Wanaume, tupeni majibu hapa...

Wanaume, tupeni majibu hapa...

Nahisi wanaume kama mimi tumeonewa tu, mie hukiri makosa... hata nikiwa mlevi, mbushi, au nimekamatwa live nina "ndogo" huwa nakiri kosa ili nisamehewe na kupigania baby come back

kungwi kanionea sana

Haya ngoja nirudi pub maana maisha ya useja yalishanishinda
 
gfsonwin sio wote kwa maneno yako ambao huwa hawaombi samahani
Kuna mazingira ambayo kabisa unajiona umeenda mchomo na hukupaswa kusema au kutenda na unaomba msamaha kwa mwenzako
yaweza isiwe ni yale maneno ya moja kwa moja kuwa samahani dear nimefanya kosa ila vitendo vingine vinaashiria kumuomba samahani
Sio kwamba dhana ya ubabe au kuwa mwanaume ndio ikifanye uwe na roho ngumu kung'ang'ania kitu ambacho kabis unajua ni kosa
Mr Rocky mimi bado najiuliza kwanini swala la nisamehe miongoni mwa walio wengi ni gumu? hao wanaofanya hayo ni ubabe ama ujinga?
 
Last edited by a moderator:
Hivi kwanini wenzetu nyie si wepesi hata kidogo wa kukiri makosa yenu na kuomba msamaha? Kwanini mara nyingi huwa mnatafuta means ya kujusfty makosa kuliko kuomba msamaha? je ni ubabe ama ni aibu ama mnahisi kufanya hivyo ni kujishusha hadhi yani kutoka kuwa mwanaume na kuwa mtu mwingine?

je na kwa wale mnaokiri na kuwaangukia wake zenu kwa samahani, je wake zenu wamewahi kubadili heshima yenu ama hata kukudharau?

leo akina mama tukae tuwatupie maswali kwa kila hoja watakazo leta hadi tujue nini ni nini.

nawasilisha.

Je unauliza kuhusu wanaume yaani gender/ sex, au husbands, au boyfirends? Maanake kichwa cha thread wanaume, halafu content waume!

Sababu kubwa ni nature! Naamini tofauti kati ya mwanaume na mwanamke ziko mpaka kwenye brain. Ukija kwenye chromosomes mwanamke hana Y bali ni X tupu na mwanaume ana Y na X!! Sasa yawezekana hiyo Y ina traits ambazo mwanamke hana!!

Ili swali lako lijibiwe vizuri ni vizuri ungetoa mifano halisi kwani yawezekana wanawake hawaombwi misamaha kwa sababu hawajitambui na wala hawatofautishi kosa na sio kosa pia hawafanyi uchunguzi wa kina kuhusu sababu ya kosa la mume, yaani cause!!!!!!!
 
Mr Rocky mimi bado najiuliza kwanini swala la nisamehe miongoni mwa walio wengi ni gumu? hao wanaofanya hayo ni ubabe ama ujinga?

Kama avatar yako ina-reflect your behaviour basi hata mimi kukuomba msamaha kidogo itakuwa ngumu!!!!
avatar80923_7.gif
 
Mkuu gfsonwin na Wakuu wanawake wote naomba kutoa hoja;
Its a matter of leadership ego...we all have it presidents, ward secretaries, fathers, mothers and even brothers and sisters.
Aliye mkubwa kumuomba msamaha mdogo ni kama anaona credibility inashuka! Ndo maana hata madaktari na walimu wagomeje-viongozi hawawezi kuadmit their mistakes(which are many by the way), watatafuta tu kujisafisha kwa justification.

Mimi naamini justification ni mbaya sana ndo maana hata kwenye bible(my fav book.) watu wote walioambiwa dhambi zao wakaanza kujijustify Mungu aliwakataa kabisa! (Ref.. our father Adam, Cain, Saul)

Na waliotubu aliwapenda sana tu hadi kuwatajataja over the generations hata kama dhambi zao zilikua kubwa kiasi gani
Ref David (He comitted adultery, killed the womans husband and married her). Yet akasamehewa.

Inaudhi sana ukimwambia mtu kosa lake anaanza kufanya hivyo...Ila you are our wives so help saving us from the men we have become.

Pai kinadada na wake zetu mnakosea the way mnavyotuaproach na kutuambia makosa yetu. Kama ukimwambia mkiwa wawili chumbani kwa upole ni wachache sana watakaokuwa hivyo (Ambao kwa niaba ya wanaume wote naomba kuwaita mafisadi wa mahusiano.)

Nawasilisha
PetCash so kwa wababa yapendeza wakiambiliwa sirini eeh! ila je mbona sisi hamtufanyii hivyo? haya tumeelewa kwamba nia leadership ego lkn a lida has to be model and not mbabe kwanini nyie wenzetu mnaweka ubabe?

jamani uzuri wanawake wote humu jamvini tu wasikivu sana na hata Asprin na Mr Rocky wanajua hilo mkitumabia mnataka tunapowaambia makosa yenu tuwaambie mkiwaje basi sisi tutatii tu.

pia kuna kitu kimoja huwa kinanishangaza sana, wanaume walio wengi hasa kwenye ndoa siku mkewe akimwambia umekosea basi yeye moyoni husema leo atanitambua kitandani, basi akifika kwa bed yaaani utafikir sijui ndo nini ana kudo kama anakomoa na mkimaliza anasema kabisa tumeshafanya hivi ugomvi hakuna je hii ni halali? eti Bishanga wewe waona ni vyema kufanya hivi kwa mtazamo wako?
 
