Wanaume ni dhaifu na hawajiamini mbele ya wanawake...!

Wanaume ni dhaifu na hawajiamini mbele ya wanawake...!

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,442
slide-39-359x414.jpg

Kwa kawaida mtu anayeamini kwamba, ni dhaifu, hujaribu kwa kila njia kuficha udhaifu wake, na moja ya njia hizo ni kujikweza ili kujaribu kumshusha yule ambaye anadhani anamzidi. Mtu asiye na nguvu anaweza kujitahidi kupiga kelele, kupiga ‘mikwala' na vitisho, na watu wanapomwogopa, hupata nafasi ya kuwakandamiza hadi pale inapotokea bahati watu hao wakamshtukia kwamba hana nguvu anazodai anazo. Hata hivyo, ule woga kwa mtu huyo utaendelea kuwepo kwa watu wengi.

couple-fighting-450pk062810.jpg

Kwa miaka mingi mwanaume aligundua kwamba, ni dhaifu mbele ya mwanamke na katika juhudi za kufidia pengo hili alipitiliza mipaka na kujikuta anafanikiwa kumkandamiza mwanamke. Eneo ambalo mwanaume anaweza kusema ni bora kuliko mwanamke labda ni mabavu ya kimwili, ambayo kwa bahati mbaya kwenye zama hizi hayana tena maana, yamepitwa na wakati.

Ukiangalia maeneo mengine yote, mwanamke ndiye bora zaidi. Mwanamke huishi miaka mingi zaidi ya mwanaume (kati ya miaka mitano hadi kumi) na mwanamke huugua au kupata maradhi kidogo zaidi kuliko mwanaume. Wanaume wengi zaidi, kwa kiasi cha mara mbili zaidi hupata matatizo ya kiakili ukilinganisha na wanawake, huku idadi ya wanaume wanaojiuwa ikiwa kubwa zaidi kuliko ile ya wanawake.

Itinerary-Pic6.jpg

Ni kweli, mwanaume anaweza kuringia mabavu yake, lakini huo siyo ubora ambao binadamu anatakiwa kuuringia sasa hivi, kwani unahusu zaidi wanyama kuliko binadamu. Enzi za kuuwa wanyama kwa mawe, mabavu yalikuwa na maana, si leo. Mwanaume kwa karne kadhaa amejitahidi kutumia mabavu yake kumwonyesha mwanamke kwamba, yeye siyo dhaifu. Kwa bahati mbaya mwanamke naye akadhani ni dhaifu. Yeye kukosa mabavu akadhani ni udhaifu. Kwa wakati huo ilikuwa ni sahihi kwa sababu binadamu aliishi kama mnyama. Mtu aliyeheshimiwa alikuwa ni yule aliyekuwa na nguvu za kuuwa mnyama kwa jiwe, lakini bila shaka, leo mambo ni tofauti.

120208081803-african-american-couple-coffee-relationship-ovulating-story-top.jpg

Hebu ona, hadi leo mwanaume anaweza kuhatarisha maisha yake au hata kupoteza maisha akijaribu kutafuta njia za kumfanya mwanamke amwone kuwa ni wa maana. Atasema uongo, atajikweza, atajifaragua, akitafuta kukubaliwa na mwanamke. Huu ni udhaifu mkubwa na unaonyesha ni kwa kiasi gani jinsia hii isivyojiamini. Udhaifu huu na mwingine ndiyo ambao mwanaume amekuwa akitafuta kuuficha ili mwanamke asiuone, ambapo ameamua kumkandamiza kwa mabavu.

