Wanaume wa JF mna shida gani?

Wanaume wa JF mna shida gani?

mimi mwenyewe nashangaa wanawake kama wewe mda wa kupikia mumeo huu upo tu unapiga kelele hapa jf au hujaolewa?basi kama huna mume una tatizo sehem solve kwanza hilo tatizo lako ndo uje kupambana na matatizo yetu
Another one thinking life is all about cooking.
 
Mwanaume unao wataka mbona tupo sema umeshindwa kugundua kama kuna vijana wa miaka ya 90 nakuendele ndio wanaosumbua kichwa yako amini nakuambia mtu mzima kama mimi hakuna asye mwelewa labda awe mlevi wa majani
Then be the change.
 
Nimekuwa mfuatiliaji wa huu mtandao not so long, mwanzoni sikuweza kujiunga kwasababu sikujua namna ya kufanya hivyo. Baadae nikikutana na mtu ambae pia ni mtumiaji wa huu mtandao ndio akanipa ABC's za namna ya kujiunga.

Nilikuwa naiona kwenye suggestions ninapogoogle jambo, nikavutiwa nao sana. Ila nikajikuta nakuwa msomaji tu na nilitamani sana kuwa mmoja wa members humu. Hatimae nikafanikiwa.
Nilijiunga na nikaendelea kuwa msomaji tu hadi hapo nilipoamua kuwa mchangiaji pia. Ila nilivutiwa sana na jukwaa la MMU na CC.

Kwa muda wote nimekuwa nikishindwa kuwaelewa members wa kiume wa humu ndani. Ni wako na tatizo gani? Ni malezi mabovu,stress,kukata tamaa,elimu duni(nieleweke sio ya darasani tu) au tatizo ni nini haswa?

Wengi wao sio wastaarabu kabisa, mtu aweza kuleta mada yake badala wachangie kwa hoja wao ni matusi tu na hii ni hata jukwaa la siasa ambapo ningetegemea kuwakuta wenye weledi na hoja madhubuti kama ilivyo sifa ya mtandao huu(home of great thinkers)
Kuna siku nilileta uzi nikashambuliwa sana kwa matusi, nasikitika niliwajibu kulingana na level yao ya thinking ila i was not proud of it at all.

Hivi nyie binadamu wenye kuitwa wanaume haswa wa humu ni kwasababu gani hamna maadili na hamjielewi?
Hii inatupatia picha wazazi watarajiwa kuwa makini sana na watu tunaotaka wawe baba wa watoto wetu, hivi kama baba wa familia anakosa maadili na upeo namna hii ataiongoza vipi familia yake?

Kuna wakati nikiona mwanaume ana app ya jf kwa simu yake namtafakari sana, namchukulia kitofauti kidogo. Nashukuru mdogo wangu sio member humu.
Wapo wachache atlest ukisoma unafarijika kuona kuwa angalau bado tuna akina baba bora kwenye jamii zetu. Tambueni nyie ni wachache kwa idadi duniani, kwahiyo mnapaswa mjitafakari sana je mnastahili kuitwa wanaume au ni viumbe wenye uume tu?

Kuitwa mwanaume tayari ni jukumu, hivyo tangu ukiwa mdogo unapaswa kukuzwa hivyo. Sasa kama mlipitia malezi mabovu kutoka kwa wazazi its about time dunia iwafunze.
Acheni kujisifia mambo ya kipumbavu, mna jukumu kubwa sana hapa duniani, kumbukeni mlipoteleza kisha mchukue hatua.

Ipeni JF heshima yake kama ilivyo kauli mbiu yake.
Usiwashangae, shule walienda kusomea ujinga.
 
Ooooh! Now i get it.
Asante mkuu.
Hahaha mama watu tuna stress. Humu tunakuja kuzipunguza, humu ndiyo baba na mwana wanarushiana madongo na inawasaidia kurelieve steam ya maisha.
 
Inategemea majukwaa yapi utakayoingia ama utakayowasilisha mada. Kwa mfano ukiingia Jukwaa la Siasa kubaliana na yote tu. Au Jukwaa la MMU nayo kubaliana na yote tu.

Ila Jukwaa kama la Intelijensia, Jukwaa la Kimataifa na mengineyo yanayofanana na hayo yapo tofauti. Sababu kuu kule kunahitaji nguvu ya hoja yenye vidhibiti, na vilevile masuala ya kule yanahitaji ufuatiliaji na usomaji. Usipokuwa nayo hayo ni ngumu kuchangia.

Ila nakuunga mkono. Ujinga upo mwingi sana! Pendelea kutembelea "Nyuzi" za zamani zina mengi ya kujenga ikiwa ni mwenye uhitaji.

Mbali na yote, pole! Karibu Jf.
 
Usiwashangae, shule walienda kusomea ujinga.
Hahahaaaa!! Shukrani sana mama, wewe ni kati ya members ambao nimekuwa nikivutiwa sana kusoma mada na comments zako hata kabla sijawa member. Sikufahamu ila kiumri unaonekana u mtu mzima kidogo au kama sio hivyo basi umekulia familia yenye maadili mema.
 
Back
Top Bottom