Wanaume tuoneeni huruma dada/mama zenu

Wanaume tuoneeni huruma dada/mama zenu

Sio akili zangu ni za aliyekimbia. Pole kwa kukimbiwa. Nxt tym jitahidi uwe mwaminifu.
Last thing, avoid creating doubts.
Acha wenge la ku attack watu, aliyekwambia nimekimbiwa nani? Umeiona thread yangu yoyote yenye kulalamika kuwa nimekimbiwa? Sasa kwa taarifa yako hata ikitokea siku nikakimbiwa watoto wangu wote naweza kuwamudu kwa kila hitaji lao kuanzia school fees,mavazi mpaka chakula na malazi, lands watakachokosa ni upendo tu wa baba! Usichukulie poa watu Mkuu
 
Shida sio mtoto na sidhani kama mwanaume anapenda kumtelekeza mtoto wake.tatizo na chanzo kikubwa ni nyuma ya pazia kati ya mama na baba..wake zetu wa siku hizi waliopitia mambo mengi hawajui kuishi na waume zao.ikumbukwe mtoto huyo hutumika kama kimvuli kumlaumu mume.sasa dawa sio kutumia mtoto ktk lawama bali ukikubali kuolewa basi kubari kubeba jukumu la kujenga amani na upendo bana ya mama na baba.sio ombi ni lazima kwa faida ya mtoto.
 
Mzigua90 . tatizo hapa ni kubwa sio kama unavyolizani.
mfano, mwanamke uliyekuwa unaishi naye mkawa na watoto kadhaa, baada ya muda hali ya maisha imebadilika hajashindwa kuishi bali mnaanza kubana matumizi. yeye anabeba anataifisha biashara chache mlizonazo,anakimbilia kujificha uswahilini kakodi/kakodiwa na wanaume,watoto kapelekwa kwao yeye aniishi kivyake huko uswahilini na wanaume anaowajua yeye.

miezi mitatu ya mwanzo ukipiga simu anatukana tu,ukiuliza habari za watoto anatukana muda mwingine ukipiga simu kujua hali za watoto anakupa mwanaume wake akutukane.analewa pombe na mumewe anakupigia simu usiku haongei unasikia sauti ya watu wakifanya mapenzi angali alikuwa mkeo unayeishi naye. watoto hawanyonyi wala hakai nao unamwambia nipe hataki,baadhi ya ndugu ukiwaeleza wanakwambia hayawahusu nimalizane na huyo mwanamke kwamba hawakunituma nimtongoze wala hawakuniita.

baada ya miezi minne anaanza kudai nimpe hela ya watoto,mbaya zaidi hakai nao kawaacha kwa mama,anipe hataki.HIYO NGUVU YA KUMTUMIA MWANAMKE HELA UTAITOA WAPI DADA YANGU? utajiuliza kwa kuwa watoto wako kijijini na wanasoma public school ambapo ada ni chakula kwa mwaka elfu 20,chochote utakachotuma anaweza kukitumia kulewea au kupata vocha ya kukutukana zaidi ndio maana baadhi ya mazingira mwanaume unakuwa atili unaona bora liwa litakalokuwa sio kujidhalilisha. mimi imenitokea mbaya kaondoka na mitaji ya biashara na kaenda kufungua uchochoroni.hapo inabidi hiyo profit alee watoto, hapati faida anipe watoto.haiwezekani basi nakubali kulaumiwa/.
Huyu wako sio mwanamke Bali ni shetani
 
Dada pole sana, lakini nataka kukuambia asilimia 99% ya wanawake mnaolea watoto peke yenu ni matokeo ya ujeuri wenu na viburi kwa wanaume nitakupa mfano hai unaonihusu mimi mwenyewe nilikuwa nikiishi na mdada mmoja huko geita akapata ujauzito na kulazimika kujifungua kwa upasuaji wazazi wake walitaka kuja kumuuguza mtoto wao niliwakatalia kwa kwaeleza kwamba hilo ni jukumu langu wala wasipate taabu mtoto wao yuko mikono salama alifanyiwa upasuaji na kupata mtoto wa kiume na nililala naye wadi ya wanawake hospitali ya mkoa ya geita kuanzia Jan 22 hadi 24 2014 baada ya kutoka hospitali nilimpeleka Guest na kumuwekea akina mama wawili wa kumhudumia kwa muda wa siku 14 ndipo aliporudi nyumbani na huko nyumbani alikuwepo mtu wa kumsaidia kufua na kupika. Baada ya afya yake kuimarika nilienda Moshi kwenye mihangaiko yangu na nikawa namtumia fedha kila wiki 50,000/= na alikuwa akizitolea kwa wakala aitwaye samweli karibu na classic kwa wanaoijua geita laikini kila anapotumiwa fedha hulaumu kwamba fedha ni kidogo mimi naponda raha tu na wanawake wengine jambo ambalo lilinitia hasira kwa kuzingatia fedha naipata kwa ugumu lakini anyeitumia hana shukrani roho yangu iliumia sana nikaamua nimtumie 150, 000/= aje Dodoma kwenye nyumba yangu ili tupunguze gharama za malezi na kodi ya nyumba baada ya kutuma fedha zile alianzisha tabia ya kusingizia mtoto anaumwa hawezi kusafiri mpaka mtoto apone nikipiga simu hospitali kama mtoto kapelekwa hapo naambiwa hakuna mtoto mgonjwa mwenye jina la mwanangu baadaye ikagundulika fedha anatumia na vijana kwenda kwa waganga ili niendelee kumpa zaidi.