Mwanazuoni mmoja wa utambuzi alipata kusema, wale wanaume wote ambao walijitahidi kuifanya dunia hii kuwa mahali penye kupendeza, walikuwa na tabia ambazo ni wanawake zaidi wanaokuwa nazo. Walikuwa na huruma, upendo, unyenyekevu, kusamehe, kusaidia na kujali. Leo hii mwanaume ukitaka kuitwa mwanamke, onyesha huruma, onyesha upendo, onyesha usamehevu. Unaweza kuona ilivyo, kwamba, bila kuonyesha mabavu manaume anahisi kuumbuka.
Black-Couple-Arguing-pointing.jpg

Kuna wakati tulikuwa tukizungumza na ndugu yangu ambaye alikuwa anatarajia kufunga ndoa. Mmoja kati ya ndugu zangu waliokuwepo alisema, ‘inabidi huyo mchumbako tumuone, kwa upole wako anaweza kukukalia ukimwoa.' Unaona? Kinachomlinda mwanaume ni kitu kimoja tu, kuwa mbabe na mkali, basi. Hana silaha nyingine na hajawahi kuwa nayo, hivyo akiiachia hii ya mabavu, anajua atakuwa amekwisha……
 
^^
Teh teh Mtambuzi ulitarajia nini kwa mwanaume ambaye ubavu wake ulichukuliwa na kupelekwa kwa mtu ambaye hana alama usoni kama ndiye au siye,
Ngoja twende kiupande upande tu (udhaifu)
^^
 
Last edited by a moderator:
Mtambuzi, huwa wanaume mnatusema sana sisi wanawake kutokana na uwongo wetu..........kumbe nanyi kuna engo mkibananishwa kidogo tu,chaliiii.
Hebu mieeeee.
 
Last edited by a moderator:
Mtambuzi ingawa hujanialika,nimeamua kujileta mwenyewe

ni kweli kwamba wanawake tuna have certain power over men
too bad most of us we dont know it!!!!!!

If a woman recognizes her power over men, and chooses to exercise it,
she can own a man unakuta mtu ni bosi mkubwa sehem fulani lakin
kwa mwanamke wake hafurukuti,
 
Thank God,,hamuitumii ipasavyo
^^
 
Hebu ona, hadi leo mwanaume anaweza kuhatarisha maisha yake au hata kupoteza maisha akijaribu kutafuta njia za kumfanya mwanamke amwone kuwa ni wa maana. Atasema uongo, atajikweza, atajifaragua, akitafuta kukubaliwa na mwanamke. Huu ni udhaifu mkubwa na unaonyesha ni kwa kiasi gani jinsia hii isivyojiamini. Udhaifu huu na mwingine ndiyo ambao mwanaume amekuwa akitafuta kuuficha ili mwanamke asiuone, ambapo ameamua kumkandamiza kwa mabavu.
shem umesema mengi sana ya ukweli kabisa....
nimefurahi sana kusoma haya toka kwa mwanaume, maana nyie mnajijua zaidi.
hiki kisehemu nilichokichukua ndo hasa nataka kukichangia. Ukweli haya mambo yapo sana na binafsi huwa yananikera saaaanaaa na naona ni udhaifu mkubwa sana ambao wanaume wengi sana wanao. wanaume wengi hawataki kukubali kuwa wanawake wanaweza kuwa bora kuliko wao, kwa namna yoyote ile..... kifedha, kielimu, kikufikiri........ na ndo maana wadada wengi sana wenye uwezo wa juu wanaishia kubaki bila wanaume waliokuwa committed kwao, sababu wanaogopwa.
nakumbuka nimewahi sema mara nyingi tu huwa nipo karibu sana na wakaka. utaona hata mkaka ambaye ana elimu nzuri tu anaogopa mdada mwenye elimu kama yake au zaidi yake... utakuta kwenye vijiwe mtu akitaja anataka kumtokea mdada fulani wenzie wanamshangaa.... "fulani? utamuweza kweli?" yaani wanatiana uoga kabla hata hawajajaribu...... huku ni kukosa kujiamini....
wadada wenye pesa zao ndo kabisaaaa, kila siku majanga, wakaka hawana guts za kuwatokea na kuishi nao kwa commitment, labda kwa siku kadhaa na kuchuna pesa zao, wanahisi watanyanyaswa....... huku ni kutokujiamini kwa high degree.....