Last edited by a moderator:
Pole kwa hayo yaliyokukutaSi wanaume wote wako hivyo, Ni huyo Wako Tu PengineMuombee Sana ili awe vile upendavyo maana kwa Mungu yote yanawezekana
mgeni 10, hapa sijiongelei mimi, ila nimejaribu kuleta mada ambayo wengi wanapitia huko. kwa bahati wa kwangu huwa anakiri na kuomba samahani ila tu malipizi yake unakoma na wewe ujitahd usiwe mkosa.................
 
Last edited by a moderator:
Nimeoa au nimeolewa? Ndio sababu kubwa, na mwanamke siku atakuwa kama mtumwa ndani ya ot, my take
 
Kuombana msamaha ni jambo la kawaida kwa wale wanaotambua wajibu wao kwa wengine iwe katika ndoa au nje ya ndoa. Wapo wanawake na hata wanaume wanaoamini kuwa hawastahili kuomba msamaha hata wakijua wamewakosea wengine.

Wapo ambao unalazimika uwachambulie makosa yao na uwaambie wanapaswa kuomba msaada. Mara nyingi utakuta hawa ni wale wenye kiburi na jeuri.

Kuomba au kutoomba msamaha sometimes inategemea na malezi ya mtu, alijifunza nini katika familia yake. Mtu anaweza kukukanyaga kwa mfano, mwengine anaweza kuomba msamaha au hata pole but mwengine wala hajali.
 
Nahisi wanaume kama mimi tumeonewa tu, mie hukiri makosa... hata nikiwa mlevi, mbushi, au nimekamatwa live nina "ndogo" huwa nakiri kosa ili nisamehewe na kupigania baby come back

kungwi kanionea sana

Haya ngoja nirudi pub maana maisha ya useja yalishanishinda

sasa nakukubali kwamba wewe ni mtu wa TIMING manake hii gia ni nzuri sana. infact wanawake tunapendwa sana kupendwa jamani halafu wenzenu siye mkituomba samahani yaani huwa tunaishia nguvu kabisa urgument zote huwa zinatoweka kabisa. yaani huwa tunaweza kujikuta tunalia kwa samahan aliyoisema hubby. na mara nyingi sana wababa sio wakosaji sana, anyway labda ndio maana ni wababa ila inapedeza sana pale wanapokosea kukiri makosa yao.
 
Last edited by a moderator:
na kama moshi unavyoumiza macho ndani ya chumba cha jiko ndivyo ilivyo kuish na mwanaume mkorofi ndani ya nyumba.

Umetafuta chanzo cha ukorofi wake? Je suluhisho ni nini? Kununua jiko la umeme au gas au kuweka chimney?
 
(according to malezi) udhaifu sio sifa ya uanaume so hatutakiwi kuwa nayo. kuhusu mwanamke udhaifu inakubalika maana wao wapo chini yetu (according to malezi)
Blaine we aare neva weak ma dia bro. women are very strong ila tu wababa nyie hamtaki kulikubali hilo. kama huamini mwambiemkeo asafiri ubaki home wewe na watoto ndipo utakapojua what i mean.
 
Last edited by a moderator:
Achika nikuoe uone utakavyostarehe.
Bishanga wewe kweli waweza kuwa na mali na pesa ningi ila upendo wa dhati, kunijali, kunitunza vikawa ni vitu vigumu kwako. mwenzio miye ni chapa kubota lkn kudeka nimo.
 
Last edited by a moderator:
Kwani kuna undugu mzuri kuliko ule? Ushawahi angalia vizuri jinsi mambo yanavyokuwa? We acha tu! Kumbe tuko pamoja kama mpaka sehemu muhimu hatutofautiani

hivi Ndahani kwenye huu uzi unataka kutuambia nini? yaani sikusomi kabisa ama ushapata mwandani sasa hapa unapanga verse za kwenda kumliwazia ukifika home?
 
Last edited by a moderator:
Nani kasema peke yenu hamna shida? Mbona peke yenu ni kama dunia iko upside down? Au ni mimi tu ninao hayo katika mtaa ninao ishi!

ukweli ni kwamba binadam wote tunategemeana ila sasa hakuna mtumwa na mtwana.
 
Kama avatar yako ina-reflect your behaviour basi hata mimi kukuomba msamaha kidogo itakuwa ngumu!!!!
avatar80923_7.gif
teh teh teh teh teh! kumbe hata wewe imekugusa eeh!.............. pole mwaya ndo nilivyo lakini.
 
PetCash so kwa wababa yapendeza wakiambiliwa sirini eeh! ila je mbona sisi hamtufanyii hivyo? haya tumeelewa kwamba nia leadership ego lkn a lida has to be model and not mbabe kwanini nyie wenzetu mnaweka ubabe?

jamani uzuri wanawake wote humu jamvini tu wasikivu sana na hata Asprin na Mr Rocky wanajua hilo mkitumabia mnataka tunapowaambia makosa yenu tuwaambie mkiwaje basi sisi tutatii tu.

pia kuna kitu kimoja huwa kinanishangaza sana, wanaume walio wengi hasa kwenye ndoa siku mkewe akimwambia umekosea basi yeye moyoni husema leo atanitambua kitandani, basi akifika kwa bed yaaani utafikir sijui ndo nini ana kudo kama anakomoa na mkimaliza anasema kabisa tumeshafanya hivi ugomvi hakuna je hii ni halali? eti Bishanga wewe waona ni vyema kufanya hivi kwa mtazamo wako?

GREEN- Okay that is funny! lol!(kwa mara ya kwanza nimetumia lol). That's a display of a man who doesn't get it at all! yani haelewi mwanzo mwisho.

Mwalimu gfsonwin, ukweli huo ni udhaifu on our side ila na nyie mko vizuri sana kwenye art of manipulation and pretending! Yani you have you own ways of getting things done at your favor bila hata sisi kurealize at the beginning
kulalamika, kulia, kusema hampendwi na kudeny marital rights.
How can you explain that behavior?
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom