Wanaume kupewa kipaumbele Kliniki za watoto ni mtego

DALALI MKUU

JF-Expert Member
May 7, 2022
1,487
2,739
Bila kupoteza Muda nijielekeze moja kwa Moja kwenye Mada.

Wanawake wamekuwa wakipambania sana usawa 50/50 na serikali imekuwa ikitumia mbinu Nyingi sana ili kufanikisha jambo hilo ambalo ni kinyume kabisa na tamaduni zetu, hata kwenye vitabu vyetu vya dini ambavyo vinataka mwanamke awe msaidizi wa mwanaume, Tena ikimtambua Kiumbe dhaifu.

Sasa siku za karibuni serikali imeweka utaratibu kwenye Clinic zetu baba akimpeleka motto apewe kipaumbele ahudumiwe kwanza asikae kwenye foleni kama wengine lengo ni kuhamasisha wanume nao waende cliniki au wapeleke watoto clinic

Wakuu huu ni mtego itafika wakati akina mama hawatapeleka tena watoto clinic na yatakuwa majukumu rasmi ya baba, tukikubali hili wanaume tumeisha Aisee, tutakuwa tumejiingiza wenyewe kwenye majukumu haya ambayo tangu kuumbwa kwa ulimwengu yalikuwa ni majukumu ya Akina mama.

Jambo la Pili Hivi karibuni NIliona taarifa moja kutoka huko mbeya ikieleza kuwa majengo ya akina mama ya kujifungulia kuwe na sehemu ambayo akina baba pia watakuwa wakishuhudia Live kabisa vile mke wake anajifungua ili nawe upate ule uchungu na maumivu.


Huu nao ni mtego Tusiposhtuka mapema Maana jukumu la kuzaa ni mwanamke kwa sisi Wakristo biblia katika kitabu cha Mwanzo 3:16 inasema hivi

Kisha akamwambia mwanamke, “Nitakuzidishia uchungu wa kuzaa, kwa uchungu utazaa watoto. Hata hivyo utakuwa na hamu na mumeo, naye atakutawala.”

Hapa napo wanataka kutushirikisha kwenye uchungu ambao sisi wanaume hatuhusiki.

Wewe kama ni mwanaume fanya kazi kwa Bidii usichague kazi ya kufanya hakikisha watoto wanaishi katika mazingira mazuri, wanakula mlo kamili, wanapata elimu kuwatimizia mahitaji yao yote hayo mengine tusiukubali huo mtego.

Wasalaam
 
Kazi nyingi za nyumbani zinafanywa na wanawake, inaweza kuwa ni mama au dada wa kazi. Hii ni kutokana na uchumi wetu kuwa chini na unaruhusu cheap Labour.

Kadiri maendeleo yanavyokuja ajira kwa dada wa kazi zitapungua, wengi watatapata ajira viwandani. Wanaume itawapasa kufanya kazi za nyumbani.
 
Umeshindwa kujenga hoja. Pia umeshindwa kuyatafsiri Maandiko

Mimi binafsi mke wangu alipokuwa mjamzito siku yake ya kwanza kwenda Kliniki hadi alipojifungua na hadi watoto walipomaliza routine zao za kliniki hakuna siku nilihowahi kuacha kwenda naye ama kwenda na watoto clinic. Nilikuwa naomba ruhusa ofisini na walinielewa

Unajua nini mkuu, ni kwamba mwanamke anapokuwa mjamzito pale anakuwa na akili tofauti na ile akili yake ya kawaida na hilo utagundua hata kwenye reasoning zake. Hivyo ujue mtoto akiwa tumbonj anawasiliana na ulimwengu wa nje kupitia wazazi na endapo mjamzito anakuwa kwenye stress za ujauzito bila kupata relief ya baba mtoto ndo unakuta anadevelop tabia ambazo unaweza kuhisi anafanya kusudi.

Jambo lingine ni kwamba kumsindikiza mama mjamzito kliniki siyo kushare uchungu wake wa kujifungua.

Jaribu kuwa na mtazamo chanya kwenye hili. Wanaume tunaongoza na tunapaswa kuonesha maongozi ndani yetu.

Muulize Depal atakueleza haya haya niliyokuambia
 
Kuna siku nilikuwa hospital, mara ghafla akaja kaka mmoja kaongozana na bi dada!

Kaka kabeba mkoba plus mazagazaga! Wakaingia clinic na kutoka!

Lakini baada ya kutoka Huku nyuma wadada na wamama wakaanza kucheka pamoja na kumjadili .
 