Wanaume wengi hawataki kukubali kuwa wanawake wanaweza kuwa bora kuliko wao, kwa namna yoyote ile..... kifedha, kielimu, kikufikiri........ na ndo maana wadada wengi sana wenye uwezo wa juu wanaishia kubaki bila wanaume waliokuwa committed kwao, sababu wanaogopwa.
nakumbuka nimewahi sema mara nyingi tu huwa nipo karibu sana na wakaka. utaona hata mkaka ambaye ana elimu nzuri tu anaogopa mdada mwenye elimu kama yake au zaidi yake... utakuta kwenye vijiwe mtu akitaja anataka kumtokea mdada fulani wenzie wanamshangaa.... "fulani? utamuweza kweli?" yaani wanatiana uoga kabla hata hawajajaribu...... huku ni kukosa kujiamini....
wadada wenye pesa zao ndo kabisaaaa, kila siku majanga, wakaka hawana guts za kuwatokea na kuishi nao kwa commitment, labda kwa siku kadhaa na kuchuna pesa zao, wanahisi watanyanyaswa....... huku ni kutokujiamini kwa high degree.....

Fixed Point, naona tunarudi kule kule kwenye hii mada:

https://www.jamiiforums.com/mahusia...-ukweli-wanaume-huwaogopa-wanawake-smart.html
 
Last edited by a moderator:
@Mi naomba nikuulize Mtambuzi....kwa nn mnatumia mabavu kama defensive mechanism?

Kwa nini mnazani au kujishuku kuwa mkiwa na tabia ya upole katika mahusiano mtatawaliwa na mwanamke?

Na je mwanamke akiwa na power over you na aka apply na mambo yakaenda vizuri kuna shida gani?

Kwa nini mkionaga girlfriends/wake zenu wanaongea na mwanaume hata km ni mambo ya kawaida au ya kiofisi mnakuwa hamjia mini, mnakuwa na wasi wasi na mnaweza hata kuzua tafrani on the scene or after?

Nimechangia kwa staili hii nikopata majibu nitaendelea
Mtambuzi, Dark City Kaizer Ruttashobolwa na wanaume woote please
 
Last edited by a moderator:
shem umesema mengi sana ya ukweli kabisa....
nimefurahi sana kusoma haya toka kwa mwanaume, maana nyie mnajijua zaidi.
hiki kisehemu nilichokichukua ndo hasa nataka kukichangia. Ukweli haya mambo yapo sana na binafsi huwa yananikera saaaanaaa na naona ni udhaifu mkubwa sana ambao wanaume wengi sana wanao. wanaume wengi hawataki kukubali kuwa wanawake wanaweza kuwa bora kuliko wao, kwa namna yoyote ile..... kifedha, kielimu, kikufikiri........ na ndo maana wadada wengi sana wenye uwezo wa juu wanaishia kubaki bila wanaume waliokuwa committed kwao, sababu wanaogopwa.
nakumbuka nimewahi sema mara nyingi tu huwa nipo karibu sana na wakaka. utaona hata mkaka ambaye ana elimu nzuri tu anaogopa mdada mwenye elimu kama yake au zaidi yake... utakuta kwenye vijiwe mtu akitaja anataka kumtokea mdada fulani wenzie wanamshangaa.... "fulani? utamuweza kweli?" yaani wanatiana uoga kabla hata hawajajaribu...... huku ni kukosa kujiamini....
wadada wenye pesa zao ndo kabisaaaa, kila siku majanga, wakaka hawana guts za kuwatokea na kuishi nao kwa commitment, labda kwa siku kadhaa na kuchuna pesa zao, wanahisi watanyanyaswa....... huku ni kutokujiamini kwa high degree.....

kama mentality za wanawake wengi wa kibongo ni kwamba A MAN MUST PROVIDE FOR HER NO MATTER WHAT,sasa mwanaume ataweza vipi kutoka na demu aliemzidizidi kipato[achilia mbali elimu]??lazima atafute aliemzidi ili niweze kuprovide kwa kiwango chake/changu.....mimi binafsi sijali kipato wala elimu nishadate walionizidi kipato na nawahandle kama kawaida tu,maybe because im too confident to the extent u can think im arrogant
 
He ni stronger than she...ukiona unamkamata ujue kuna ishu ananufaika nayo...kwa bible wao ni ubavu product tena wa kushoto,wasaidizi...lakin ili dume lifaidi ndo utaona linalemaa ukakamavu wake eg. Samson na delilah
 
Back
Top Bottom