Wanaume ni dhaifu na hawajiamini mbele ya wanawake...!

Wanaume ni dhaifu na hawajiamini mbele ya wanawake...!



Hebu ona, hadi leo mwanaume anaweza kuhatarisha maisha yake au hata kupoteza maisha akijaribu kutafuta njia za kumfanya mwanamke amwone kuwa ni wa maana. Atasema uongo, atajikweza, atajifaragua, akitafuta kukubaliwa na mwanamke. Huu ni udhaifu mkubwa na unaonyesha ni kwa kiasi gani jinsia hii isivyojiamini. Udhaifu huu na mwingine ndiyo ambao mwanaume amekuwa akitafuta kuuficha ili mwanamke asiuone, ambapo ameamua kumkandamiza kwa mabavu.

Mwanazuoni mmoja wa utambuzi alipata kusema, wale wanaume wote ambao walijitahidi kuifanya dunia hii kuwa mahali penye kupendeza, walikuwa na tabia ambazo ni wanawake zaidi wanaokuwa nazo. Walikuwa na huruma, upendo, unyenyekevu, kusamehe, kusaidia na kujali. Leo hii mwanaume ukitaka kuitwa mwanamke, onyesha huruma, onyesha upendo, onyesha usamehevu. Unaweza kuona ilivyo, kwamba, bila kuonyesha mabavu manaume anahisi kuumbuka.

Black-Couple-Arguing-pointing.jpg


Kuna wakati tulikuwa tukizungumza na ndugu yangu ambaye alikuwa anatarajia kufunga ndoa. Mmoja kati ya ndugu zangu waliokuwepo alisema, ‘inabidi huyo mchumbako tumuone, kwa upole wako anaweza kukukalia ukimwoa.’ Unaona? Kinachomlinda mwanaume ni kitu kimoja tu, kuwa mbabe na mkali, basi. Hana silaha nyingine na hajawahi kuwa nayo, hivyo akiiachia hii ya mabavu, anajua atakuwa amekwisha……



mh hi mkuu

ni kweli zaidi ya mabavu hakuna kitu bure kabisa
 
Ndugu yangu Fixed Point talking of wadada wenye mkwanja mrefu "kuogopwa" na wanaume hii inatokana na malezi/makuzi au tamaduni zetu za kiafrika, jambo kama hili huwezi kuliona ama kulisikia kwa wenzetu hasa wazungu.

Kwahiyo hili jambo ukitaka kulielewa vizuri zaidi unatakiwa kuliangalia katika dimensio hiyo badala ya kusema tu kwamba hatujiamini kuwatokeo wanawke wenye mkwanja. Kiafrika afrika mwanaume ndiye anatakiwa kugharimia mahitaji yote ya familia yake/mke wake/rafiki yake wa kike. Sasa katika hali ya kawaida basi kila mwanaume angetaka kuonekana yeye ndiye anagharimia mahitaji ya wategemezi wake au mwenzi wake. Sasa ikitokea mwanamke ana mkwanja mrefu basi mwanaume anajihisi kuwa ameporwa mamlaka yake, anajihisi ameporwa haki yake ya kuwa msimamizi wa familia.

Na bahati mbaya pia usisahau kuwa wanawake wengi wenye mkwanja mrefu nao ni matatizo makubwa kwa wanaume na hapo ndipo tatizo la msingi lilipo. Huenda nao wanahitaji kujifunza kwa wazungu ni namna gani wanaweza kumanage mahusiano na waume zao/marafiki zao wa kiume wenye vipato vidogo kuliko wao.

Kuna rafiki yangu wa karibu sana aliwahi kuwa na relation na mwanamke mwenye shahada ya kwanza wakati yeye akiwa na FTC na walikuwa wanakwenda vizuri tu almost miaka minne hivi lakini mara tu yule mwanamke alipohitimu shahada ya pili wakashindwana kabisa baada ya mwanamke kubadilika na kutoonyesha kumheshimu tena mshikaji na hakutaka aulizwe chochote na bf wake na jamaa yangu hakutaka kunyanyasika kwasababu ya elimu yake hivyo uhusiano ule ukavunjika. Katika relationship kunakuwa na tabia ya "possession", mwanaume anataka kum-possess mwanamke na mwanamke anataka kum-posses mwanaume. Sasa hapa ndipo palipomshinda bibie na shahada zake mbili hakutaka aonekane yuko chini ya himaya ya kijana wa FTC!!!

Kwahiyo kwa ujumla suala hili linachagizwa zaidi na mila na tamaduni zetu waafrika kuliko kitu kingine chochote na hili linawahusu watu wote wanaume na wanawake.

Kuna uwezekano mkubwa tu kuwa huyo jamaa yako bidada alivyokuwa anaongeza shule ye alikuwa anaongeza control ili ajihisi ndo mwanaume. Hapo ndo matatizo yanapoanza. Mwanamke akipata si mnasaidiana shida iko wapi?
 
Last edited by a moderator:
Wote hawajiamini na hawajakamilika na Mungu aliliona hilo akawaumba pamoja ili watengeneze huo ukamilifu. Wewe na heaven on earth ndio strong/smart women here.You two deserve to be referred to as Great Thinkers.May God bless you.
 
Kuna uwezekano mkubwa tu kuwa huyo jamaa yako bidada alivyokuwa anaongeza shule ye alikuwa anaongeza control ili ajihisi ndo mwanaume. Hapo ndo matatizo yanapoanza. Mwanamke akipata si mnasaidiana shida iko wapi?

