Wanaume wa JF mna shida gani?

Wanaume wa JF mna shida gani?

Jifunze kutumia neno "Baadhi"... Nawe sijakuona tofauti na hao unawaokosoa, umetanguliza hasira,.. Ungetangulia kutumia heshima na hekima tofauti na hao uliowananga, uzi wako ungekua bora sana,.. Ila nawe malezi na elimu yako inafanana na wao... BAADHI ya wanaume!
 
Kusoma ni kuelewa, kuleta jockes na kutokuwa serious sidhani kama inamaanisha kutukana.
Kuna majukwaa ya kufanya hayo na walaa hautoonekana mpuuzi. Ila kutukana kunabaki kuwa jambo lisilokubalika hata kama unadai uko kwenye jockes.
Possibly, kuna wanawake wanatamani kuwa wanaume...lakini kuwa mwanaume haimaanishi kuwa stiff all the time to what you're doing, ndio maana kuna jokes za apa na pale, hivyo mahali kama hapa ndio watu wanaona ni sehemu ya ku relax. Sio vyema kumlazimisha mtu awe kama unavyotaka, kila mtu ana life style yake na ana approach yake ya ku handle mambo yake. Otherwise, huyo bado binti na hawaelewi vyema wanaume walivyo.
 
Nimekuwa mfuatiliaji wa huu mtandao not so long, mwanzoni sikuweza kujiunga kwasababu sikujua namna ya kufanya hivyo. Baadae nikikutana na mtu ambae pia ni mtumiaji wa huu mtandao ndio akanipa ABC's za namna ya kujiunga.

Nilikuwa naiona kwenye suggestions ninapogoogle jambo, nikavutiwa nao sana. Ila nikajikuta nakuwa msomaji tu na nilitamani sana kuwa mmoja wa members humu. Hatimae nikafanikiwa.
Nilijiunga na nikaendelea kuwa msomaji tu hadi hapo nilipoamua kuwa mchangiaji pia. Ila nilivutiwa sana na jukwaa la MMU na CC.

Kwa muda wote nimekuwa nikishindwa kuwaelewa members wa kiume wa humu ndani. Ni wako na tatizo gani? Ni malezi mabovu,stress,kukata tamaa,elimu duni(nieleweke sio ya darasani tu) au tatizo ni nini haswa?

Wengi wao sio wastaarabu kabisa, mtu aweza kuleta mada yake badala wachangie kwa hoja wao ni matusi tu na hii ni hata jukwaa la siasa ambapo ningetegemea kuwakuta wenye weledi na hoja madhubuti kama ilivyo sifa ya mtandao huu(home of great thinkers)
Kuna siku nilileta uzi nikashambuliwa sana kwa matusi, nasikitika niliwajibu kulingana na level yao ya thinking ila i was not proud of it at all.

Hivi nyie binadamu wenye kuitwa wanaume haswa wa humu ni kwasababu gani hamna maadili na hamjielewi?
Hii inatupatia picha wazazi watarajiwa kuwa makini sana na watu tunaotaka wawe baba wa watoto wetu, hivi kama baba wa familia anakosa maadili na upeo namna hii ataiongoza vipi familia yake?

Kuna wakati nikiona mwanaume ana app ya jf kwa simu yake namtafakari sana, namchukulia kitofauti kidogo. Nashukuru mdogo wangu sio member humu.
Wapo wachache atlest ukisoma unafarijika kuona kuwa angalau bado tuna akina baba bora kwenye jamii zetu. Tambueni nyie ni wachache kwa idadi duniani, kwahiyo mnapaswa mjitafakari sana je mnastahili kuitwa wanaume au ni viumbe wenye uume tu?

Kuitwa mwanaume tayari ni jukumu, hivyo tangu ukiwa mdogo unapaswa kukuzwa hivyo. Sasa kama mlipitia malezi mabovu kutoka kwa wazazi its about time dunia iwafunze.
Acheni kujisifia mambo ya kipumbavu, mna jukumu kubwa sana hapa duniani, kumbukeni mlipoteleza kisha mchukue hatua.

Ipeni JF heshima yake kama ilivyo kauli mbiu yake.


