Mimi si shabiki wa hawa wanaoitwa Celebreties sijui ila Ndugu Gadner Habbash huu ni ushauri wangu kwako "Wewe ni kichwa cha ile familia mliolishana agano, daima hakukosekani ups n downs, haijalishi nani kamtosa mwenzake nani kasababisha haya.
Lakini kwa sababu Mama kautangazia umma kile mlichoafikiana ktk kushindwana, ni vema sana ukaruhusu ukweli ukajitetee wenyewe pasipo kufungua kinywa chako wala kuandika lolote limhusulo aliyekuwa mwenza wako. Mume aliyeenda jando hastahili kumjadili mkewe au aliyekuwa mkewe na watu wengine isipokuwa Mme na Mke tu"
Ukimya, utulivu,hekima huufanya ukweli ulinde dhamana yako kama mwanaume.