Wanaume tuoneeni huruma dada/mama zenu

Wanaume tuoneeni huruma dada/mama zenu

Jitathmini nawe kwanza uone umechangiaje kwenye hilo. Uliolewa alafu akakukimbia kwenye ndoa au mlipeana mimba za kimazoea?
 
Acha kuhukumu usichokijua. Namtesa ulikuwepo? Hata kama nilimtesa kwani si mimi ndio nilimtesa mtoto anahusika nini?
Kwa mambo aliyonifanyia baba yake ni bora asingekuwepo ningemuelewa.
Tatizo tunahukumu upande mmoja na kwa vyovyote utamkandamiza. I wish ningemjua ningemleta hapa aeleze upande wa pili wa shillingi na ungekimbia hili jukwaa nina uhakika. Kama hutajali nipe simu yake katika PM nilete mrejesho hapa!
 
WANAWAKE WANA MATATIZO SANA

wakati nakuwa nilikuta wazazi wangu wametangana
Nikapata malezi ya upande mmoja ambayo ni ya mama
Kwa kiasi flani mama alijaribu kunijengea chuki dhidi ya baba.........
Na kweli alifanikiwa nilimchukia sana baba
Nikajiapiza katika maisha yangu sitakuja kuruhusu mwanangu apitie maisha niliyopitia........
Mwaka jana mwezi wa nne nilifanikiwa kumpatia ujauzito mwanamke ambaye nimedumu nae katika mahusiano kwa zaidi ya miaka mitano na niliamini ange kuwa mke wangu siku moja
Mkasa ukaanza wakati wa huo ujauzito nimetukanwa matusi ambayo sikuwahi kutukanwa kabla na sitakuja kutukanwa tena
Wazee wakaniambia yamkini mimba yake imekuchukia ishi nae kwa umakini sana............
To shorten story jana kanizalia mtoto wa kiume lakin sina hamu ya kumuona huyo mtoto sina mapenz nae amenitoka moyoni kutokana na maneno machafu ya mama yake
Nilipopata taarifa kajifungua nikamtext kumpa hongera lakin jibu nililopewa lilifanya niamini kile nilichokuwa nakiamini enzi akiwa mjamzito
NB; Nilijitahid kumsupport financially licha sikuwa nikiishi nae
Wengi wako vile na Mzigua90 ni vile vile asikudanganye. Ona majibu yake anavyojibu ni ghaleghale tu
 
Pole dada najua unapopitia ni pagumu ila jipe moyo utavuka, mwenyewe ni mhanga ila nishazoea maisha yanaendelea mtoto anasoma yeye laana inamla
 
Nikiwa kama mhanga wa mwanamke alieachiwa matunzo ya mtoto bila msaada wa baba naumia sana.
Hivi wanaume huwa mnawaza nini mnapotupa adhabu ya kulea watoto peke yetu na wewe baba ukiwa hai na unajiweza? Hata kama hujiwezi basi kumjali mtoto wako japo kwa kuulizia maendeleo yake mtu anashindwa kabisa. Hivi kina kaka mmejiuliza nyie baba zenu wangewakimbia mngekuwa wapi sasa hivi? Mnajua ni chuki gani mnaweka kwa watoto wenu mliowakataa? Mnajua ni laana gani mnapata kwa Mungu kwa kukataa kutimiza wajibu wenu kama wazazi? Au mnatukomoa kwa sababu mama hawezi kumuacha mtoto wake nyuma hata apate tatizo gani? Labda wewe na mama wa mtoto hamko sawa lakini ile hasira ya ninyi kutokua sawa baba usimkomeshe mama kwa kuacha kumtunza mwanao ukijua unamkomoa mama, pale unaemkomoa ni mtoto wako ambae ulimtafuta kwa mapenzi/tamaa zako mwenyewe.
Naandika nikiwa na uchungu mwingi sana moyoni. Mwanaume usiemtunza mwanao ona aibu na muogope Mungu wako kwa kitendo unachokifanya.
Jiulize ingekua ni dada yako au mwanao ameachwa na mwanaume alee mtoto peke yake ungejisikiaje?
KARMA IS A BITCH. Ukinifanyia mimi leo wakati unao dada na watoto wa kike jua itakuumiza na wew kwa mmoja kati ya hao kufanyiwa kama unavyofanyia wengine.
Baba mtoto wangu nimeshamlilia Mungu juu yako na nina hakika huyu mtoto ulieniachia nimlee peke yangu atanifuta machozi siku moja na utatamani akutambue kama baba yake utakua umeshachelewa.
Kaka/baba zangu baba Diamond akawe mfano kwenu, Obama aliekataliwa na baba yake mwishoni alikuja kuwa Rais wa marekani/dunia.
KWANI LAZIMA KUZAA?
 
Kama umezaa na huwez kulea jilaumu mwenyewe maana ulitakiwa ujiandae namalezi badala yakutegemea mwanaume.ata ivyo siku hizi hii biashara mnasema Haki sawa kwa wote sijui usawa wa kijinsia uku mkiongezea na maneno ya shombo ya " achana na mimi kwani nashindwa nini,namaneno mengine mbovu mbovu ndo yanayoongeza ayo matukio na mnasema bila kujua a man has nothing to loose.Kwaiyo kwakua mnahubiri wenyewe Haki sawa za kijinsia basi na watoto mlee bila kulaumu yoyote.Japo suo vyema watu kukimbia majukum ila naamin madhila mengi kwenye mahusiano yanawakuta wanawake na wanawake wenyewe ndo chanzo cha madhila yao wenyewe.
 
uchepuk uje ulalamike mwenzako ajajianda kuzaa na wewe wew una kurupuka ndo matokeo hayo.
labda kama ni mme wako ndo kakususa basi jua una kasoro
 
Back
Top Bottom