Wanaume wananichukulia tofauti na nilivyo

Wanaume wananichukulia tofauti na nilivyo

Pana kazi hapo, najitahidi kufanyia kazi mambo kadhaa, kidogo kidogo nasonga.

Ni kweli kabisa. Kujikosoa mwenyewe, na kukubali makosa yako mwenyewe, na kisha kujifanyia marekebisho ni kazi ngumu sana.

Na kwa sababu ni kazi ngumu, watu huishia tu kunyoosha vidole vya lawama kwa wengine....ooh wanaume hivi...wanawake vile.

Wakati inawezekana kabisa kuwa wewe mwenyewe labda ndo unawafanya watu wakuone jinsi ulivyo kwa sababu hivyo ndivyo ulivyo lakini hutaki kukubali mapungufu yako.
 
^^
Ni kawaida ya kundi la aina yenu, nje mnajiamini, nje mna nguvu, nje mnajiweza, nje mnazidi sifa za baadhi ya wanaume! Ndani mnaumia, mna upendo, mnahitaji kufarijiwa, mnapenda kujitoa kwa dhati na kwa hiari, Lakini wanaume wanaojua siri yenu hii hamkutani nao sana!
Sasa, vaa tabasamu, ondoa mikunjo ya uso, tembea na ufunguo wa kuyaona mambo ni mepesi ! Azima sauti ya kawaida! Be simple!
Wanaume wengi hawavutiwi na mwanamke aliyekama mwanaume! Make a femine revolution inside yourself. Your a beautiful woman trust me.
(oo! Sorry kumbe hii ni thread ya wanasaikolojia, yachukulie hayo maneno ya mlevi tu)
^^

Shikamoo Himidini

"Azima sauti ya kawaida"... Umehisi na sauti yake ni kubwa, nzitooo tehe.. Ushauri mzuri
 
Last edited by a moderator:
Wengine tunaambiwa ni wababe, wakali, tunajiamini na bado tunatongozwa
Tulia hajapatika tu wa kwako atakuja tuu, atakuvumilia hivyo hivyo na ubabe wako
 
Wengine tunaambiwa ni wababe, wakali, tunajiamini na bado tunatongozwa
Tulia hajapatika tu wa kwako atakuja tuu, atakuvumilia hivyo hivyo na ubabe wako
Ndo jf hii.
thanks
 
Unayosema miss chagga ni kweli kabisa. Hizi tabia zetu za, I can pay, I can argue, I can challenge him bila kuangalia uko wampi na mtuo zinawatisha hawa viumbe wa jinsia tofauti na yetu. Sometimes ni kuwaacha wajione wanaume wanaoweza kutumiliki na ku-take care of us.

Kudeka muhimu sana: we hata panya na mende unataka uwaue wewe wkt kidume mwenye nguvu yupo, ukipigiwa simu hata sauti ulainishi.

hapo sasa.. yani mimi nikiona panya au mende kama kuna mwanaume naruka hata juu ya kabati napanda afu akisha muua najifanya nimefikaje huku njoo nishushe looh... mwanamke raha ujue kudeka loh
 
Ila kwenye haya makitu hakunaga mbabe...si unamjua simba? Na ubabe wake wooote ila yakimfika shingoni anapigwa ma love bites ya kutosha na anakuwa mpoleeeeee kama kondoo dadadeki...endelea kukomaa tu kigum! gum!
anapigwa malavidavi na pundamilia au impala?
 
badilisha muonekano usijibu watu vibaya yaan jibu la mojakwamoja mwanamke kaumbiwa aibu na staha,sasa kama ww huna aibu ukitongozwa hung'ati hata kucha na majibu ya direct si lazima uonekane mbabe,hiyo ni tabia ambayo unaweza kujibadilisha ondoa hofu kwa ushaur zaidi unaweza uka-n-pm
 
ukiambiwa kitu kinachokuhusu na watu zaidi ya watatu ambao hafahamiani uchukulie kuwa watu wanakuchukulia hivyo. la muhimu hapa badala ya kupinga maneno ya watu uyafanyie kazi.
Kuna vitu ambavyo tunavifanya bila wenyewe kujua, watu wanaotuambia wanatupenda na wanataka tubadilike (kama ni kitu ambacho hakina maslahi).
Fanyia kazi hayo wanayokuambia badala ya kubishia.
Nakutakia kila la heri katika mabadiliko

umeniigilizia nilichotaka kusema natania tu mimi sina la kuchangia umemaliza yote mkuu
 
hapo sasa.. yani mimi nikiona panya au mende kama kuna mwanaume naruka hata juu ya kabati napanda afu akisha muua najifanya nimefikaje huku njoo nishushe looh... mwanamke raha ujue kudeka loh

Hongera sana miss chaga,yaan jinsi unavyojua hizo ishu utafikiri si mchagga...
 
ni mchaga(mchanganyiko wa Marangu na Rombo) ila sio mmachame

Okay,pole sana aicee but ni tabia ambayo unaweza kabisa kuiondoa kama ukiamua,tatizo ni kuna wale wengine huwa hawakubali udhaifu huo hata ukiwaambia ukweli ni wabishi...
 
Learn to be feminine...no man wants another man as a partner my dear...
Jifunze kuongea polepole kwa sauti ya chini,aibu ya kike kiasi,be more caring and loving,supportive,usiwe mgumu na kimbelefront all the time,let ur man take care of things and you esp in public, deka na umdekeze mpenzi wako,dress like a woman,...inshort do everything like a woman...life is really sweet this way
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom