Wanaume: Mnajisikia vipi mnavyoombwa pesa?

Wanaume: Mnajisikia vipi mnavyoombwa pesa?

Kiasili mwanamume ndiye mwenye jukumu la kumtunza mwanamke kwa kuwa muumba amempa mwanaume huyo uongozi na ndio maana ni jambo la ajabu kwenye jami kuona familia inaongozwa na mwanamke na hali ya kuwa mwanaume yupo na ni mzima wa afya......na kwa kila mwanaume rijali na mwenye afya ya akili kumhudumia mwanamke na kumtimizia mahitaji yake ni jambo lenye kujivunia kwake....na hata kwenye jamii mwanaume anayeimudu vyema familia yake anaheshimika sana....na kuonekana ni wa maana....

Kitendo cha wewe kuona haya kumwambia shida zako mpenzi wako ambaye ndiye msiri hali ya kuwa wewe huna kipato chochote kinaweza kikazusha maswali na hali ua wasi wasi kwa huyo mpenzi wako......anaweza akahisi labda kuna mwingine anayekuhudumia kwa kila hali ya kuwa yeye umemfanya kama chombo cha starehe.....

Hakuna haja ya kumuonea haya mpenzi wako kwani mambo madogo tunayoyadharau mwanzoni ndiyo yanayogeuka kuwa makubwa na kupelekea kuvunjika kwa mahusiano.....hebu chukulia kama mwanandoa anashindwa kumuomba mwenzie unyumba unategemea nini kwa mwenzio..!!

Nakushauri ondoa hofu na uwe huru kwa mpenzi wako kwani hali hiyo inamfanya mwenzio ajiamini na kujiona ni mwanamume kamili na hata kupelekea utendaji mzuri hata kwenye uwanja wa sita kwa sita......
Nimekupenda bila hela mpwa. Ni raha sana kuhudumiwa na mtu wako wallah
 
Kama ni wapenzi waaminifu na muombaji anazitumia kwa matumizi muhimu sio anasa haina shida. Zingatia umuhimu wa msaada unaouona sasa uukumbuke ktk ufalme wako wa mafanikio yako usimtose.
 
Mimi ni msichana nina mpenzi wangu ambaye nampenda ila nikiwa na shida huwa najishauri sana kumuomba hela,sipendi hiyo hali lakini nitafanyaje,sina kazi na bado nasoma,japo nikimuomba ananipa lakini sijui huwa anajisikiaje.

Huwa natumia njia ya simu kumuomba kwasababu nikiwa nae nashindwa kabisa kumwambia yani sielewi namuogopa ama nini.

Please nisaidieni wanaume huwa mnachukuliaje wapenzi wenu wanaowaomba hela ila mimi mpaka nikiwa na shida kubwa, please help.
We!!! Unanifaa kabsa
 
mimi huwa najisikia sana vibaya kuomba ila sipewi wala nini...na mimi sitoi papuchi wala nini ...tunaachanaga hivo...
siku nikipata wa kunipa hela nitamkubalia tutulie tupange maisha mimi naamini kuomba hela sio uhuni
no money no honey!
We ndo unanifaa kabsa n pm
 
Inauma hasa kama haikuwa kwenye bajeti.. Ika wale wanaotegesha na kusubiriwa waombe wala haiwaumi
 
Ain't nothing going on but the rent, no romance without finances...hayo Maneno ya Gwen Guthrie, katika wimbo wake wa Ain't nothing going on but the rent
 
@Lady_Jay umeuliza swali la maana sana. Mimi najisikia kawaida tu maana ni mtu tunapendana. Lakini sasa tatizo la wanawake wengi hutumia hiyo nafasi kama kuwakomoa wapenzi wao na kusababisha baadhi yetu kuwaona wanawake kama hawafai. Kama kweli ni mapenzi ya dhati toka moyoni mpenzi ataomba pesa kwa mpangilio mzuri ambao hauwezi kuleta maswali mengi. Apart from that, ladies wengine wanafanya ni kitegauchumi kwao ambapo baadae wanakuja kuwakimbia wapenzi wao na kudandia kwingineko jambo ambalo linaumiza sana.
 
For sure nisikufiche mnapotuomba pesa huwa mnatufanya tuwadharau si mnataka 50 kwa 50 yaani haki sawa mtupe na sisi pesa.
 
kuna manz alinikomesha yeye mizinga yake "naumwa" "sijala" huwez chomoa,coz ni dent wa chuo na mimi pia bado nilikuwa bado napga kitabu nikaamua nimtumie kias flan cha fedha kwa mwez kwa ajili ya chakula tuu ili hata nikiwa sina asilale na njaa,matokeo yake hela akaenda kusuka akafanya shoppin ikaisha ndan ya siku nne,akaendelea na mizinga yake ya sababu za muhimu lakin za uongo,utasikia "naumwa" leo anakuomba hela ya party ya birthday ya rafiki ake kesho anaomba hela ya kula.nikaconclude kuwa huyu hajui budget so hafai,zikaongezeka na sababu nyingine kadhaa nikaamua kujitoa mazima.nilishindwa ukizingatia me mwenyew kipind hcho nilikuwa nategemea boom na wazaz,ahaha semester inaisha mweupeee.
 
Mimi ni msichana nina mpenzi wangu ambaye nampenda ila nikiwa na shida huwa najishauri sana kumuomba hela,sipendi hiyo hali lakini nitafanyaje,sina kazi na bado nasoma,japo nikimuomba ananipa lakini sijui huwa anajisikiaje.

Huwa natumia njia ya simu kumuomba kwasababu nikiwa nae nashindwa kabisa kumwambia yani sielewi namuogopa ama nini.

Please nisaidieni wanaume huwa mnachukuliaje wapenzi wenu wanaowaomba hela ila mimi mpaka nikiwa na shida kubwa, please help.
Wewe huna kazi sawa jee yeye anayo kazi?
Kama hana kazi huhisi kama umemuongezea jukumu la stress manake hata kama hana mwanaume kusema hana hela kwa anaempenda huwa ngumu.
Usisahau pia kama anakupa hela huyo ni mteja kwako sio kama mpenzi wako kwasababu analipia huduma anayoipata kutoka kwako.
Lakini kama unamuomba once every 3 month hapo hapana tabu ni kawaida tu.
 
Back
Top Bottom