Wanaume wa JF mna shida gani?

Wanaume wa JF mna shida gani?

Binadamu anayependa kulalamika sijui anashindwa kuelewa kujifunza au vipi, tusipende kulalama kwa kila kitu. Tujue kuwa vitu kama hivi katika jamii zetu huwa sio jambo geni.


Kuna forum huwa naangaza macho nikipata muda(japo kimalikia ni tatizo ), hakuna ulalamishi wa ajabu. Sema ndio hivyo, jamii tofauti.
 
Hivi wewe unapokuwa faragha na mumeo huwa act the same way mkiwa mbele ya watoto wenu au watu wengine.


Always people act according to the environment and situation.

Usimuone Zero IQ ana stori nyingi za migegedo ukadhani kwenye kiwanda chake cha kuchakata chips pia ana hizo hizo stori, never.

Mbona unaonekana una IQ kubwa lkn fact ndogondogo kama hizi unashindwa kuzing'amua?
Jibu lako hilo hapo.
 
Binti andiko lako siyo ya kupuuzwa hata kidogo mabaharia tutafanyia kazi
 
Hiyo hoja yako eti tu wachache duniani, naomba source ya hiyo data yako @Uvelia
Nimekuwa mfuatiliaji wa huu mtandao not so long, mwanzoni sikuweza kujiunga kwasababu sikujua namna ya kufanya hivyo. Baadae nikikutana na mtu ambae pia ni mtumiaji wa huu mtandao ndio akanipa ABC's za namna ya kujiunga.

Nilikuwa naiona kwenye suggestions ninapogoogle jambo, nikavutiwa nao sana. Ila nikajikuta nakuwa msomaji tu na nilitamani sana kuwa mmoja wa members humu. Hatimae nikafanikiwa.
Nilijiunga na nikaendelea kuwa msomaji tu hadi hapo nilipoamua kuwa mchangiaji pia. Ila nilivutiwa sana na jukwaa la MMU na CC.

Kwa muda wote nimekuwa nikishindwa kuwaelewa members wa kiume wa humu ndani. Ni wako na tatizo gani? Ni malezi mabovu,stress,kukata tamaa,elimu duni(nieleweke sio ya darasani tu) au tatizo ni nini haswa?

Wengi wao sio wastaarabu kabisa, mtu aweza kuleta mada yake badala wachangie kwa hoja wao ni matusi tu na hii ni hata jukwaa la siasa ambapo ningetegemea kuwakuta wenye weledi na hoja madhubuti kama ilivyo sifa ya mtandao huu(home of great thinkers)
Kuna siku nilileta uzi nikashambuliwa sana kwa matusi, nasikitika niliwajibu kulingana na level yao ya thinking ila i was not proud of it at all.

Hivi nyie binadamu wenye kuitwa wanaume haswa wa humu ni kwasababu gani hamna maadili na hamjielewi?
Hii inatupatia picha wazazi watarajiwa kuwa makini sana na watu tunaotaka wawe baba wa watoto wetu, hivi kama baba wa familia anakosa maadili na upeo namna hii ataiongoza vipi familia yake?

Kuna wakati nikiona mwanaume ana app ya jf kwa simu yake namtafakari sana, namchukulia kitofauti kidogo. Nashukuru mdogo wangu sio member humu.
Wapo wachache atlest ukisoma unafarijika kuona kuwa angalau bado tuna akina baba bora kwenye jamii zetu. Tambueni nyie ni wachache kwa idadi duniani, kwahiyo mnapaswa mjitafakari sana je mnastahili kuitwa wanaume au ni viumbe wenye uume tu?

Kuitwa mwanaume tayari ni jukumu, hivyo tangu ukiwa mdogo unapaswa kukuzwa hivyo. Sasa kama mlipitia malezi mabovu kutoka kwa wazazi its about time dunia iwafunze.
Acheni kujisifia mambo ya kipumbavu, mna jukumu kubwa sana hapa duniani, kumbukeni mlipoteleza kisha mchukue hatua.

Ipeni JF heshima yake kama ilivyo kauli mbiu yake.
 
And this is exactky what i am talking about.
Id na avata zaweza kuwa fake lakini anayecomment ni binadamu sio kuku.
Mtu huwa halisi sana anapohisi hakuna anayemfahamu, utajiuliza what if alichoandika ni uongo? Then jibu ni ameandika fantancy ya vile anatamani kuwa(hii ni kwa wale wanaofake maisha mitandaoni) hivyo hiyo bado haiondoi uhalisia wake.

Mdogo angu uvella uschukulie mambo serious sana humu mitandaoni

Wengine humu tunachangamsha watu tuu !
 
Bidadaa, humu ndan usiuumize kichwa sanaaa.

Mimi na ID kibao.

Saa ingine ID moja naigiza Jeuri jeuriiii.


ID ingine nakua bonge la Mume mwema.

Hata ivo Sijaoa, MD sijaajiliwa serikalini, nmeajiliwa Hosp Binafsi hapa Bongo

Umri wangu hata sijafika 30

Nina kakitambi fulan ivi kakijinga

Mweusi kama Lamiii

Vimacho.vidogoooo



Karibu tuyajenge Lavu
Nshaijua id yako chief 😅😅
 
Back
Top Bottom