Kuna siku nilikuwa hospital, mara ghafla akaja kaka mmoja kaongozana na bi dada!
Kaka kabeba mkoba plus mazagazaga! Wakaingia clinic na kutoka!
Lakini baada ya kutoka Huku nyuma wadada na wamama wakaanza kucheka pamoja na kumjadili .
Haha hii ni hatari sana Mkuu. Wanaume tunapoteza hadhi yetu ya utawala
 
Umeshindwa kujenga hoja. Pia umeshindwa kuyatafsiri Maandiko

Mimi binafsi mke wangu alipokuwa mjamzito siku yake ya kwanza kwenda Kliniki hadi alipojifungua na hadi watoto walipomaliza routine zao za kliniki hakuna siku nilihowahi kuacha kwenda naye ama kwenda na watoto clinic. Nilikuwa
Hayo pia na mawazo yako Mkuu. Yaani ukae leba unwangalie mke wako anajifungua hutasikia maumivu Yale? Uone kabisa anachanwa ...Kwa kisu
 
Kazi nyingi za nyumbani zinafanywa na wanawake, inaweza kuwa ni mama au dada wa kazi. Hii ni kutokana na uchumi wetu kuwa chini na unaruhusu cheap Labour.

Kadiri maendeleo yanavyokuja ajira kwa dada wa kazi zitapungua, wengi watatapata ajira viwandani. Wanaume itawapasa kufanya kazi za nyumbani.
Wanaume wawapi? Labda Kinondoni B kama watakubali
 
Kuenda tutaenda nao (kama hatuna kazi za kufanya) ila sio lazima. Sisi tuna mambo mengi ya kuvuja jasho ya kufanya!

Kuhusu huo mtego ni kweli kuna mtego maana kwa baadhi ya wanawake wasiojitambua wanaweza wakayachukulia kuwa hayo ya kumpeleka mtoto au kwenda naye Clinic ni majukumu ya lazima kwa mwanaume!

Sasa siku itokee usiende hapo ndo shida huanza mara minuno, makasiriko kibao.
 
Umeshindwa kujenga hoja. Pia umeshindwa kuyatafsiri Maandiko
Mkuu hapa umepuyanga,

Kwanza unapaswa utambue kua Mungu aliyemtengeneza mwanamke anamfahamu vizuri kuliko hawa wanaharakati wetu uchwara na maprofesa wa wetu wa michongo tulionao hapa duniani

Mungu anajua kiumbe kilichopo tumboni knaishije raha mustarehe tokea day one mpaka kinazaliwa na kukua hivyo mstari wa majukumu baina ya mwanamke na mwanaume uheshimiwe kama ilivyokua awali tuachane na huu usasa una malengo tofauti

Kuna wakati nilijiuliza hivi paka,sungura punda, mbuzi n.k ni nani anawasimamia process zao za uzazi hadi kujifungua salama ilihali wao hawaendi kupigwa utrasound kujua mtoto alivyokaa tumboni, hawapewi vidonge vya kuongeza damu kwa kua wanapoteza damu nyingi wakati wa kujifungua, watoto wao hawafunikwi na kanga ama kitu ch kuwatia joto n.k

Wakati unaendelea kupata jibu la yote hayo unapaswa kutambua kua Mungu katuumba katika mfumo ambao ni natural complete ndio maana toka enzi na enzi wazee wetu walijifungua salama majumbani mwao bila shida yoyote na maisha yaliendelea

Nakubaliana na mtoa mada nyakati hizi sekta ya afya imegeuzwa kua mtego na mabeberu watapenyeza agenda zao nyingi sana kupitia sekta hii, mfano mzuri ni hii agenda ya chanjo ya korona ambayo imezua mjadala mkubwa duniani

Zipo pia tetesi za kupunguza idadi ya watu duniani kwa kupenyeza agenda za uzazi wa mpango, abortion n.k
 
Hayo pia na mawazo yako Mkuu. Yaani ukae leba unwangalie mke wako anajifungua hutasikia maumivu Yale? Uone kabisa anachanwa ...Kwa kisu
Naam ndo maana nasisitiza upo nyuma sana kwenye eneo la kutafsiri.

Sikusema kuwa nilikaa leba kumshuhudia mke wangu akijifungua. Bali nilikuwa naenda naye hospital hata siku ya kujifungua kwake lakini hakuna mahala nimesema twende leba nao ndo maana nikaweka phrase pale juu kuwa kuwasindikiza siyo kushiriki uchungu wao.

Show love to them. Hata kama ni mchepuko nenda naye clinic🤣
 
Back
Top Bottom