Wanaume: Ushawahi kuwa na mwanamke mgomvi?

Wanaume: Ushawahi kuwa na mwanamke mgomvi?

Huyo ndio mwenyewe sasa,mi dem akiwa mtata ndio nampenda kwa sana,huyo usingemwoa angekutana na mimi tungekuwa tumematch kinyama,ukitaka kumuacha niPM mkuu nijichukulie chaguo langu halisia
Haah! Kwahiyo wewe unapenda tu vurumai? Kweli watu tunatofautiana.
 
Huwa natamani sana nipate mwanamke anaejikuta mbabe
 
Wanawake huwa wanatazama Mwanaume wa kuwafanyia upuuzi kama huo, sasa mie uniletee ujinga wa namna hiyo…………nitakunyoosha!
 
Nakumbuka visa Vingi lakini hizi Ndio vilikuwa too much.
1.jirani zetu,
Wote wanyakyusa lakini mwanaume alikuwa anapigwa mpaka anatoka nje kuomba pooh na msaada. Yaani anatoka nje baada ya kujaribu kuzichapa ndani,akiona amezidiwa na anavuja damu kabisa anatoka nje kuomba msaada,wanazichapa mpaka mwanaume anatoka nje yuko uchi kabisa wa mnyama. Tuliamulia mpaka tukachoka wakawa wanaokoa polisi jamii,mpaka mwenye nyumba akawapa notice na mtaani wakatimuliwa Maana mjumbe alisha wachoka na kesi zao kila siku.

2.Shangazi yangu
Ni mkorofi typically,Yaani yeye bila ugomvi kwa siku hajalala vizuri aisee. Anazichapaga na mume wake mpaka mwanaume anazimia. Kuna siku wakawekwa kikao na ndugu wa mume,sasa vile walivyokuwa wanamsema na mume wake akachangia maeno machafu sana,aisee alinyanyuka akaanza kutembeza kichapo kwa mumewe,akakimbilia ndani akamfuata huko huko alipiga mpaka mwanaume akawa anavuta pumzi kama anakufa hivi lakini bado anaendelea kupiga. Baba Ndio alikuwa ana wasili eneo la tukio,alikata nyaya akamgusisha nazo alipigwa na shoti Ndio akaacha.

3. Rafiki yangu,
Alikuwa mtata jamani sijawahi kuona wala Ku image,mzuri na ana msambwanda kama basi la Kilimanjaro. Ilikuwa akianza kuzichapa na bwana ake,mpaka wanakatana nyembe na kushikiana visu,full ngeu kila siku. Siku moja akatuita Mimi na Marafiki zetu wengine wa4,tumsindikize ubungo. Alawasha gari yake tukaingia sisi haoooo to ubungo. Alivyofika akapark,akaenda kugonga nyumbani Fulani wakati Huo na sisi tunashuka. Yule msichana aliyefungua,alivutwa kama mwizi. akaanza kumpa kipondo,alipiga,mwanamke anapigana kama john cena. Akaja kaka wa yule binti,akaingilia ugomvi. Rafiki etu akarudi kwenye gari,kwenye buto alitoa nondo na nyundo,ule ugomvi uliamuliwa na wanajeshi. Maana ilikuwa anapiga watu wawili na anawachakaza.
Nilivunja urafiki nae days ahead,nikawa simpokelei simu wala sijibu Sms zake.

4. Cousin wangu,
Ameolewa toka mwaka 2014. Around 2016 mume wake akawa anachepuka,lakini she is decent and hakuwa anamfuatilia. Na Hata alipo ambiwa mumeo huko Hapo somewhere na mchepuko hakuwahi kumfatiliza.
There is a day yule bwana akajichanganya,akamwambia cousin "Yaani wewe malaya umenichosha,bora ningeoa mama ako" ile siku ni alimpiga sitaki Kukumbuka ni alipiga kwa kiasi gani,akapiga tu simu nyumbani akasema jamani nimeua huku. Tulivyoenda jamaa hajitambui,alikaa ICU mwezi mmoja. Cousin nae akawekwa ndani na ndugu wa mume wake,sababu wakwe walivyofika Wifi mmoja akaleta jeuri aKampa kipigo akachanika mdomo na jicho wakaenda polisi. Mume wake alivyoamka akasema namtaka mke wangu,good thing mpaka Leo wapo pamoja,mwanaume alijua makosa yake,yakaisha. Wakafuta kesi polisi.
Una story za kusisimua
 
Kuna wengine saa zote wanawaza namna ya kutengeneza ukorofi saa zote na kila siku, yupo jirani mmoja karibu kila jirani keshagombana naye na hakuna hata mmoja anayemsikiliza huyu jirani korofi, kwa kweli anaishi kama kisiwa, anajiita mlokole anajua kutukana huyo duuh!!! Sipati picha mwanaume atakayemuoa atavyopata shida....
 
mtu mgomvi unamuonesha kuwa wewe ni zaidi yake
 
hahahahhaha..wee kaa na mwanamke mpole sana!!nyumba inakuwa too boring!!sisemi mgomvi kupindukia!!kila kitu inabidi uwe na kiasi!!Usipunguze wala usiongeze!!Mm kaskazin mkuu
Duuu kumbe mpalestina
 
Dah me ninalo hilo janga aise sijapata kuona msichana mgomvi kama huyu niliye nae, wiki kama mbili hivi zimepita alikuja kunianzishia bonge latimbwili mwanamke aamuliki kosa langu nikumpiga kibao2 ndio ikawa nimechokoza aise yaan nikaamua nimuache afanye kile anachotaka alinikaba shingo maumivu niliyohisi aise nilijikuta nimepiga kelele maana nilihisi kufa nilipotoka hapo kwahasira nilimuuma shavu ila ndio akasara hatar watu wanaamua ila wap mpaka akaja mama yake mtu ataki kuacha ugomvi kanikwida kama vile mwizi mpaka akaja mama yangu mtu bado2 kakaza ikabidi wamuamue kwangu watu wanne ndio walifanikiwa kumtoa ndani naalipotolewa ndan nikaambiwa nijifungie mlango ndani, akawa kazinda mlangoni anatukana hatar anafoka mpaka akazimia hapo hapo mlangoni yaan mpaka sasa anaumwa maana alilazwa kabisa baada yakumpeleka hospital
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji124][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji23][emoji124][emoji124][emoji23][emoji124][emoji23][emoji124][emoji124]
 
Back
Top Bottom