UPDATES:
Ukitaka uamini kuwa nililoandika ni kweli tupu bila ya chenga basi soma comments za kwenye huu uzi.
Dah..si bure Kuna kitu wanaume wamekufanya.... https://www.jamiiforums.com/index.php?threads/1610844/
 
huyu Uvelia haijui JF ndo kwanzaa ametumbukiamo humu juzu tu. wacha achemke ndo ataijua vizuri. huu mchezo hautaki mihasira yeye anadhani ni sawa na kule INSTA au TWIT alikojifunzia mitandao
Keshageuzwa geuzwa huyu ndomana analia na jf

Sasa hivi atajua wenzie wanaishije humu
 
Umekosea heshima wanaume wa JF

Ku generalize inaonesha na wewe pia hujielewi, kukoseana na wanaume wawili watatu humu isiwe sababu ya kuwasema wanaume vibaya

Pia elewa kwamba wanaume waliopo umu ndio wanaume waliopo mtaani, pengine hata baba yako pia yupo humu

Mwisho ombi lako linaendelea kufanyiwa kazi (umegusia swala la kupata na baba watarajiwa wa watoto wako), be patient utapata hitaji la moyo wako.
Soma uelewe, wangekuwa wawili watatu maybe tungesema tatizo ni dogo. Ila wengi wenu hamjielewi. Wapo wachache sana wanaojielewa.
 
Na ukitaka ujue kuwa wamefanikiwa ktk hilo angalia ni wanawake wangapi wanao uwezo wa kuwaambia pale wanapokosea zaidi ya wale wa praise and worship team.
Oohh kwahiyo kwa wanaume tu huwa ndiyo iko hivyo ila kwa wanawake huwa mnalazimisha kuwa tuna stress kutokana na hizi hizi comments zetu za humu siyo?
 
Haahaa dada haamini macho yake
Alitegemea watu watamwelewa lakin majibu aliyokutana nayo nyege zote kwishaaaaaa gademiti
Hapana, i was expecting this, ninaamini kabisa maana wengi wenu ndipo uwezo wenu wa kufikiri unapoishia.
 
Wala usipate tabu, soma tu comments kwenye huu uzi. Una majibu yote ya maswali yako.
kwani kina evelyn salt na Money Penny ni wanaume hao?? wapo kifungoni ebu jiulize wamefata nini huko rumande? endelea tu kudhani wanaume tu ndio wenye shombo..

Kuna wanawake physicaly nawajua na wana ID za kiume..wanashombo hata za samaki zina afadhali..we kaa ukituhukumu wanaume tuliojiweka wazi kua ni wanaume..Kuna watu humu wana jinsi mbili mbili,tukisemwa wanaume Anakaa kwa wanawake,wakisemwa wanawake anarudi kiumeni..

Asee member wa JF sio kama wa Insta au badooo...Lawama zako ziweke kwa wote usitaje JINSIA kabisa maana ukiweka jinsia basi usi include wote Mtaje muhusika wako unae mlenga ila kusema "wanaume wa jf" unakosea.

ukitaka kujua unakosea

Nitajie ID 10 ambazo huwajui kwa kuwaona Live(physicaly) ila umewajulia huku JF ambao wewe unasema ni WANAUME...ukiweza taja ID 10 za wanaume nakupa vocha ya 10,000.

Nataka tu ufahamu kuwa JF member wachache sana walio amua kujiweka live kuwa ni ME au KE...wengi wao wanacheza nafasi zote KE na ME.
 
Bora angeleta thread hii mwanaume, yani mwanamke ndo utufundishe ku behave sisi? Wtf
 
Wanawake wengi wanawapiga wanaume kwenye kudanga, huwezi kuona sana JF.

Kuna msemo wa Kiingereza "All is fair in love and war".

Wengine JF bila drama ni kama chipsi bila kachumbari.

Ukitaka kubadilisha JF ni vigumu kuliko kuchunga paka kama ng'ombe.

Pia, ni vizuri uka address specific examples, maana hapa bila specific examples utaweka mtego wa panya unaoshika mpaka panzi.

Naona umeshahukumu wanaume wote wenye app ya JF.

Wakati unaweza kukuta hata wahashamu na wahadhiri wenye staha zao wamo.

Ukiongelea mtu specific, kwa ushahidi specific, hata mimi naweza kukuunga mkono nikijiridhisha.

Ukitoa shutuma za jumla haisaidii, inatengeneza vita zaidi kati ya wanaume na wanawake, unakuwa kama unataka kuzima moto kwa kuumwagia petroli.

Hiyo staha unaionyesha wapi ukiwa kama mhadhiri au mhashamu?
Mfano nimeutoa, pia mfano hai ni thread hii hii.
 
Bora angeleta thread hii mwanaume, yani mwanamke ndo utufundishe ku behave sisi? Wtf
Thread kama hii nishawahi kuona moja kama sio mbili na zililetwa na wanaume, mliwashambulia pia.
Inshort, wengi wenu hamjielewi.
 
Back
Top Bottom