ni swala la kujua tu malengo yako. pamoja na kila kitu unachotaka kujifanyia/kufanyia watu, unatakiwa kujua mwisho wa siku wewe unataka nini.
huwa nawatimuaga ndugu zangu ambao wao na mimi wote wafanyakazi, wao inapofika muda wa kulipa ada ya shule ya mwanaye anakuja kwako kukuambia anaomba msaada hana hela ya ada, hali kadhalika inapofika kulipa kodi ya nyumba.
Huwa najiuliza hiki kitu hakijatokea ghafla, mtu unajua kabisa mwezi fulani nalipa ada/kodi kiasi fulani. Mshahara wako kwa miezi 2 hautoshi kulipa (usiniambie ulikuwa unategemea dili). kwa nini usianze ku-accumulate kidogo kidogo mpaka itakapokamilika? hilo deal likitokea utafanyia kitu kingine.....
Mfanyakazi nalikumbuka sana na coverage yake ya ile kesi mpiga picha/mwandishi wa habari (jina limenitoka kidogo) ndo iliyompaisha Masumbuko Lamwai kutoka kwenye obscurity na kuwa household name. Nilikuwa napenda sana kusoma 'Amini Usiamini'.
Je, kwa sasa umesikia huo mshahara ni mara 58 zaidi ya ule wa kima cha chini toka kwa nani/wapi?
Hiyo 'haujamtoa kwenye umaskini' inahitaji qualification nadhani. Maana kuwa na gari tu haimaanishi kwamba mtu ndo ushatoka kwenye umaskini na kutokuwa na gari haimaanishi mtu ni maskini.
Mara ya kwanza niliposikia Mzee Gurumo wa Msondo Ngoma
anadai ameimba zaidi ya miaka 50 na maisha yake bado
ya 'kimaskini mno' niliona kuna kitu hakiko sawa..
sikuwa na ushahidi tu lakini nilikuwa na uhakika kwa vyovyote vile
'atakuwa alichezea maisha ujanani'
Sasa jana walioona akifanyiwa interview na Salama kipindi cha MKASI
watakubaliana na mimi huyu Mzee na wengine wengi tunaosikia
wakihojiwa na vyombo vya habari ..wakilaumu serikali kwa kutowajali.
wengi wao walipata 'golden opportunities' za kuwa na maisha bora
lakini 'walichezea pesa' na 'opportunities hizo' so many times...
mfano Mzee Gurumo jana alisema alilipwa 'elfu ishirini'
mwaka 1978 ili kuhamia bendi ya Sikinde...kumbuka
kuwa Mshahara wa Rias mwinyi mwaka 1992 ulikuwa 'elfu ishirini na saba tu'
sasa pata picha huyu mzee alikuwa na pesa kiasi gani?
na mshahara wake ulikuwa 'shilingi elfu tatu' mwaka hu0 1978..
wakati kima cha chini mpaka mwaka 1987 kilikuwa hakijafika 'shilingi elfu saba'
Kuna Mzee mwingine alitunga kitabu riwaya 'Simu ya Kifo' alilipwa
'elfu kumi na mbili ' miaka hiyo nyumba Kariakoo zinauzwa shilingi 'mia nne'
na alikufa bila nyumba wala kibanda..
Orodha ni ndefu...na wapo wengine Baba zetu,Wajomba,babu na kadhalika
ukiwaona uzeeni wanavyolalamika na kuomba wasaidiwe....utasema hawakupata chochote ujanani
kumbe anasa,starehe na kuhonga wanawake ndo sababu....
ukweli ni kwamba watu 'huchezea maisha mno' halafu uzeeni hutafuta wa kumpa lawama
mara watoto,mara serikali na kadhalika....
huyu Mzee Gurumo alikuwa sio mtu wa kupewa gari na Diamond...
angekuwa na magari na majumba tele ya kuwarithisha watoto na wajukuu...
Samahani Kibibi Jongo, Eiyer . Kuna watu hawalali katika maisha yao wao kucha kutwa wanahangaika kusaka maisha tena wakiwa na mipango mizuri ya kipesa lakini mwisho wa siku hawafanikiwi wanabakia hohehahe hili linasababishwa na nini? Pia huwa ?
