Wanaume: Ushawahi kuwa na mwanamke mgomvi?

Wanaume: Ushawahi kuwa na mwanamke mgomvi?

TAKE THE POINT BELOW:

Yaani hiyo kusema tu "Mdada au Mwanamke anakuonea" kikwetu ni UDHAIFU mkubwa sana.

Mchukulie Mwanamke kama Mtoto mdogo hata akipanic akaliaaa akajigaragaza bado hawezi kuwa na nguvu kukuzidi wewe Mwanaume.

Ndio maana mimi visirani vyao vya masaa kadhaa navipenda tena napenda anililiiie hadi achoke alale mwenyewe.

Halafu sasa walivyo...baada ya muda ukimuahidi kitu ambacho anakipenda au ukimpa kitu ulichomuahidi zamani anasahau na hasira zinaisha.

Mwanzoni nilikuwa sijawaelewa...ila nakuambia wanawake ni kama watoto, hasira zao hazifiki mbali.

M baya ni yule tu mwenye maneno meeengi halafu anapayuka nje au mtoa siri za ndani.

Jitahidi uwafahamu hawa hawatakuumiza kichwa.




u r a real MAN,ila jamani yoooote tisa 10 ogopa mwanaume mwenye GUBU JAMAN,
 
Duh!!!!aisee huu Uzi..
GuDume Dragoon njooni mnipe na nyie za kwenu hapa
hahaaaa.
Nilishakuwa nae mmoja tulipendana sana, lakini hakuwa anataka ninywe pombe mbali na nyumbani. Siku moja nipo mtaa wa mbali kidogo na marafiki zangu tunakunywa na kupiga stori za hapa na pale mara huyu hapa kaibuka bwana. Demu bila hata kusalimia washkaji niliokuwa nao moja kwa moja kanivaa, anauliza huku unatafuta nini? Nilijibu kwa kujiamini.. NIMEKUJA KUNYWA. Demu alininasa kibao hadi nikaona pombe chungu. Washkaji walinyamaza kimya kama hawajaona chochote kile. demu kaniambia twende nyumbani nikagoma katakata. ikabidi aondoke mwenyewe kanuna. Washkaji walinionea huruma sana, wananiambia achana nae yule si demu wa kuishi nae.
Tuliendelea na maisha lakini siku moja nikaamua nimlipizie kisasi. Siku moja nikaenda baa moja kuna mhudumu nafahamiana nae, nikampa mchongo wote. nikachukua simu yangu nikamtumia ma sms kibao ya kumtongoza halafu namwambia hela ipo, nitampa laki tano. baadae nikarudi nyumbani, usiku. nilipofika nikampigia yule mhudumu simu mbele ya demu wangu, nikamwambia cheki sms unijibu ombi langu kabla sijalala. Baada ya hapo nikaacha simu mezani nikaenda kuoga. Kumbe demu kachukua simu kaanza kusoma sms (nilifanya makusudi sababu namjua tabia yake). Nilipomaliza kuoga lile zogo lake siwezi elezea. akawa anasema... YAANI BADALA YA KUFANYA MAMBO YA MAENDELEO UNAHONGA MALAYA HADI LAKI TANO.. NI AKILI GANI HIYO. Majirani walisikia lakini mimi nilinyamaza kimya tu huku miyoni ninafurahia. Alivyokuwa anazidi kuchonga nikazuga natoka nje kumbe ndio nduki.. hadi night club nikakesha wala sikulala nyumbani. Kesho yake akadai anarudi kwao akazani nitambembeleza, nikasema nenda hata mini siwezi kuishi na mtu kama wewe. Huo ukawa mwisho wa mahusiano yetu.

