Wanaume wa JF mna shida gani?

Wanaume wa JF mna shida gani?

Wengi funapenda mzaha na kujisikia huru unakuta wengine hatuna marafiki wengi wa mzaha kama humu jf, ila ikija swala la sirias watu huwa sirias si wakati wote watu huleta mzaha
 
Kwahiyo kwenye kusoma kwako kooote haujaona hilo neno?
Jifunze kutumia neno "Baadhi"... Nawe sijakuona tofauti na hao unawaokosoa, umetanguliza hasira,.. Ungetangulia kutumia heshima na hekima tofauti na hao uliowananga, uzi wako ungekua bora sana,.. Ila nawe malezi na elimu yako inafanana na wao... BAADHI ya wanaume!
 
Huku ndio kichaka cha maovu sio?
huyu Uvelia haijui JF ndo kwanzaa ametumbukiamo humu juzu tu. wacha achemke ndo ataijua vizuri. huu mchezo hautaki mihasira yeye anadhani ni sawa na kule INSTA au TWIT alikojifunzia mitandao
 
Eti wanasema ukikaribia kumjua mwanamke ujue nakifo chako kimekaribia. Nahata JF ukikaribia kuwajua member wahumu nini wanataka ujue unakaribia kupigwa ban yamaisha RELAX mrembo
 
Tunaomba fanya analysis pia kwa wadada wa JF,(wewe pia ukiwemo)

Unachopaswa kukumbuka ni kwamba,hao wanaume na wanawake wa JF ndiyo hao hao waliopo mtaani,hawa wa humu hawana dunia yao peke yao!

Kubwa zaidi ni kwamba,katika jamii yoyote,kuna watu wa aina mbali mbali,wapo wenye busara zao,na wapo wenye mizaha mingi,na wapo wajinga wajinga,lakini pia wapumbavu hawakosekani, na hii sio kwa wanaume tu,hata wanawake!

Kwa mfano,tazama mada za baadhi ya wanawake walio wake za watu hapa MMU,wanavyojiachia kuelezea nia au namna walivyotombwa na wanaume wasio waume zao,tena kwa kujisifia kabisa,(hayo ni maadili?)

Kikubwa si kuwalaumu wanaume,tuseme ukweli kwamba kizazi hiki kimepotoka,na shetani amefanikiwa sana kukiponda ponda, namna ya kutoka hapa sio nyepesi,inahitaji nguvu kubwa,ukatili kidogo,na uvumilivu wa hali ya juu sana, vinginevyo kwa siku za usoni,hali itakuwa mbaya zaidi!
 
Ulichoshindwa kujua kuwa humu watu wanatumia fake ID so u can not tell!
Usitake watu wawe seriuos sana,wengine wapo humu kupunguza stress tu!So mind ur business and let go!
 
Nimekuwa mfuatiliaji wa huu mtandao not so long, mwanzoni sikuweza kujiunga kwasababu sikujua namna ya kufanya hivyo. Baadae nikikutana na mtu ambae pia ni mtumiaji wa huu mtandao ndio akanipa ABC's za namna ya kujiunga.

Nilikuwa naiona kwenye suggestions ninapogoogle jambo, nikavutiwa nao sana. Ila nikajikuta nakuwa msomaji tu na nilitamani sana kuwa mmoja wa members humu. Hatimae nikafanikiwa.
Nilijiunga na nikaendelea kuwa msomaji tu hadi hapo nilipoamua kuwa mchangiaji pia. Ila nilivutiwa sana na jukwaa la MMU na CC.

Kwa muda wote nimekuwa nikishindwa kuwaelewa members wa kiume wa humu ndani. Ni wako na tatizo gani? Ni malezi mabovu,stress,kukata tamaa,elimu duni(nieleweke sio ya darasani tu) au tatizo ni nini haswa?

