WANAUME: Nimewainulia mikono!!

WANAUME: Nimewainulia mikono!!

Safi sana

Hawa dawa yao ni hiyo tu

Ukijidai mstaarabu inakula kwako siku sio nyingi!!!!!!!!!

Pongezi nyingi sana za dhati zimuendee Mshkaji huyo....... Mdada alijidai ndege mjanja mwishoni akanaswa kwenye tundu bovu... na hiyo ndo adhabu kutokana na kitendo alichomfanyia BF wake wa zamani.....
 
Hope weekend ilikuwa poaaaaaa........!

Kuna dada mmoja alikuwa anafanya kazi ofisi moja ya Serikali Mkoani Mtwara ila ni mwenyeji wa Mwanza, (Majina, kabila na mahali sio halisi tafadhali) Huyo dada alikuwa mrembo kweli, basi akapata boyfriend wa Kimakonde hapo Mtwara (Tumuite Maneno) Wakapenda hakuna mfano, yaan ukienda ofisini hapo hutochukua muda kusikia habari za mapenzi yake na huyo Boyfee wake, kila mtu alikuwa anatamani kuwa na mahusiano kama ya yule dada.....

Basi kaka mmoja mwenye pesa zake (Tumuite Aman) akawa anamtaka yule dada (Tumuite Tumain) Tumain alimpa za uso, "Ooh mie nina mchumbaangu, tunapendana saaaana na tutaoana siku si nyingi" Aman hakukata tamaa, kila apatapo nafasi ya kuonana na Tumain alikuwa akimkumbusha ombi lake. Kumbuka Maneno hakuwa na pesa kama Aman..... Miaka ikasonga hakuna dalili ya ndoa kati ya Mrembo Tumain na Kaka Maneno, Hatimaye akawa anakumbuka kuwa kuna mkaka anamsumbua sumbua huenda akawa ana lengo la kumuoa.....

Mrembo Tumain akatafuta ni jinsi gani atampata Aman bila Aman kumstukia, kama bahati vile wakati anafikiria Aman naye akawa anarudi kujaribu bahati yake, Ndipo Mrembo Tumain akajaribu kufungua moyo ya kumsikiza Aman..... Aman akaanza na gia ya Ndoa, dah kumbe hapooooo ndipo alipokuwa anapatamani Mrembo Tumain........

Basi Mrembo Tumain akamwambia Aman iwapo wataka kunioa hakuna kufanya mapenzi mpaka siku ya Ndoa... Aman alikubali bila kinyongo akijua kuna mahali ambapo atamkamatia tu..... KIMSINGI AMAN HAKUWA NA NIA YA KUMUOA MREMBO TUMAIN BALI ALITAKA KUMKOMOA KWA KUFANYA NAYE MAPENZI TU KISHA KUMUACHA KWANI ALIKUWA AMARINGIA SAAAANA......

Basi bana, Mrembo Tumain akavunja uhusiano na Boyfee wake wa siku nyingi ambaye walikuwa wakipendana saaaana! Mara akaanza mahusiano na Aman kwa lengo la kutofanya mapenzi kabla ya ndoa. Haya haya ndoaaaaaaa hiyooooo yabisha hodi. Aman akamwambia jiandae twende nikajitambulishe kwenu Mwanza. Tumain akachukua likizo kwa ajili ya kwenda kumtambulisha Aman....

Mrembo Tumain huyoooo akawasiliana na familia yake huko Mwanza kwa ajili ya kwenda kumtambulisha Aman.. Siku ikawadia safari ikaanza Mrembo Tumain na Aman haoooo wakaanza safari kupitia Dar es salaam... Kufika Dar wakachukua chumba, wakalala. Aman akamwambia Tuma mie ndie mumeo mtarajiwa na sasa tunakwenda kwenu kwa ajili ya utambulisho je bado huna imani nami?? Tuma kuambiwa hivyo akaona ni kweli... Wakafanya mapenzi, siku ya kwanza hiyo ikapita, siku ya pili hiyo ikapita na siku ya tatu ndipo wakaanza safari toka DSM kwenda Mwanza. Hapo familia ya Tumain inangoja ugeni wa Mkwe, Basi kufika Shinyanga ile wameteremka kuchimba dawa ndipo mambo yalipoharibika............

Aman na baadhi ya waliteremka kuchimba dawa na kumuacha Tumain ndani ya gari, baada ya muda watu wote walirudi ndani ya gari lakini Aman hakurudi mpaka gari liakaanza kuondoka. Tuma akaingiwa na wasiwasi akaanza kumpigia Aman simu "mbona hurudi na gari linaanza kuondoka??" Aman akamjibu nimepata dharura ila tangulia nakuja na gari litakalo fuata. basi Tuma akaruhusu gari kuondoka... haoooooooo mpaka Mwanza, kufika akakuta nduguze wanamsubiri stand ya Bus. wakamuuliza mbona ulisema unakuja na mgeni yu-wapi???? Tuma akawaambia "kapata dharura ila atakuja na mabasi yanayofatia" Tuma akafika kwao wakiwa na Matumani kuwa mgeni kapata dharua na akishindwa kufika siku hiyo anaweza akafika siku inayofuata asubuhi....

Kesho yake Tuma akampigia simu Aman... Kwani simu inapatikanaaaaaa...... Holaaaaa... piga piga na wewe simu haipatikani, basi Tuma akapiga kwa rafikize Aman, kuwauliza kama wana taarifa zozote, kumbe Aman aliwaeleza mchezo mzima na hao rafikize wakamwambia A-Z.... Tuma alilia sana na kujuta kumuacha mchumba wake kisa kukimbilia Ndoa hewa............. Mwisho wa siku akamaliza likizo akarudi kazini kwa aibu na fedheha sana kwani Aman alitangaza njia aliyotumia kumpata Tuma kiulainiiii tena siku tatu wanabanjuka tu bila tatizo!!!!!!!!