The truth!
 
ndugu yangu Son of Gamba umepotoka kabisa ndugu yangu hivyo vigezo ulivyoweka haviendani na mada inayozungumiziwa hapa kwani nani amekwambia maumbile ndo yanafanya kuwa wewe si dhaifu, mtoa mada amefanya ufumbuzi na utafiti ndo mana ametoa post hiyo hajakurupuka to from no way akaandika hapo kuwa makini, mdadisi, na mfumbuizi utaelewa kuwa nyie wanaume ni wadhaifu kwetu hiyo ni true kwa 100% utake usitake iko hivyo. Are you together hapo?
Udhaifu upi Ladyfurahia?? Udhaifu upi? Wanaume ni wadhaifu kwenu ninyi wanawake, udhaifu upi???? Mfano mdogo tu, mimi kama mwanaume nikimuona mwanamke yeyote yule mzuri kama wewe ladyfurahia, nikikupenda, naweza kukusimamisha, nikakutongoza, nikakudanganya kidogo na ukanikubalia na nikakuchukua; sasa nani dhaifu hapo???? Au wewe unafikiri tunapowanunulia wanawake magari na kuwajengea majumba huo ni udhaifu???? Hapana Ladyfurahia, tunafanya hivyo kwa sababu ya sifa tu! Tukiwa wanyenyekevu mbele ya wanawake sio udhaifu, kuna kitu huwa tunakitaka, tukishapata kile tunataka, unyenyekevu wetu huwa unakwisha. Mwanaume huwa mpole mbele ya mwanamke kwa kipindi fulani, na katika kipindi hichi, mwanaume anaweza akafanya baadhi ya vitu, akaonekana mbele ya mwanamke kama ni dhaifu, lakini sio kweli, ni mbinu tu fulani ya kutafuta anachokitaka. Mimi nakataa kabisa dada yangu Ladyfurahia, mwanaume sio dhaifu mbele ya mwanamke, hata Mtambuzi aliyeanzisha hii mada, analijua hilo vilivyo.
 
Mungu akusaidie yaelekea hata mama yako pia ni jambazi maana umetuorodhesha wote, una matatizo ya kisaikolojia acha nimwite Lady doctor aanze kukupima vipimo vya kwanza halafu mm nije kumalizia

Hahaha...uliona ukimjumuisha na mama yangu kwenye hili utaukwepa ukweli au? hata kwenye maandiko ya biblia wanaume tumeambiwa kabisa kuwa tuishi na wanawake zetu kwa busara na hekima. sasa mpaka hapo usichoelewa ni nini? the fact will remain the same....wanawake ni majambazi (ofcourse excluding my mother to be precise)

Sema jingine sasa.
 
unamaanisha Mwita Maranya au???????????

Acha hizo Blue G wanaume wa kikurya ndio tunajua kutake care ya wanawake zetu. Kama ni mabavu yapo kote kote tu bila kujali kabila la mtu.

Nakupa changamoto kidogo tu, ni kwanini wanaume wa kikurya tunapendwa sana na wanawake wa makabila mengine kuliko wanawake wa kikurya? kwa kukusaidia tu pa kuaznia kawaulize wanawake wa kiwachaga wanatupendea nini?
 
Last edited by a moderator:
naomba proof za makaratasi sio tu unajisemea mwenyewe,nashindwa kukubali kwa kuwa wahenga walisema mwambaaa ngomaa.........malizia na wewe afu useme kama ni uwongo au ukweli.......
Acha hizo Blue G wanaume wa kikurya ndio tunajua kutake care ya wanawake zetu. Kama ni mabavu yapo kote kote tu bila kujali kabila la mtu.

Nakupa changamoto kidogo tu, ni kwanini wanaume wa kikurya tunapendwa sana na wanawake wa makabila mengine kuliko wanawake wa kikurya? kwa kukusaidia tu pa kuaznia kawaulize wanawake wa kiwachaga wanatupendea nini?
 
Hii ndo JF home of GT. nimeipenda mada inafikirisha. My wife to be is so smart and she is so ready to learn from my steps namshukuru Mungu kwa nguvu kubwa ya upendo iliyopo kwenye uhusiano wetu kwani imeniwezesha kukubali kufundishwa na huyu mrembo hasa kwa yale mambo ambayo yuko fit zaidi yangu na kutokana na utayari huo kila mmoja anafurahia akili na maarifa ya mwenzake.
 
mie namsikiza shaggy anaimba strength of woman, wimbo ukiisha ntarudi kucomment
 
Acha hizo Blue G wanaume wa kikurya ndio tunajua kutake care ya wanawake zetu. Kama ni mabavu yapo kote kote tu bila kujali kabila la mtu.

Nakupa changamoto kidogo tu, ni kwanini wanaume wa kikurya tunapendwa sana na wanawake wa makabila mengine kuliko wanawake wa kikurya? kwa kukusaidia tu pa kuaznia kawaulize wanawake wa kiwachaga wanatupendea nini?
Kuna kaukweli nimekaa na hawa jamaa (wakurya) yaani kwa mkoa wa Mara na makabila yote yaliyopo kama una kazi yoyote ya maendeleo fanya kazi na Mkurya itafanikiwa (jamaa wapo real nilichojifunza kwa kufanya kazi kwangu huko kipindi cha miaka 2 na ushee ni kwamba ubabe wanaoufanya mpaka uingie kwenye kumi na nane zake tena lazima atakupa warning na mara nyingi kama sio kabila lake utakuwa umeingia either kwa mtoto wake wa kike ambae bado anasoma au mkewe).
 
Back
Top Bottom