Wanaume: Mnajisikia vipi mnavyoombwa pesa?

Wanaume: Mnajisikia vipi mnavyoombwa pesa?

Kiasili mwanamume ndiye mwenye jukumu la kumtunza mwanamke kwa kuwa muumba amempa mwanaume huyo uongozi na ndio maana ni jambo la ajabu kwenye jami kuona familia inaongozwa na mwanamke na hali ya kuwa mwanaume yupo na ni mzima wa afya......na kwa kila mwanaume rijali na mwenye afya ya akili kumhudumia mwanamke na kumtimizia mahitaji yake ni jambo lenye kujivunia kwake....na hata kwenye jamii mwanaume anayeimudu vyema familia yake anaheshimika sana....na kuonekana ni wa maana....

Kitendo cha wewe kuona haya kumwambia shida zako mpenzi wako ambaye ndiye msiri hali ya kuwa wewe huna kipato chochote kinaweza kikazusha maswali na hali ua wasi wasi kwa huyo mpenzi wako......anaweza akahisi labda kuna mwingine anayekuhudumia kwa kila hali ya kuwa yeye umemfanya kama chombo cha starehe.....

Hakuna haja ya kumuonea haya mpenzi wako kwani mambo madogo tunayoyadharau mwanzoni ndiyo yanayogeuka kuwa makubwa na kupelekea kuvunjika kwa mahusiano.....hebu chukulia kama mwanandoa anashindwa kumuomba mwenzie unyumba unategemea nini kwa mwenzio..!!

Nakushauri ondoa hofu na uwe huru kwa mpenzi wako kwani hali hiyo inamfanya mwenzio ajiamini na kujiona ni mwanamume kamili na hata kupelekea utendaji mzuri hata kwenye uwanja wa sita kwa sita......

Wengi wao ni wabinafsi na wachoyo ...ukimwomba pesa anakuona hufai ila **** wanataka.....
 
Yaani nyie wanafunzi tena wa CBE mnamizinga sana unataka hela kubwa Mimi siku ya kwanza anataka mtoto tukale Selena mshahara wangu laki Tisa nakulala Selena wapi na wapi na Mimi .

Hahaha
 
Kuombwa hela siyo tatizo, wala kumsaidia mpenzi au rafiki yako kwa kumpa fedha siyo tatizo. Kwangu mimi, nadhani hata kwa wanaume wengi, tatizo huwa ni pale ninapoombwa hela kama malipo ya kitu fulani. Hapo ndo wanawake wengi hukosea, kwa kuomba hela kama malipo ya aidha kuwa rafiki tu au kufanya mapenzi. Ikiwa hivyo basi inakuwa siyo urafiki tena ni biashara, tit-for-tat. Kumsaidia kifedha rafiki au mpenzi ni kitu cha kawaida, hasa anapokuwa na hitaji fulani, au hata asipokuwa na hitaji basi unampa tu just for fun. Lakini mdada anayetegemea kuomba hela kila baada ya 'kakitu' basi huyo siyo rafiki wa kweli.

Kwa point yako hii ndo imeweza kutofautisha Kati ya X na kuzidisha . ....
 
shda yenu ni kukremisha ukiwa na mtu mpaka umuombe hela ni ya nini hiyo hela unayoshindwa omba wazazi wako ? au kisa jamaa unampa papuch kwan huwez mpa kwa kujitolea?

Quid pro quo
Nothing goes for nothing....
 
Hawa ndugu zetu banah ukiishiwa pesa na yeye hutamsikia tena....ila ukiwa nazo sasa utaitwa majina yote my baby, mpenzi wangu,my honey, my hubby, my sweet, my chocolate, my candy, mume wangu, my lovepie, my beloved, my man, my toilet paper nk....jitahidi sana kusoma nyakati utagundua...
 
mm mpnz wangu hajawahi kuniomba pesa hata siku moja...mm kama mwanaume najisikia vbaya mana sijui nani huwa anampa pesa akiwa na shida japo wote tunafanya Kazi

Mpaka akuombe si ujiongeze ala! Halafu eti najickia vibaya..mmmh you are weird
 
Mwenyewe nilikua kama wewe,nikaja kugundua michepuko yake inachuma tu hata waombe sh ngapi wanapewa,na simu wananunuliwa,so i had to change my mind mdogo mdogo nikaomba hadi kiwanja.
Ila kama hupendi endelea hvohvo,ila usipanic ukiskia kuna wenzako wanachuma.
[emoji1435][emoji1435][emoji1435][emoji1435][emoji1435][emoji1435]
 