Wengi wao sio wastaarabu kabisa, mtu aweza kuleta mada yake badala wachangie kwa hoja wao ni matusi tu na hii ni hata jukwaa la siasa ambapo ningetegemea kuwakuta wenye weledi na hoja madhubuti kama ilivyo sifa ya mtandao huu(home of great thinkers)
Kuna siku nilileta uzi nikashambuliwa sana kwa matusi, nasikitika niliwajibu kulingana na level yao ya thinking ila i was not proud of it at all.

Hivi nyie binadamu wenye kuitwa wanaume haswa wa humu ni kwasababu gani hamna maadili na hamjielewi?
Hii inatupatia picha wazazi watarajiwa kuwa makini sana na watu tunaotaka wawe baba wa watoto wetu, hivi kama baba wa familia anakosa maadili na upeo namna hii ataiongoza vipi familia yake?

Kuna wakati nikiona mwanaume ana app ya jf kwa simu yake namtafakari sana, namchukulia kitofauti kidogo. Nashukuru mdogo wangu sio member humu.
Wapo wachache atleast ukisoma unafarijika kuona kuwa angalau bado tuna akina baba bora kwenye jamii zetu. Tambueni nyie ni wachache kwa idadi duniani, kwahiyo mnapaswa mjitafakari sana je mnastahili kuitwa wanaume au ni viumbe wenye uume tu?

Kuitwa mwanaume tayari ni jukumu, hivyo tangu ukiwa mdogo unapaswa kukuzwa hivyo. Sasa kama mlipitia malezi mabovu kutoka kwa wazazi its about time dunia iwafunze.
Acheni kujisifia mambo ya kipumbavu, mna jukumu kubwa sana hapa duniani, kumbukeni mlipoteleza kisha mchukue hatua.

Ipeni JF heshima yake kama ilivyo kauli mbiu yake.


UPDATES:
Ukitaka uamini kuwa nililoandika ni kweli tupu bila ya chenga basi soma comments za kwenye huu uzi.

Shida sio wanaume nadhani shida ni WAVULANA hii forum yetu pendwa imeshavamiwa na wavulana au vitoto vya kiume . Nilisha sema JF basi tena tukubali tuu smart phones zilipo anza kuwa bei rahisi ndio haya matokeo. Pole sana dada hakuna namna tena . Wanaume tunatizama tuu pakuchangia tunajaribu basi hivyohivyo.
 
Usiwalaumu sana ndo staili ya maisha afu wa dizain hio ndo wenye market siku hizi kwa wadada
 
Wanawake wengi wanawapiga wanaume kwenye kudanga, huwezi kuona sana JF.

Kuna msemo wa Kiingereza "All is fair in love and war".

Wengine JF bila drama ni kama chipsi bila kachumbari.

Ukitaka kubadilisha JF ni vigumu kuliko kuchunga paka kama ng'ombe.

Pia, ni vizuri uka address specific examples, maana hapa bila specific examples utaweka mtego wa panya unaoshika mpaka panzi.

Naona umeshahukumu wanaume wote wenye app ya JF.

Wakati unaweza kukuta hata wahashamu na wahadhiri wenye staha zao wamo.

Ukiongelea mtu specific, kwa ushahidi specific, hata mimi naweza kukuunga mkono nikijiridhisha.

Ukitoa shutuma za jumla haisaidii, inatengeneza vita zaidi kati ya wanaume na wanawake, unakuwa kama unataka kuzima moto kwa kuumwagia petroli.
Sijasema wanaume wote mkuu, ila ni wengi wao maana najua wapo wanaume wengi tu ambao hawanaga hata muda wa kubishana kuhusu mapenzi na mahusiano wako busy kwenye majukwaa ya siasa na elimu huko.

Mimi nawaongelea wale wengi wao wanaochangia mada za mapenzi na mahusiano yaani hadi kuna wengine nimewakariri maana ndiyo mabingwa wa kubishana na wanawake humu na maneno yao ni matusi na kejeli tu kwa wanawake they always speak ill of women so sijamaanisha wote
 
Back
Top Bottom