Wanaume wa JF mna shida gani?

Wanaume wa JF mna shida gani?

Bidadaa, humu ndan usiuumize kichwa sanaaa.

Mimi na ID kibao.

Saa ingine ID moja naigiza Jeuri jeuriiii.


ID ingine nakua bonge la Mume mwema.

Hata ivo Sijaoa, MD sijaajiliwa serikalini, nmeajiliwa Hosp Binafsi hapa Bongo

Umri wangu hata sijafika 30

Nina kakitambi fulan ivi kakijinga

Mweusi kama Lamiii

Vimacho.vidogoooo



Karibu tuyajenge Lavu
 
Nimekuwa mfuatiliaji wa huu mtandao not so long, mwanzoni sikuweza kujiunga kwasababu sikujua namna ya kufanya hivyo. Baadae nikikutana na mtu ambae pia ni mtumiaji wa huu mtandao ndio akanipa ABC's za namna ya kujiunga.

Nilikuwa naiona kwenye suggestions ninapogoogle jambo, nikavutiwa nao sana. Ila nikajikuta nakuwa msomaji tu na nilitamani sana kuwa mmoja wa members humu. Hatimae nikafanikiwa.
Nilijiunga na nikaendelea kuwa msomaji tu hadi hapo nilipoamua kuwa mchangiaji pia. Ila nilivutiwa sana na jukwaa la MMU na CC.

Kwa muda wote nimekuwa nikishindwa kuwaelewa members wa kiume wa humu ndani. Ni wako na tatizo gani? Ni malezi mabovu,stress,kukata tamaa,elimu duni(nieleweke sio ya darasani tu) au tatizo ni nini haswa?

Wengi wao sio wastaarabu kabisa, mtu aweza kuleta mada yake badala wachangie kwa hoja wao ni matusi tu na hii ni hata jukwaa la siasa ambapo ningetegemea kuwakuta wenye weledi na hoja madhubuti kama ilivyo sifa ya mtandao huu(home of great thinkers)
Kuna siku nilileta uzi nikashambuliwa sana kwa matusi, nasikitika niliwajibu kulingana na level yao ya thinking ila i was not proud of it at all.

Hivi nyie binadamu wenye kuitwa wanaume haswa wa humu ni kwasababu gani hamna maadili na hamjielewi?
Hii inatupatia picha wazazi watarajiwa kuwa makini sana na watu tunaotaka wawe baba wa watoto wetu, hivi kama baba wa familia anakosa maadili na upeo namna hii ataiongoza vipi familia yake?

Kuna wakati nikiona mwanaume ana app ya jf kwa simu yake namtafakari sana, namchukulia kitofauti kidogo. Nashukuru mdogo wangu sio member humu.
Wapo wachache atlest ukisoma unafarijika kuona kuwa angalau bado tuna akina baba bora kwenye jamii zetu. Tambueni nyie ni wachache kwa idadi duniani, kwahiyo mnapaswa mjitafakari sana je mnastahili kuitwa wanaume au ni viumbe wenye uume tu?

Kuitwa mwanaume tayari ni jukumu, hivyo tangu ukiwa mdogo unapaswa kukuzwa hivyo. Sasa kama mlipitia malezi mabovu kutoka kwa wazazi its about time dunia iwafunze.
Acheni kujisifia mambo ya kipumbavu, mna jukumu kubwa sana hapa duniani, kumbukeni mlipoteleza kisha mchukue hatua.

Ipeni JF heshima yake kama ilivyo kauli mbiu yake.
Comments ziwe fupifupi jamani, niko nawasubiri wanaume wa jf
shunie.........
 
Kweli jukwaa la intelijensia kwa kiasi kikubwa kuna unafuu. Ila kwani siasa ni lazima matusi? Hatuwezi kufanya siasa safi zisizo na matusi na udhalilishaji wa utu wa watu ambao ni kaka,dada,mama,baba zetu pengine hata babu na bibi zetu?
Inategemea majukwaa yapi utakayoingia ama utakayowasilisha mada. Kwa mfano ukiingia Jukwaa la Siasa kubaliana na yote tu. Au Jukwaa la MMU nayo kubaliana na yote tu.

Ila Jukwaa kama la Intelijensia, Jukwaa la Kimataifa na mengineyo yanayofanana na hayo yapo tofauti. Sababu kuu kule kunahitaji nguvu ya hoja yenye vidhibiti, na vilevile masuala ya kule yanahitaji ufuatiliaji na usomaji. Usipokuwa nayo hayo ni ngumu kuchangia.

Ila nakuunga mkono. Ujinga upo mwingi sana! Pendelea kutembelea "Nyuzi" za zamani zina mengi ya kujenga ikiwa ni mwenye uhitaji.

Mbali na yote, pole! Karibu Jf.
 
Hahahaaaa!! Shukrani sana mama, wewe ni kati ya members ambao nimekuwa nikivutiwa sana kusoma mada na comments zako hata kabla sijawa member. Sikufahamu ila kiumri unaonekana u mtu mzima kidogo au kama sio hivyo basi umekulia familia yenye maadili mema.
bora umpambe hivyo hivyo, usije ukatereza kutoa maneno ya shombo kwa faiza foxy
 
Bidadaa, humu ndan usiuumize kichwa sanaaa.

Mimi na ID kibao.

Saa ingine ID moja naigiza Jeuri jeuriiii.


ID ingine nakua bonge la Mume mwema.

Hata ivo Sijaoa, MD sijaajiliwa serikalini, nmeajiliwa Hosp Binafsi hapa Bongo

Umri wangu hata sijafika 30

Nina kakitambi fulan ivi kakijinga

Mweusi kama Lamiii

Vimacho.vidogoooo



Karibu tuyajenge Lavu
Uzuri ni kuwa hata ubadilike badilike vipi, basi uhalisia wako bado uko katika hizo id. Ukiona una tabia chafu chafu na unaigiza tabia njema basi tambua unatamani kuwa na tabia njema. Then acha kuigiza maana ukiigiigiza tabia fulani kwa muda mrefu inageuka kuwa tabia yako.
 
Hii ni platform kubwa sana ukienda play store utakuta ipo downloaded na 1M+ sasa hapo kwa idadi hio lazima msafara wa mamba na kenge wawemo ndani since watu wametoka sehemu tofauti tofauti na malezi pia vile vile tofauti hivyo uki generalize kua wote tupo kama unavyodhani utakua unakosea sana
 
Back
Top Bottom