Nilimsubiri Dodoma kwa wiki mbili nzima hakuja nami muda wa kukaa hapa ulikwisha kwa amujibu wa shughuli zangu na siwezi kuacha ufunguo wa nyumba kwa jirani wakati ninaye msubiri hana nia ya kuja na zaidi ya yote huku ni mgeni nyumba bila mwenyeji huwezi ingia bila maelekezo fulani ya kijamii. Nilimtaarifu baba yake mzazi ambaye ni William Sunja Mwalimu Mkuu shule ya msingi msemembo Manyoni kuwa "Kwakuwa mwanaye alikuja geita kunifuata mimi na si mwanaume mwingine yeyote na kwamba hakuwa na mwenyeji mwingine tofauti na mimi pamoja na kumtumia nauli bado ananiwekea masharti ya kuja kwangu maana yake ana mwenyeji wake mwingine kule hivyo toka dakika ile binti yake hayuko mikononi mwangu tena na asije tena dodoma nafasi yake haipo tena siwezi kupoteza kumsubiri yeye wakati yeye ndo ananitegemea na mimi ndiyo mkuu wa familia ninayeratibu familia yangu iishije na wapi tena hana kitu cha msingi anachofanya huko kitakacholeta mafanikio katika familia.

Matokeo yake aliuza vitu vyote kule vyenye thamani kubwa zaidi ya 25Mna kuondoka na mwanaume mwingine na mpaka leo anaishi naye huyo mwanaume na amezaa naye, cha ajabu ni kwamba baada ya mwaka mmoja ananiomba fedha ya matunzo ya mtoto hivi hapo hata kama una matope kichwani fedha unatoa kwa ajili ya nini na unampa nani kama siyo kutafutiana kesi za mada bure lakini bado kana kwamba hilo halitoshi mtoto kabatizwa bila mimi kuambiwa sasa kwa maelezo hayo mafupi ninakuthibitishia kuwa dharau zenu huwaletea majanga siyo la kulea mtoto peke yako hata mengine yasiyowezekana kuandikwa hapa. KAMA NI HIVYO BASI AMALIZE KILA KITU YEYE NA BABA YAKE LABDA NDIYO BABA WA HUYO MTOTO MAANA MZEE ANA SAPOTI UPUMBAVU WA BINTI YAKE. MTOTO ATATESEKA KWA UJINGA WA FAMILIA YA MAMA YAKE.
Pamoja na yote, kamuokoe mwanao kaka! Nenda tu ikibidi mchukue umsomeshe boarding school ili ajikwamue na ujinga wa mama yake
 
Nakupa Pole sana Dada, lkn na mimi nimeachiwa mtoto na mama yake wakati ana mwaka mmoja. Leo mtoto anakimbilia kutiza miaka saba hajui mwanae yukoje, anaishije, kwa hiyo hii tabia co kwa wababa/na wakaka hapana mpaka wanawake wapo wenye tabia hiyo. Kwa hiyo tumuombe M/Mungu atuondoshe na hali hiyo, kugombana kwa baba na mama kusigeuke mateso kwa mtoto.
 
Acha wenge la ku attack watu, aliyekwambia nimekimbiwa nani? Umeiona thread yangu yoyote yenye kulalamika kuwa nimekimbiwa? Sasa kwa taarifa yako hata ikitokea siku nikakimbiwa watoto wangu wote naweza kuwamudu kwa kila hitaji lao kuanzia school fees,mavazi mpaka chakula na malazi, lands watakachokosa ni upendo tu wa baba! Usichukulie poa watu Mkuu
Poa mkuu.
 
Nashauri dada zetu muwe makini coz hili jambo linaumiza lakini msipende kujiachia kwa kila mtu.. inatakiwa mfahamu ya kwamba si kila fundi mhashi ni mjenzi...waweza kuta hata kwake hamna zizi la fito.... na ninyi madume punguzeni munkari... tafuteni njia mbadala kama mazoezi nk nk...
 