me mwenyew napenda kumpa pesa manzi yangu hyo inanifanya nijione kidume ninayewajibika na naitumia kumkoleza manz yangu aamini namjali. lakini nampa kutokana na kipato changu na yeye anatambua hlo na anajua na mimi nna shida zangu pia nnazotaka kuzitatua ananisupport hadi raha yani sio mbinafsi,sio mtu una mshahara 300,000 halaf unampiga miznga ya lakilaki,kama mm saiv sina ajira na manz yangu anajua so huwa nampa hela nikipata na hawez niomba hela inayozid 15,000 anajua dili za kuungaunga nnazopotaga znaweza kuniingizia maxmum sh ngap, nikiwa sina namwambia asubiri na huwa anikumbush mara kwa mara(mana inaboa, hlo nilimwambia na ametii) mpaka napata nampa,na pia huwa ananiambia shida ya hyo hela so namm najua kuwa ni ya muhimu sana niitafute kwa nguvu zote haraka au ya matumiz ya kawaida naweza kumpa muda wowote,lakini mbali na mm kumpa na yeye pia kuna siku akiwa na hela anajua me niko vbaya ananipa hata ya vocha.huyu manzi me naoa.Manzi kama huyo nimpate nijidai?😉😉 nawish ningempata wa hvyo lakin sijui kama atatokea.
 
Kumuomba pesa si tatizo tatizo kuomba bila utaratibu.........tafiti kwanza uwezo wake wa kipato kisha uwe na uhakika unachomuomba kipo ndani ya uwezo wake au unampa mtihani wa kukutafutia pesa ambayo hata yeye kuipata ni mtihani.
 
Mimi ni msichana nina mpenzi wangu ambaye nampenda ila nikiwa na shida huwa najishauri sana kumuomba hela,sipendi hiyo hali lakini nitafanyaje,sina kazi na bado nasoma,japo nikimuomba ananipa lakini sijui huwa anajisikiaje.

Huwa natumia njia ya simu kumuomba kwasababu nikiwa nae nashindwa kabisa kumwambia yani sielewi namuogopa ama nini.

Please nisaidieni wanaume huwa mnachukuliaje wapenzi wenu wanaowaomba hela ila mimi mpaka nikiwa na shida kubwa, please help.

Mi nasikia rahaa kweli [emoji18][emoji18]
 
mm mpnz wangu hajawahi kuniomba pesa hata siku moja...mm kama mwanaume najisikia vbaya mana sijui nani huwa anampa pesa akiwa na shida japo wote tunafanya Kazi
Anasubiri umpe bila kuomba,..me mwenyewe kuomba hela ni mtihani I wish atoe mwnyw willingly, japo nkibanwa shida ntaomba
 
hata mimi sijui nna shida gani.yaan kuumbwa pesa na msichana ndo imekuwa lisence ya kum dump....nmesha broke in more than 4 relations kwa kosa kama lako la kuombwa pesa.....kiukweli TUNAJISIKIA VIBAYA SANA....ukizingatia anakuomba pesa soon after or before game......nahisi kama nauziwa chezo wakati ni HAKI YANGU
Haki yako kwani umeoa?
 
Mimi ni msichana nina mpenzi wangu ambaye nampenda ila nikiwa na shida huwa najishauri sana kumuomba hela,sipendi hiyo hali lakini nitafanyaje,sina kazi na bado nasoma,japo nikimuomba ananipa lakini sijui huwa anajisikiaje.

Huwa natumia njia ya simu kumuomba kwasababu nikiwa nae nashindwa kabisa kumwambia yani sielewi namuogopa ama nini.

Please nisaidieni wanaume huwa mnachukuliaje wapenzi wenu wanaowaomba hela ila mimi mpaka nikiwa na shida kubwa, please help.


Ukiniomba pesa ujue hiyo kei nimeinunua, unanishikia tu ila nikiitaka muda wowote nagonga!!
Au kwa lugha nyingine, kila mwanamke ni muuza kei, tofauti ni ktk kuwauzia wateja wao!!
 
Kwa wanaume wengi wanaojielewa, issue sio kuombwa hela.. Issue ni inaombwa kwa style gani, nyakati gani, sababu gani.. Pia utegemezi uliopita mipaka nao unazingua.. Na vile vile mahusiano ni ya namna gani kwa wahusika..


True man!!!Utakuta msichana haangalii hali ya mwenza wala umuhim wa hitaji lake,utasikia elf 50 ya kusuka siku mbili kafumua anataka tena kusuka ili hali maisha ya mwenza anayafaham,hii mbaya omba pesa kwa kuangalia hali na shida uliyonayo.
 
Kiukweli Mimi huwa sisubiri kuombwa hela kwa sababu ni jukumu langu kumpa mpenzi wangu so ambacho nakifanya kila jumapili huwa natoa mkwanja wa kujikimu wiki nzima....hivo tu yani!!
 
Kuomba siyo shida .....lakin unatambua thamani ya mtu unaomuomba?...mwingine anaomba pasipo rejesha mrejesho wa mara ya kwanza amaeitumiaje,,,,,hana kitu kinachoaitwa ahsanteeee,,,,,na akitoa ahsante yenye kejeli,,,,,,Mimi kwa upande wangu mwanamke asiye na matumizi sahihi na mrejesho wa pesa husika sijikiii faraja na sipendi kumpa pesa labda nimnunulie kitu ama vitu.....
 
Back
Top Bottom