Wanaume ni dhaifu na hawajiamini mbele ya wanawake...!

Wanaume ni dhaifu na hawajiamini mbele ya wanawake...!

Familia ni msingi mkubwa na wa mwanzo kabisa katika jamii. Msingi huu unahitaji uongozi na utawala. Baba kama kichwa cha familia ni mtawala, na mtawala maana yake anaendesha utawala wake kwa misingi aliyojiwekea yeye mwenyewe (hapa mabavu ni muhimu).

Mama ni kiongozi ndani ya familia - hivyo huchukua maagizo toka kwa mtawala (baba) na kuyafanyia kazi. Katika hili iwapo viongozi hawa watakuwa wa kiasi, kila mmoja kumsikiliza mwenzake, siamini kama kuna atakayekuwa dhaifu kwa mwenza wake wala kutokujiamini.
 
Mtambuzi Umenena
Juzi nilikuwa Morogoro nikashukia Hotelini, chumba cha jirani kulikuwa na ugomvi mwanaume anagombana na kiburudisho chake. Anamfokea na kumtolea matusi sana. mara huyo bwana yako bado uko! nae mie nitakuonyesha kila siku ankupigia simu na matusi meengi sana
Nikamuuliza mwenzangu!! unasikia ugomvi nyumba ya jirani? akasema ndio nikamuuliza unafikiri huyo mwanaume yuko sahihi? mwenzanhu akajibu ndio!
Mie nikamwambia kwa mtizamo wangu mwanaume hayuko sahihi kabisa! kwani amelipia hotel ili aje agombanie huko? kwa nini asifanye kilichompeleka huko he! he! he! nikamwambia huyu hajiami na hajui anataka nini!! ningelikuwa mie hata sina muda na pesa za kupotezea hotelini kama huyo jamaa!! ninge...mengine baadae
 
pole best umesharudi kwenye maziko ya mama yetu
Familia ni msingi mkubwa na wa mwanzo kabisa katika jamii. Msingi huu unahitaji uongozi na utawala. Baba kama kichwa cha familia ni mtawala, na mtawala maana yake anaendesha utawala wake kwa misingi aliyojiwekea yeye mwenyewe (hapa mabavu ni muhimu).

Mama ni kiongozi ndani ya familia - hivyo huchukua maagizo toka kwa mtawala (baba) na kuyafanyia kazi. Katika hili iwapo viongozi hawa watakuwa wa kiasi, kila mmoja kumsikiliza mwenzake, siamini kama kuna atakayekuwa dhaifu kwa mwenza wake wala kutokujiamini.
 
wengine huwaogopi lakini kwangu ni tofauti nikitokeza tu wakuwa mpole utadhani umemwagiwa na maji
unajua sababu gani "i'm strong woman" hebu ona hapa unachotaka kwangu tuu.jpg
Sakapal sikuogopi!!!

kwanza watu8, what happened to the lunch!??
 
kwa hiyo ndio kusema kuwa ""When I'm right no one rembers but when I'm wrong no one forgets" @Baba V
 
Mmmmhh na wewe Bro na hao "wataalamu" wako aisee...

Sikieni hapa!

Haya mambo nyie ndio mnaoharibu. Kila kitu kipo safi kabisa na kimekuwa kinapendeza mbele ya Mungu mwenyewe. Masimulizi yanasema hata baada ya kumaliza kazi ya uumbaji yeye mwenyewe Muumbaji alikaa akatuangalia na akaona imempendeza machoni mwake.

Sasa hizi shida za kulinganisha sijui nani dhaifu au nani imara ni porojo tu za kupoteza mda na wengine wapate hela za kula ila cha maana hapa ni kuwa haya yote (ya mwanaume na mwanamke) yalimpendeza Mwenyezi.
 
Nionavyo mimi si mwanamke au mwanaume anayejiamini. Wote hawajiamini na hawajakamilika na Mungu aliliona hilo akawaumba pamoja ili watengeneze huo ukamilifu. Hivyo mwanaume bila mwanamke hawezi kujiamini na mwanamke bila mwanaume hawezi kujiamini. Wote tunategemeana na kukamilishana. Ukisema mwanaume hajiamini mbona kila siku wadada wanapigana waolewe na ukisema wanawake hawajiamini mbona wakaka kila siku kujitutumua ili ampate mdada fulani kwa gharama yoyote? Wote tuna mapungufu fulani
 
nitajie kitu gani Mwenyezi Mungu alichokitoa kwako na kumuumba mwanamke, kwani alitoa kitu ukabaki na kimoja sasa hapo huoni kuwa wewe ni dhaifu kwetu?
Mmmmhh na wewe Bro na hao "wataalamu" wako aisee...