Pamoja na yote, kamuokoe mwanao kaka! Nenda tu ikibidi mchukue umsomeshe boarding school ili ajikwamue na ujinga wa mama yake

Ahsante kwa ushauri labda nikuombe uwe peacemaker uende kule uongee na yule mzee mjinga anayeng'ang'ania mtoto wa mtu mwingine utadhani kamzaa yeye maana mimi nikienda akileta za kuleta nawezafungwa bure namuomba Mungu aninusuru kwa hilo sijaficha jina wala kijiji na hii ni habari ya kweli sina kinyongo na mtoto ila wao wanamtumia kama fimbo na kitega uchumi hata mwanaume aliyezaa naye kwanza walikataa asimchukue mtoto wake na wamembadili jina anaitwa ubini wa babu yake utadhani huyu binti kazaa na baba yake mzazi!!! NAOMBA MSAADA WAKO
 
Mbona mie nliachiwa mtoto wa Miezi 6 Kisa mamaake amepata Dili la kazi Uarabuni na Mwisho wa siku haikuwa Dili bali ni Mwanaume wake wa Zaman alirudi kupasha Kiporo..
Sasa na sisi Wanaume tukamlilie nani.? Au na sie Tutoe laana kwa wakina dada/mama wenye matendo haya.? Hili Tatizo lipo kwa Jinsia zote tu.
Waswahili wanasema Toa mwiba wa takoni ili ukae chini uweze kutoa wa kwenye Unyayo

Wew Futa matako tu dadaake usonge Mbele kosa moja katika hatua za Maisha zisifanye Uchukie na Kuwalaumu Wengine wew samehe kuza mwanao Yale maumivu na Uchungu yafanye kuwa ni Upendo juu ya mtoto wako Mkuze aweze kuwa Gentleman. Ili asije kuvaa Viatu vya babaake mwisho wa siku Lazima yote yatimie yaliyo andikw kwenye Torati By the way Pole sana
 
Ahsante kwa ushauri labda nikuombe uwe peacemaker uende kule uongee na yule mzee mjinga anayeng'ang'ania mtoto wa mtu mwingine utadhani kamzaa yeye maana mimi nikienda akileta za kuleta nawezafungwa bure namuomba Mungu aninusuru kwa hilo sijaficha jina wala kijiji na hii ni habari ya kweli sina kinyongo na mtoto ila wao wanamtumia kama fimbo na kitega uchumi hata mwanaume aliyezaa naye kwanza walikataa asimchukue mtoto wake na wamembadili jina anaitwa ubini wa babu yake utadhani huyu binti kazaa na baba yake mzazi!!! NAOMBA MSAADA WAKO
Kurahisisha hili nakushauri Nenda ustawi wa jamii wa wilaya husika, hapo wataku direct kwa afisa ustawi wa jamii atakayeshughulikia tatizo lako mpaka ngazi ya kijiji waliopo,eleza tu ukweli na dhamira yako wao watakusaidia zaidi
 
Pole sana, wanaume wengi wa sasa usharobaro umezidi ni Kazi ya kunyoa viduku na kukataa mbele za wenzao kwamba wanawatoto. Ni maana ya kuruka mkojo halafu mguu unaenda kwenye mavi
 
Kurahisisha hili nakushauri Nenda ustawi wa jamii wa wilaya husika, hapo wataku direct kwa afisa ustawi wa jamii atakayeshughulikia tatizo lako mpaka ngazi ya kijiji waliopo,eleza tu ukweli na dhamira yako wao watakusaidia zaidi

AHSANTE DADA NITAZINGATIA USHAURI NA MAELEKEZO YAKO.
 
Pole sana Dada yangu kwa tatizo hill,na mm nitoe wazo kwenu Dada zangu kuweni making mnapokutana na wanaume ,wachunguzeni kwanza,msikurupuke kukutana nao kimwili kisa vishawishi vya pesa na Vito vya thamani,wengine wanatamani tu wawapate watimize Baja zao na kuondoka, najua no vigumu sana kumtambua mwanaume mwenye mapeenzi ya dhati na asiye na mapenzi ya dhati,kikubwa msipende kujilahisisha sana ,ukimpata MTU kaa nae kwanza kabla hujakutana nae ili ujue kama anania nzuri au in mwongo....pole juu hilo pambana na naamin mungu atakusaidia

Sent from my TECNO-Y4 using JamiiForums mobile app
 
Alafu kingine wanawake wengi hawaoni thamani ya mwili wao,kwa sasa wanacho angalia ni pesa kwanza mwili badae,then yakitokea hayo tunaombeana mabaya, hebu jaribuni kuthamini maisha yenu na miili yenu ,pesa zipo tu japo maisha ni magumu lakini alichokupangia mungu binadamu hakipangui.

Sent from my TECNO-Y4 using JamiiForums mobile app
 
Pole mdada.

Huyo alikuwa ni "mume wa mtu" aliyekuingiza chaka.

Msiingie kwenye mahusiano kichwa kichwa bila kuwachunguza patina wenu.

Ni hilo tu.
 
Kidhungu chako hakika kinahitaji alignment. Next time ukiongea name mwanao ongea naye Kiswahili maana utamchanganya mtoto.
Na watoto wanaamini Daddy can never go wrong...
tehe..tehe..Nilichokiandika ni maisha halisi huku tuliko sio kwa kukosea
 
Back
Top Bottom