uka mpa ushauri kuwa hafai na bado akawa naye na akaja kujuta. So naona bora ku acha mtu ateseke cos ndicho alicho kitaka.
Tukuze maarifa ni chakula cha nafsi.
Pia kuna angle yakujifunza maana waigizaji ni wengi kutest them na kuwapush kihisia wataonesha rangi zao alisi. Tunajofumza kwenye makosa.
Ukitaka kuoa au uchumba basi mtizame mama wa mpenzi wako namna anavyoishi na mumewe au jamii kwanza kabla hujafanya maamuzi au familia yake. Mf. Tabia au standard yao maana ni adimu kuwa na watoto wafalme walio lelewa na mtumwa.
 
Ndo unajifariji hivyo? Unafikiri kisa anakuvumilia na kapuku wako siku akipata offer ata bali kuku Heshimu? Acha kujipa umuhimu ambao huna
Heshima hainunuliwi kijana, ninyi good boys mna tabu sana.

Na kaa ujue kua mwanamke haridhiki, utamnunulia kila atakacho bado atadai tu. Sasa wakibatika kupata buzi moja la kulichuna kama wewe hivi aloo ndio wanajengaga kupitia kibunda chako maana huna cha kuoffer zaidi ya pesa tu.
Na hiyo heshima utayopewa ni feki, kuna kapuuzi hakahudumii na neno lake ni sheria kwa huyo demu wako unaemuhudumia.
 
Watu mkipigwa matukio huko mnakuja JF kutisha watu na kutujaza ubaya wanawake, tafuta pesa kwa ajili ya ustawi wa maisha yako na si kwa sababu ya mwanamke kwani wangapi wana pesa na mapenzi yanawanyoosha??? mapenzi hayana maalumu.

Madogo hawa wameshalambwa za uso huko mtaani kwao, then wanakuja kulia lia huku. Mapopoma kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…