affinitytz
JF-Expert Member
- Feb 10, 2020
- 280
- 1,151
Wasalaam;
Miaka hiyo nikiwa mwaka wa pili chuoni. Dada ambaye tulikuwa naye kwenye group moja akanitumia meseji ni sms haya mambo ya whatsapp hayakuwepo). Meseji fupi tu ''njoo hapa room kwangu, uje na Eddy''.
Kwa kuwa alikuwa kama dada kwangu na vile tulikuwa kwenye group moja la assigmnet, nikamcheki Eddy ba kumwambia kuwa Naima(sio jina halisi) anataka twende room kwake.
Labda nikupe historia fupi ya huyu dada; kwanza alikuwa mrembo na alionekana kuwa hana shida ambazo sisi wengine tulikuwa nazo. Chumbani kwake tu alikuwa na Sony Bravia TV miaka ile kabla ya Singsung kujaa hapa mjini, friji ndogo (japo warden alikuwa haruhusu) lakini pia alikuwa na Laptop latest zaidi pale chuoni sisi wengine tulikuwa na zile Laptop za Dell nzito kwelikweli na simu nzuri miaka ile Motorola zile za RAZR. Kiufupi alikuwa yupo vizuri hata sisi wanafunzi wenzake tuliona kabisa kuwa Naima sio daraja letu ni vile elimu imetukutanisha.
Turudi siku ya tukio sasa, mimi na Eddy tukasogea upande wa hostel ambapo Naima alikuwa anaishi.
Tukafika na kukaribishwa tukiwa tunataka kujua sababu ya kutuita muda huo; tukakaribishwa na juice ya Delmonte sijui kama bado zipo maana wakati huo Azam Fruit hazikuwepo, ukitaka juice aidha ni Delmonte ama Ceres.
Tukiwa tunakata kiu kwa juice, Naima akatuambia kuwa ana ugomvi na jamaa yake na wakati huo jamaa yupo njiani anakuja. Tukashtuka, akaendelea nimewaita mkae hapa na mimi ili asifanye fujo ama walau muwepo hapa.
Nikauliza kwani anajua chumba anachokaa? Naima akajibu Yes, anajua ameshawahi kuja hapa mara kadhaa.
Eddy aliyekuwa mtu wa mazoezi akaniambia '' tukae hapa tuhakikishe usalama wa sister'' nikamwambia poa huku nawaza kama wamegombana jamaa akija si ndio nafasi ya wao kuongea.
Nikamwambia Naima kwa nini asimwambie jamaa wakutane nje ili waweke sawa mambo yao? Naima akajibu kwa tulipofika sidhani kama tutaelewana na jamaa ana hasira sana.
Nikaona hapa naweza pata jeraha kwa ajili ya mapenzi ya watu, nikamwambia basi amwambie mlinzi ili amzuie jamaa kuingia upande wa hostel. Kabla Naima hajajibu, mlango ukawa unagongwa; Eddy akainuka huku akiwa amekunja sura na kufungua mlango.
Nikaona mlinzi wa hostel huyu alikuwa anaitwa Chigaga, nyuma yake kuna vijana wawili. Chigaga akamwambia Naima una mgeni wako hapa nje, Naima akainuka na mimi sasa nikaona ndio wakati wa kuonyesha kuwa naweza kuwa na msaada.
Chigaga akasogea ndipo nikamwona jamaa umri wa kati kidogo, shati safi, suruali ya kitambaa na alioneka kuwa mtulivu.
Kabla ya salamu jamaa akamwambia Naima ''Nimefuata vitu vyangu''
Nikaona Naima anamwambia ''kwani si nigekuletea mpaka uje hosteli''; jamaa akawageukia wale vijana wawili na kuwaambia ''beba friji, beba TV, beba laptop, beba na hilo begi la pinki.
Mimi Eddy tukabaki kama wasimamizi wa uchaguzi, tunakodoa macho tu maana yule jamaa alijifanya kama hatuoni kabisa.
Nikamtazama Naima naona anaanza kuwa mwekundu usoni na jasho linamtoka, huku akiwa anatoa maneno nusunusu.
Chigaga naye akawa anawasaidia wale vijana kubeba mizigo.
Jamaa akaingia ndani na kufungua kabati na kuanza kuchambua nguo, akamaliza zoezi na kuwaambia vijana zake beba na hizi.
Nikajua zoezi limeisha, jamaa akamwambia Naima naomba na hiyo simu pia. Hapo sasa Naima akaanza kulia na kusema ''Mwanaume hauna ustaarabu kabisa na una roho ya kimaskini sana''
Jamaa hakuongeza neno, akasogea mezani, akatoa line (Kipindi hicho zile Line Kubwa kabisa) akaweka line mezani na kugeuka kuanza kuondoka akiwa na vijana wake wawili na Chigaga pembeni.
Sisi sasa Special Force mimi na mwenzangu hakuna kitu tulifanya zaidi ya kuwa mashuhuda tu.
Tukampa maneno ya faraja dada Naima na tukaaga huku tukiwa vichwa chini. Mission failed.
Siku ya pili nikamfuata Chigaga na kumuuliza mbona kama alikuwa upande wa jamaa? Chigaga akaanza kuniambia kwamba yeye alikuwa anahakikisha usalama tu; hapo nikacheka kwanza, nikamdodosa akafunguka kwa alilipwa na jamaa 15,000/- ili asaidie kwenye kufanya zoezi la kurudisha mali liwe rahisi. Lakini pia akaendelea kuwa jamaa anamjua kwa sababu mara kadhaa huwa anamfuata Naima na gari hasa weekend, kiufupi ndio jamaa yake. Na kilichotokea ni kwamba dada ana mpenzi mwingine; kwa hiyo jamaa amejua ndio maana amekuja kufuata vitu vyake kwa kuwa mapenzi yamefikia mwisho.
Maisha na matukio.