Sikieni hapa!

Haya mambo nyie ndio mnaoharibu. Kila kitu kipo safi kabisa na kimekuwa kinapendeza mbele ya Mungu mwenyewe. Masimulizi yanasema hata baada ya kumaliza kazi ya uumbaji yeye mwenyewe Muumbaji alikaa akatuangalia na akaona imempendeza machoni mwake.

Sasa hizi shida za kulinganisha sijui nani dhaifu au nani imara ni porojo tu za kupoteza mda na wengine wapate hela za kula ila cha maana hapa ni kuwa haya yote (ya mwanaume na mwanamke) yalimpendeza Mwenyezi.
 
kwa hiyo ndo kusema kuwa tukiungamanishwa na kushikamanishwa na Mungu tu wamoja siye na tu wakamilifu?
Nionavyo mimi si mwanamke au mwanaume anayejiamini. Wote hawajiamini na hawajakamilika na Mungu aliliona hilo akawaumba pamoja ili watengeneze huo ukamilifu. Hivyo mwanaume bila mwanamke hawezi kujiamini na mwanamke bila mwanaume hawezi kujiamini. Wote tunategemeana na kukamilishana. Ukisema mwanaume hajiamini mbona kila siku wadada wanapigana waolewe na ukisema wanawake hawajiamini mbona wakaka kila siku kujitutumua ili ampate mdada fulani kwa gharama yoyote? Wote tuna mapungufu fulani
 
Last edited by a moderator:
Kwa dhana nzima ya kutokujiamini ni kweli kuwa mtu asiejiamini hutumia baadhi ya mambo uliyoainisha hapo juu
'
Lakini kwenye suala la mwanaume na mwanamke nimeshindwa kuipata point yako hasa iko wapi
'
Je,unazungumzia udhaifu wa kiafya wa mwanaume dhidi ya mwanamke?
'
Je,ni udhaifu wa baadhi ya wanaume wa kujiona hawajakamilika mpaka wawe na wanawake?
'
Kwenye suala la protection,wanawake mpaka leo wanahitaji jambo hili kutoka kwa mwanaume hata kama awe na mafanikio kiasi gani
'
Mkuu sijaielewa mada yako kabisa!

Mkuu Eiyer. katika mada hii nimezungumzia swala la kutojiamini.
Na katika maelezo yangu hapo juu pamoja na mifano kadhaa nimejaribu kueleza jinsi wanaume wasivyojiamini mbele ya wanwake na ndio maana hutumia mabavu ili kutaka kuwajengea hofu. swala si kutawala bali ni kuongoza, na kuongoza sio lazima kutumia mabavu, ukisoma falsafa za watu wengi waliokuwa wakitafuta haki kwa amani kamwe hawakutumia mabavu bali walikuwa wakiongozwa na hekima na busara, hebu angalia mfano wa Budha, Mahatma Gadhi, Osho na wengineo.

kama ukisoma vitabu vya Dini vilisema mwanaume ni kichwa cha nyumba na sio mtawala wa nyumba, je unaona tofauti?
lakini mwanaume kwa kumhofia mwanamke akatafuta namna ya kumtawala mwanamke na njia aliyochagua ilikuwa ni mabavu.

Kuhusu swala la kiafya, mbona majibu ni rahisi, kumbuka kwamba huyu mwanaume kwa kutaka kujionyesha kwa mwanamke kwamba yeye ni shujaa na hatishiki alidiriki kujiingiza katika harakati za hatari hivyo kuuchosha mwili wake, kumbuka kwamba, mwanaume hawezi kuwa na amani pale anapohisi hamudu kutekeleza mahitaji ya mwanamke, badala ya kutumia busara katika kutafuta suluhu, atajaribu kwa kila namna hata kuhatarisha maisha yake ili aweze kumtimizia mahitaji ya mwanamke na hiyo ipo hata katika harakati za kumuwania mwanamke anayeonekana kuwa mzuri, mwanaume anaweza kujiweka katika hali ngumu ili tu kumpata mwanamke amtakaye ili kuthibitisha kwamba yeye ni shujaa, lakini wakati mwingine unaweza kukuta mwanamke hahitaji yote hayo bali tu hofu ya ushindani inamfikisha mwanaume mahali ambapo anafupisha umri wake wa kuishi.

Kuhusu Protection ni kweli, mwanamke anahitaji Protection kutoka kwa mwanaume lakini si kutawaliwa kwa mabavu.

hebu soma mada yangu vizuri utaelewa point yangu
 
Mkuu nna wasiwasi hi makala kaandika shemeji wewe umemsaidia kupost tu, oungo?
 
Back
Top Bottom