Pole sana kila mtu ana woga na 'future'
me included but kuwa na woga ni first step
as long as unaogopa itakusaidia...sanaa
pesa ndo hizi hizi tu
unapandisha nyumba kozi tatu zingine una spend
ukirudi unaongeza kozi nne na una spend kidogo
Jamani mnapoyasema yeye msimsahau na Mungu wote tungekuwa kama daimond nan angekuwa ngurumo?kumbukeni kwamba jitihada zako pekee hazishindi kudra za MUNGU.simtetei ngurumo wala simlaumu kila kitu kinasababu yake............
The Boss hiyo ndiyo reality...mwanzoni nilikuwa najiuliza sana watu wanawezaje kujenga? Thinking of my father, aliwezaje kujenga? Nikasema no starehe, no nothing unnecessary...kweli mambo yakabadilika...nikapata plot, nikanunua building materials...na sasa kibanda kinaiunuka...umri ukienda my kids will realize kwamba I did something for them! Mambo yanawezekana sema tu vijana wanataka Verossa na kuning'inia SamakiSamaki!
Hakuna kitu kama hicho
Huwezi kufanya kazi kwa bidii halafu ukawa na mipango mizuri ya kifedha halafu usifanikiwe
Unaweza kufanya kazi sana,kufanya kazi sana kuna maana ya kuingiza sana pia
Lakini ukawa unatumia sana pia
Hapa kosa ni lako
Kanuni ya kufanikiwa inasema kuwa haijalishi unaingiza kiasi gani bali unatunza kiasi gani!
Tatizo la watu wengi ni kuweka vipaumbele....
ndiyo maana huwa na kumbuka sana kauli ya Mwalimu Nyerere..."Kupanga ni kuchagua"!!!
Babu DC!!
yaani The Boss umetugusa wengi, babangu anaelekea kustaafu lakini hata nyumba hana. halafu sioni kama hili linamuumiza yaani sie tumekuwa wa kuishi kotta wakati mzee ana uwezo wa kujenga lakini anaendekeza starehe hadi uzeeni. sas sijui atamlaumu nani.
Unavyopenda mambo ya hivyo, hata sijui unajisikiaje... Lol!
Ila ni kweli, mtu ukipata mke wa hovyo imekula kwako!
Kwenye hili sina ubishi mkubwa mwenzangu....
Mwenzenu hadi sasa, karibia vitu vingi sifanyi bila ruhusa ya bibi....ila wakati mwingine anakaba sana hadi natamani kukimbia nyumba....
Mwanamke wa hovyo ni zaidi ya kiroba cha misumali.....
Ndiyo maana nawakubali na kuwaheshimu akina na mama wenye busara zao, wakiongozwa na Bibi DC, mama yangu mazazi na wengine kibao....!!
Babu DC!!
rafiki, dont underestimate the power of a woman....never......na ukipata mume wa hovyo je?
Mimi nafikiri ukipata mke wa hovyo na ukakubali kufuata uovyo wake nawe ni wa hovyo au akili zako ni za kushikiwa. Ofcourse kama couple mnahitaji kuwa na malengo mliyokubaliana na strategy mlizokubaliana.
kweli usipojipanga ujanani uzee wako lazma uwe wa tabu sana, ahsante kwa kutukumbusha hili The Boss.
Kwenye hili sina ubishi mkubwa mwenzangu....
Mwenzenu hadi sasa, karibia vitu vingi sifanyi bila ruhusa ya bibi....ila wakati mwingine anakaba sana hadi natamani kukimbia nyumba....
Mwanamke wa hovyo ni zaidi ya kiroba cha misumali.....
Ndiyo maana nawakubali na kuwaheshimu akina na mama wenye busara zao, wakiongozwa na Bibi DC, mama yangu mazazi na wengine kibao....!!
Babu DC!!
kuna rafiki huwa anamlalamikia baba yake kuwa hakuwajengea misingi mizuri, baba yake nae huwa anamwambia tatizo sio mimi mwanangu tatizo babu yako!! kweli kila mtu awajibike na asimame kutokea pale alipo na kusonga mbelena si kufikiria amefikaje pale.......kutoa lawama kwa serikali na kumtolea lawama mzazi wako yote sawa!
......be responsible for your own life!
Halafu utasikia wengine oohh, "baba ndio kichwa cha familia" ...jukumu lake hilo, akiweza mke anataka compliments, "behind every successful men....!"
C.r.a.p!
rafiki, dont underestimate the power of a woman....never......
hawa ni wajanja tu wakiwa nje yetu..... wakiwa ndani ya 18 hawafurukuti, hata uwe smart namna gani