Mpaka wa leo Tumain hajaolewa ni zaidi ya miaka mitano imepita, hakuna hata mtu wa kumtania kuwa anataka ndoa. Boyfee wake wa zamani keshaoa na watoto juu!!!!!!!!!

SAMAHANI KWA KUWACHOSHA WAPENDWA.... HILI LIWE FUNDISHO KWA AKINA DADA.

ILA NA KWA WANAUME JAMANI MSIWE KAMA AMAN LOL!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

pole zake huyo bidada,tatizo uvumilivu wake ndo ulikuwa zero.
 
Pongezi nyingi sana za dhati zimuendee Mshkaji huyo....... Mdada alijidai ndege mjanja mwishoni akanaswa kwenye tundu bovu... na hiyo ndo adhabu kutokana na kitendo alichomfanyia BF wake wa zamani.....
no comment
 
Booooooooonge la ushauri... hahahaaaaaa!!!!! Nakushukuru! :clap2::clap2:
Unajua nini Charminglady huwa nafikiria kwanini kila siku wadada wanalalamika eti "kanitumia halafu kaniacha" ifike wakati tuwe tunasema tumetumiana au tulitumiana kisha tukaachana, hapa mjini hakuna anaetumiwa wote tunatumiana. Ukiambiwa tu kwamba unapendwa na utaolewa baaaasi unaanza nakufanya majukumu ya mke, kwa nini usiumie siku ukiachwa! kwanza wanaume hawapendi mwanamke wa hivyo kwa sababu anaanza kukuhisi unataka kumganda na unaweza ukahamia hata kabla ya ndoa, Jifanye kama huna shida ndoa kivilee. Subiri uone vitendo na si maneno
 
najiuluza baada ya huyu kaka kumpata yule dada kuna nini alikipata akarudi nacho kama ushindi huko mtwara au ni ujinga na ushamba tuu na lazima stile izo ni za kihuni na utazijua tuu mwanamke ukiwa makini.
 
Story imenifundisha WHATER WERE DOING WE MUST REMEMBER OUR AIM. Halafu imekuwa zali kuna mmoja wa Humhum JF Ananisumbua kweli. NGOJA NIMKOMESHE KWA STYLE HIYOHIYO.
 
Ni kweli rafiki, kuna watu wanafanya hivyo na hao ni wanafiki, na mtu kama huyo si wakuoa haijalishi kakupa ama la, mtu anayefanya usaliti kwenye mapenzi si mtu mzuri maana hata kwenye ndoa atafanya vivyohivyo, wazuri huwa hawaishi cha msingi ni kuridhika na uliyenaye madamu mnapendana kwa dhati. Mapenzi ni zaidi ya ngono, kuthibitisha hilo ni pale tafrani litakapotokea seriously, hata hamu ya ngono kwa mwenza wako unaweza usiwe nayo ila kama mko peace utajiskia mhitaji wa tendo kia wakati. Maoni yangu yalilenga wadada wanaojitunzana kumaanisha, hakika wanakubalika na wanaume wenye akili japo wasiojitambua wanaweza kuwakejeli.

Je ni wadada pekeyao ndio wanaotakiwa kujitunza¿¿¿??? Mdada anaweza kujitunza ila sasa huyo mwanaume, anavuwavua hutatamani kusikia kwa masikio wala kuona kwa macho!!!!!
 
teh teh.... mdada katoa papuchi kiulainiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii sijui atarudije kwa jamaa yake wa kwanza sasa

Haezi rudi kwa jamaaake wa kwanza make jamaa ashaoa na watoto juu... Hafai hata kuwa nyumba ndogo ya jamaa!?!
 
Mashetani huwa wanakuwa na uhusiano na mashetani wenzao, sasa kama wewe ni binadamu ya nini kudeal na viumbe ambao si Kingdom yako? Na ukiona hawakupi usingizi kwa kuwainulia miguu yote miwili basi tambua na wewe ni mwenzao.

hilo nalo neno
 
Ni kweli hao ndo kukudume kenya midume miwili imekubaliana kumuoa mdada mmoja na dada kakubali
 
Pongezi nyingi sana za dhati zimuendee Mshkaji huyo....... Mdada alijidai ndege mjanja mwishoni akanaswa kwenye tundu bovu... na hiyo ndo adhabu kutokana na kitendo alichomfanyia BF wake wa zamani.....

Exactly!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kadalikwa sasa akalale nachooooo-kombolela hilo butua mchezo uishe!!!!!!!

Mwanaume mwingine ukijifanya mgumu hata kwa baba yako anakwenda na mali anatoa,akikuhakikishia hayo tu basi umelamba joker na mchezo umeisha.!!!!
Wengine huvikwa mpaka pete ya uchumba , sasa mdada anaringisha kidole chake maskini kumbe ilikua kanya boya lol . Michezo ya namna hii si mizuri kwa kweli .
 
Haezi rudi kwa jamaaake wa kwanza make jamaa ashaoa na watoto juu... Hafai hata kuwa nyumba ndogo ya jamaa!?!

hahahahhahahaaaaa tena Amani hajafanya kama inavyotakiwa... ilitakiwa afanye zaidi ya hilo.... Halafu mbona vile visa vingine huvileti humu?
 
Wengine huvikwa mpaka pete ya uchumba , sasa mdada anaringisha kidole chake maskini kumbe ilikua kanya boya lol . Michezo ya namna hii si mizuri kwa kweli .

Hiyo sio michezo. Ni adhabu... Kumbuka kuwa what goes around comes around
 
Back
Top Bottom