Jack Daniel
JF-Expert Member
- Sep 23, 2021
- 4,687
- 19,104
Chizi anachekesha kama hatokei kwenu.
Salaam jamiiforum, hope ni wazima na hata wale wagonjwa pole mtapata nafuu.
Kwanza niseme tu Mimi si muumini wa kupost habari za siasa,ila ni mfuatiliaji mzuri wa habari za siasa na nipo karibu mno.
Kunako social networks na sources kibao naona kunatangazwa Kwamba siku ambayo huwa ni sherehe, tukiadhimisha sikukuu muhimu hii Kwa wakulima, eti kutakuwa na maandamano, yaani hii siku ambayo tumezoea ni siku ya maonesho ya vitu mbalimbali, basi kuna kikundi cha watu wachache wanataka kutumia siku hii kuumiza watanzania.
Kwanza nijiweke wazi, Mimi ni mwanachama hai wa chama cha mapinduzi (CCM).
Sikulazimishwa na yeyote kuchagua chama hiki tangu miaka 30 iliyopita, na ni haki yangu kikatiba kuwa na chama nachokipenda kwasababu zangu binafsi.
Si kwamba chama changu hakifanyi makosa ama hakuna mapungufu, lah kuna mapungufu mengi mno,kuanzia kwenye muhimili wa Bunge na mihimili mingine.
Nalimiss Bunge la Spika Samweli Sita.
Nalimiss Bunge la Spika Anne Makinda.
Namiss heka heka za wabunge hawa
Tundu Lissu,
Godbless Lema,
Zitto Kabwe,
Halima Mdee,
Ester Bulaya
Bila kumsahau kubwa la maadui
Freeman Aikael Mbowe.
Wako wengi siwezi kuwamaliza wote,lakini angalau kulikuwa na chachu huku lengo likiwa kupush na kuendeleza gurudumu la taifa Kwa maana nzima ya kuleta maendeleo ndiyo maana Hadi Leo hii naweza sema Rais kikwete ni pekee na ana upekee wake.
Yote kwa yote, kizazi kimebadilika,uelewa wa mambo ni mpana,taarifa zinawafikia wananchi mapema na kirahisi.
Mtu hasubiri tena taarifa ya habari ya usiku ajue nini kinaendelea,ni yeye na vyanzo vyake tu.
Kiukweli nchi imefikia sehemu ambapo mambo mengi yapo na vibaya wananchi hawaridhishwi nayo,Mimi mwenyewe kuna mengi siyakubali,haki imeminywa Kwa namna fulani, nashindwa kuelewa ni nani haswa mwenye kudrive haya yote,
je ni mfumo ndiyo mbaya?
Ni wananchi hatuelewi tunataka nini?
Au mitandao inatupeleka haraka kuona yale yanayoendelea kwenye nchi za wenzetu tukiona na Sisi tunaweza kuyafanya?
Kwangu MAANDAMANO ni HARAMU.
Zipo njia nyingi za kufikisha malalamiko Kwa serikali si lazima maandamano,si lazima kuandamana.
Je, watanzania ni wepesi kusahau kiasi hiki?
Hata mwaka hatujafika tangu zitokee ghasia mbaya na zenye huzuni zilizoacha maumivu na machungu Kwenye mioyo ya watu.
Polisi na Askari wote ni binadamu na ni watanzania, mara nyingi wanafanya kazi Kwa Amri si Kwa matakwa yao,kila wanalofanya lipo kisheria kama itifaki inavyotaka.
Lakini kutoka pande zote za Tanzania Polisi wengi tu walikufa October 29 2025,Polisi waliharibiwa miradi na nyumba zao,
Huwa najiuliza kila siku Polisi Wana makosa gani?
Kwakuwa kuhakikisha usalama wa Raia na Mali zao ni jukumu Lao na ikiwa kuna mwananchi ataleta ujeuri huwa kuna nguvu lazima itumike.na hili lipo wazi.
Kabla hujaandamana fikiria haya....
Ni yupi mtoto au ndugu wa mwanaharakati aliandamana Oct 29?.au aliripotiwa kupoteza Maisha
Yaani mtoto wa Lissu ama Heche,
Yaani familia ya Mbowe ni lini uliwahi kuiona Barabarani.
Maria Sarungi Tsehai,hayupo Nchini
Mange kimambi hayupo Nchini,
Edgar Mwakabela (Sativa)kijana mwenye laana maana matusi ambayo huwa anatukana sidhani kama ana akili ya kawaida.hakai hapa.
Onesmo Mushi hakai hapa.
Rachel Dangwa (mjaa laana)hayupo hapa.
Wapo wengi ambao wao hulipia gharama za internet na kuwapigia simu familia zao kuwaasa wasitoke huku wao wakiwasiliana Kwa njia za mitandao ,wakiwa sebuleni na vyumbani mwao,wakikuangalia wewe kupitia TV zao ukibeba sululu na tairi ukichoma vituo vya mafuta,ukichoma vituo vya Polisi huku wakitikisa vichwa Kwa lengo Lao huwa limekamilika.
Maandamano yapo Kwa mujibu wa katiba na ni haki ya mwananchi kuandamana ikiwa ni sehemu ya kufikisha kero.huku mkiwa na mabango yanayosomeka. Vizuri nini mnataka.
Yaani uvunje duka la simu la mtu si la serikali,Polisi akuangalie.
Uchome kituo cha Polisi wakuangalie,
Uchome gari la mtu watu wa usalama na vyombo husika vikupigie magoti,Kwa kukuogopa au.
Kwasasa Mimi mwenyewe nipo upande wa serikali,yeyote mwenye kuleta harufu ya uchochezi, lazima ashughulikiwe,maana ni MHAINI
Tuwe na subira mbona maisha yanaenda freshi tu yaani ukosee mwenyewe life style kisha uisingizie serikali.
Hesabu zenu ni mbovu , Idara ipo makini imejipanga vyema Kwanza hakuna mtu mwenye akili timamu atawaelewa,wajinga kama nyinyi ambao mnaiminishwa ujinga mnakubali,kazi yenu kulinda nyeti zisiibiwe, yaani unaamini ukiguswa bega nyeti zitapotea.
Halafu hapo hapo eti unataka mabadiliko,kupitia uvunjifu wa Amani acheni ujinga