Wanaume wa JF mna shida gani?

Wanaume wa JF mna shida gani?

Mada nzuri

Umewachoma wengi haswaaaaaaa
💉💉💉💉💉💉 sinawauma
 
Umejuaje hao wanaokudisappoint ni wanaume wakati wanatumia id fake?

BTW usione watu wanachangia kwa mizaha/matusi ukadhani ndio walivyo hivyo pia kwenye real life, noo. Sometimes wanafanya ivo kuchangamsha jukwaa tuu.

Mwenye tatizo ni ww unayedhani ndivyo walivyo hadi kwenye real life.
Possibly, kuna wanawake wanatamani kuwa wanaume...lakini kuwa mwanaume haimaanishi kuwa stiff all the time to what you're doing, ndio maana kuna jokes za apa na pale, hivyo mahali kama hapa ndio watu wanaona ni sehemu ya ku relax. Sio vyema kumlazimisha mtu awe kama unavyotaka, kila mtu ana life style yake na ana approach yake ya ku handle mambo yake. Otherwise, huyo bado binti na hawaelewi vyema wanaume walivyo.
 
Tatzo watu wanashindwa kuelewa kuwa watu waliopo huku jamii forum ndio wale wale tuliopo huku mtaani.
Yaan mnachulia kana kwamba waliopo humu ni cream tu

Palipo na wengi kuna mengi kwahyo humu kuna

waadilifu
waaminifu
waongo
masikini
matajiri
mabachela
wasiowaadilifu
wenye dharau
wenye heshima
wapiga kelele
wezi
watukanaji
wazinzi
matapeli
wanasiasa
single mazas
mabinti
mabachela
wake za watu
slay kwins
malaya
n.k
 
Nimekuwa mfuatiliaji wa huu mtandao not so long, mwanzoni sikuweza kujiunga kwasababu sikujua namna ya kufanya hivyo. Baadae nikikutana na mtu ambae pia ni mtumiaji wa huu mtandao ndio akanipa ABC's za namna ya kujiunga.

Nilikuwa naiona kwenye suggestions ninapogoogle jambo, nikavutiwa nao sana. Ila nikajikuta nakuwa msomaji tu na nilitamani sana kuwa mmoja wa members humu. Hatimae nikafanikiwa.
Nilijiunga na nikaendelea kuwa msomaji tu hadi hapo nilipoamua kuwa mchangiaji pia. Ila nilivutiwa sana na jukwaa la MMU na CC.

Kwa muda wote nimekuwa nikishindwa kuwaelewa members wa kiume wa humu ndani. Ni wako na tatizo gani? Ni malezi mabovu,stress,kukata tamaa,elimu duni(nieleweke sio ya darasani tu) au tatizo ni nini haswa?

Wengi wao sio wastaarabu kabisa, mtu aweza kuleta mada yake badala wachangie kwa hoja wao ni matusi tu na hii ni hata jukwaa la siasa ambapo ningetegemea kuwakuta wenye weledi na hoja madhubuti kama ilivyo sifa ya mtandao huu(home of great thinkers)
Kuna siku nilileta uzi nikashambuliwa sana kwa matusi, nasikitika niliwajibu kulingana na level yao ya thinking ila i was not proud of it at all.

Hivi nyie binadamu wenye kuitwa wanaume haswa wa humu ni kwasababu gani hamna maadili na hamjielewi?
Hii inatupatia picha wazazi watarajiwa kuwa makini sana na watu tunaotaka wawe baba wa watoto wetu, hivi kama baba wa familia anakosa maadili na upeo namna hii ataiongoza vipi familia yake?

Kuna wakati nikiona mwanaume ana app ya jf kwa simu yake namtafakari sana, namchukulia kitofauti kidogo. Nashukuru mdogo wangu sio member humu.
Wapo wachache atlest ukisoma unafarijika kuona kuwa angalau bado tuna akina baba bora kwenye jamii zetu. Tambueni nyie ni wachache kwa idadi duniani, kwahiyo mnapaswa mjitafakari sana je mnastahili kuitwa wanaume au ni viumbe wenye uume tu?

Kuitwa mwanaume tayari ni jukumu, hivyo tangu ukiwa mdogo unapaswa kukuzwa hivyo. Sasa kama mlipitia malezi mabovu kutoka kwa wazazi its about time dunia iwafunze.
Acheni kujisifia mambo ya kipumbavu, mna jukumu kubwa sana hapa duniani, kumbukeni mlipoteleza kisha mchukue hatua.

Ipeni JF heshima yake kama ilivyo kauli mbiu yake.
Nimefuatilia thread zako....
Anyway km hutojali tufahamiane
 
And this is exactky what i am talking about.
Id na avata zaweza kuwa fake lakini anayecomment ni binadamu sio kuku.
Mtu huwa halisi sana anapohisi hakuna anayemfahamu, utajiuliza what if alichoandika ni uongo? Then jibu ni ameandika fantancy ya vile anatamani kuwa(hii ni kwa wale wanaofake maisha mitandaoni) hivyo hiyo bado haiondoi uhalisia wake.
Nimekukubali hapa tu.
 
Mwanaume unao wataka mbona tupo sema umeshindwa kugundua kama kuna vijana wa miaka ya 90 nakuendele ndio wanaosumbua kichwa yako amini nakuambia mtu mzima kama mimi hakuna asye mwelewa labda awe mlevi wa majani
Ofcz.Inawezekan
 
Unachotakiwa kufahamu kama unatumia ID fake, ata mawazo au ushauri unaweza kuwa fake;kwa hiyo mawazo ya wachangiaji unaweza kuyachukulia siriazi au kuyapuuzia ili maisha yaendelee.
 
Back
Top Bottom