Dada hii JF ime include watu wa rika tofauti tofauti, nyadhifa tofauti tofauti, elimu tofauti tofauti, tamaduni tofauti tofauti, malezi tofauti tofauti n.k
Kwahiyo unaposema wanaume wa humu unakosea, labda useme baadhi ya wanaume wa humu.
Ujue humu kuna mawaziri, wabunge, wanasheria, maaskofu, wachungaji, mashekhee na watu wengine wengi ambao wanaaminiwa katika ambao pia ni wanaume na pia ni members katika hili jukwaa.
Pia tambua kuwa asilimia 90 ya members humu tunatumia ID fake, wapo wanaume wanaotumia majina ya kike na pia wapo wanawake wanaotumia majina ya kiume, hivyo kutambua jinsia ya mtu humu sio rahisi wakati mwingine.
Utofauti wa mwanaume na mwanamke ni jinsia tu katika hali ya kawaida, sio akili wala uelewa.
Ila kiimani kuna tofauti kubwa kati ya mwanamke na mwanaume. Kwasababu Mungu alimuumba mtu mmoja tu, ambaye ni Adam ambaye pia ni mwaume. Kutokana na Adam ndo akatolewa Eva/Hawa(ambaye ni mwanamke) katika ubavu wake.
Hivyo unapomtaja mwanaume uwe makini.