Ebwana eeee! Mungu si athumani nikapata demu mwingine nikajua huyu ndo wa maisha. Hajui kuchuna wala nini, hata buku hajawahi kuniomba. Tatizo la huyu mda wote ukawa ni kulalamika tu. Mtapiga stori za kawaida mkimaliza malalamiko, mara sipendi unavyovyaa, mara marafiki zako wamekuzidi kimaendeleo. Mara sipendi unywe pombe, mara sijui nini. yaani inafikia kipindi siku nzima strori zetu ni kulalamikiana tu. Nikawa isiwe taabu... Nikakata mawasiliano, akituma sms sijibu, akipiga sipokei. Akiibuka gheto nazuga niko mbali nina dharura. ikitokea bahati kanikuta gheto nasingizia naumwa nataka kupimzika. akajishtukia nae kakata mawasiliano
 
Nakumbuka visa Vingi lakini hizi Ndio vilikuwa too much.
1.jirani zetu,
Wote wanyakyusa lakini mwanaume alikuwa anapigwa mpaka anatoka nje kuomba pooh na msaada. Yaani anatoka nje baada ya kujaribu kuzichapa ndani,akiona amezidiwa na anavuja damu kabisa anatoka nje kuomba msaada,wanazichapa mpaka mwanaume anatoka nje yuko uchi kabisa wa mnyama. Tuliamulia mpaka tukachoka wakawa wanaokoa polisi jamii,mpaka mwenye nyumba akawapa notice na mtaani wakatimuliwa Maana mjumbe alisha wachoka na kesi zao kila siku.

2.Shangazi yangu
Ni mkorofi typically,Yaani yeye bila ugomvi kwa siku hajalala vizuri aisee. Anazichapaga na mume wake mpaka mwanaume anazimia. Kuna siku wakawekwa kikao na ndugu wa mume,sasa vile walivyokuwa wanamsema na mume wake akachangia maeno machafu sana,aisee alinyanyuka akaanza kutembeza kichapo kwa mumewe,akakimbilia ndani akamfuata huko huko alipiga mpaka mwanaume akawa anavuta pumzi kama anakufa hivi lakini bado anaendelea kupiga. Baba Ndio alikuwa ana wasili eneo la tukio,alikata nyaya akamgusisha nazo alipigwa na shoti Ndio akaacha.

3. Rafiki yangu,
Alikuwa mtata jamani sijawahi kuona wala Ku image,mzuri na ana msambwanda kama basi la Kilimanjaro. Ilikuwa akianza kuzichapa na bwana ake,mpaka wanakatana nyembe na kushikiana visu,full ngeu kila siku. Siku moja akatuita Mimi na Marafiki zetu wengine wa4,tumsindikize ubungo. Alawasha gari yake tukaingia sisi haoooo to ubungo. Alivyofika akapark,akaenda kugonga nyumbani Fulani wakati Huo na sisi tunashuka. Yule msichana aliyefungua,alivutwa kama mwizi. akaanza kumpa kipondo,alipiga,mwanamke anapigana kama john cena. Akaja kaka wa yule binti,akaingilia ugomvi. Rafiki etu akarudi kwenye gari,kwenye buto alitoa nondo na nyundo,ule ugomvi uliamuliwa na wanajeshi. Maana ilikuwa anapiga watu wawili na anawachakaza.
Nilivunja urafiki nae days ahead,nikawa simpokelei simu wala sijibu Sms zake.

4. Cousin wangu,
Ameolewa toka mwaka 2014. Around 2016 mume wake akawa anachepuka,lakini she is decent and hakuwa anamfuatilia. Na Hata alipo ambiwa mumeo huko Hapo somewhere na mchepuko hakuwahi kumfatiliza.
There is a day yule bwana akajichanganya,akamwambia cousin "Yaani wewe malaya umenichosha,bora ningeoa mama ako" ile siku ni alimpiga sitaki Kukumbuka ni alipiga kwa kiasi gani,akapiga tu simu nyumbani akasema jamani nimeua huku. Tulivyoenda jamaa hajitambui,alikaa ICU mwezi mmoja. Cousin nae akawekwa ndani na ndugu wa mume wake,sababu wakwe walivyofika Wifi mmoja akaleta jeuri aKampa kipigo akachanika mdomo na jicho wakaenda polisi. Mume wake alivyoamka akasema namtaka mke wangu,good thing mpaka Leo wapo pamoja,mwanaume alijua makosa yake,yakaisha. Wakafuta kesi polisi.
namba 1...2...3 bado wapo na hao wanaume wanaowadunda..
 
Back
Top Bottom