Wanaume jiandaeni kupokea maisha baada ya kustaafu

Wanaume jiandaeni kupokea maisha baada ya kustaafu

Unaweza ukawa na muda na watoto halafu wakakutupa uzeeni. Kuna kitu kinaitwa utu, watoto wakikosa utu usitegemee watakutunza ukiwa mzee hata kama uliwapa muda wako na maisha mazuri.

True mkuu, ila ukizaa watatu na ukakaa nao vizuri. Siamini utakosa hata mmoja wa kukumbuka japo huwa yanatokea pia

Cha msingi ni kumuomba Mungu tu huku ukijiandalia maisha yako bila kutegemea watu
 
True mkuu, ila ukizaa watatu na ukakaa nao vizuri. Siamini utakosa hata mmoja wa kukumbuka japo huwa yanatokea pia

Cha msingi ni kumuomba Mungu tu huku ukijiandalia maisha yako bila kutegemea watu
Ni kweli mkuu, kwenye hii dunia usitegemee kuwa nikimsaidia mtu au nikitimiza majukumu yangu nitapata fadhila, maisha hayako hivyo. Kinachotakiwa, kipaumbele namba moja iwe ni wewe, wengine wanafuatia. Hata ukifa leo utazikwa nanutasahaulika na hata wale ambao walikuwa karibu nao. Hakuna mbadala wa maisha yako.
 
Uweke akiba au usiweke mwisho wa siku utakufa tu!
 
Wanaume wengi hasa wa mijini ni wajinga linapokuja suala la familia na mahusiano. Wanakubali kuishi ndoa nyonyaji wakinyonywa na wake zao ujana wao wote halafu utegemee mabadiliko uzeeni! Mke ana kipato sawa au kinakaribia sawa na cha mume lakini hachangii gharama za lazima za uendeshaji fanilia kana chakula nk.
Mke ukishamkosea mwanzoni kwa kuruhusu sera za kijinga ndani ya familia yako tegemea taabu uzeeni. Imefika hatua mume anastaafu mke anadai wagawane pensheni ya mume tena na watoto wanagawiwa. Mwinginen eti abahangaika kuwanunulia watoto viwanja na au kuwajengea nyumba , ujinga ulioje. Nyumba ukijenga jenga kwa ajili yako, watoto wasomeshe basi inatosha tena hakikisha hufanyi kazi moja tu ya kusomesha watoto shule ghali zisizowiana na kipato chako. Ukiweka akiba benki weka kwa jina lako hata ukistaafu chukua pensheni kila nwezi kula kulingana na ukubwa wa pensheni usitake kuendeleza ufahari wa kuchangia michango mikubwa kwenye maharusi, nyumba za ibada au mambo ya ukoo au ujirani kama wakati ulipokuwa kazini.
Kuna mtu alikuwa jirani yangu tena kazini kwake alikuwa mkuu wa idara, alipostaafu mkewe akadai kila mtu afe na chake eti wagawane pensheni, yulenmzee akakubali shinikizo la mkewe , mkewe akadai tena kuwa wakati anaolewa hakuja na watoto hivyo apewe 50% na pia akadai watoto aliozaa na huyo mumewe ndio wagawane na baba yao 50% ya baba. Huyo baba kwa ujinga akakubali hiyo fomula akagawana na watoto 50% na mama peke yake akatia kibindoni 50%. Ya pensheni ya baba Huyo mama naisha yake yote hajawahi kuajiriwa alikuwa mama wa nyumbani akifanya biashara za hasara huku zikitegemea gharama za uendeshaji toka mshahara wa mumewe. Huyo mumewe tulimzika makaburi ya pugu kanisani ndani ya miaka isiyozidi miwili baada ya kustaafu.

Ujinga wa ujanani ndio kitanzi chako uzeeni.
Wanaume ni kazi,.......mimi sitakua tayari kubembeleza ndoa hata kama tumezaa watoto zaidi ya 3 ykidetect tatizo mapema react mapema uondokane nalo mapema.
 
Uweke akiba au usiweke mwisho wa siku utakufa tu!
Mkuu suala sio kufa suala muhimu umekufa je?inasikitisha sanaa mtu alie kua meneja ws tasisi kufa kwasbb ya lishe mbovu, kupikiwa na majirani nk.
 
Ni kweli mkuu, kwenye hii dunia usitegemee kuwa nikimsaidia mtu au nikitimiza majukumu yangu nitapata fadhila, maisha hayako hivyo. Kinachotakiwa, kipaumbele namba moja iwe ni wewe, wengine wanafuatia. Hata ukifa leo utazikwa nanutasahaulika na hata wale ambao walikuwa karibu nao. Hakuna mbadala wa maisha yako.
Nimejifunza hili in a hard way, nitazingatia hili zaidi. Shukrani sana mkuu
 
Ukitegemea watoto ulio lipia ada kubwa kwenye private schools kukutunza au ukitegemea mke ulio mvumilia siku zote eti ndo atakutunza au ukitegemea hiyo pession 33% yako na bima ya afya ulio pata baada ya kustaafu, hapo umechemsha mkuu.....

Maisha ya kustaafu yanahitaji cash flow or cash in hand sio assets au promises, mzee mstaafu jirani mwenye watoto 5 gradutes kati yao wawili wako wingereza watatu wameajiriwa serikalini, amekufa kifo cha kimasikini sana 'died like apauper' wakati mke wake ameenda kutembelea bint yake mkoani takribani miezi 3 sasa hayupo.....kweli meneja mstaafu ndo wakukosa sh 10,000 kuwayishwa dispensary, ndo wa kupewa chakula na wapangaji?????

Rai yangu if you are 45+ anza kujianda jinsi ya kustaafu kwa heshima uza baadhi ya mari zako utunze pesa sio sehemu moja never ever over trust your wife, hao wa dudu tukikua wana badilika na kuhamia kwa watoto wao. Kwa kweli nime umia sanaa mzee kajitahidi sanaa kutunza familia uwe first class nyumba yake ni 300m to 500m worthy ila bado maiti iko hospitali next of kin bado hawajafika hi ni siku ya pili.
Haya ni makosa ya kimalezi, period!

Watoto waliolelewa katika imani ya dini watakosea hapa na pale lakini kumtelekeza mzazi wao mazima ni ngumu! Tatizo kubwa la jamii tuliyonayo sasa ni kwamba tupo too material oriented. Watoto wanalelewa katika mazingira yalioyojaa fikra za kufanikiwa maishani ndio main goal! wanapelekwa mashule ya gharama ili wawe na nafasi nzuri zaidi ya kufanikiwa maishani na kinyume chake mafunzo ya kiimani yamekuwa ignored juu yao.

Mbaya zaidi sasa hata huko wanapopaswa kupewa mafunzo ya kiimani na humility ambapo hupelekwa once in a while, wakienda wanaishia kupata maombi ya kufanikiwa maishani!!!
 
duh basi wastaafu naowajua mie sio mnaowajua nyie..mtu alikua manager hakosi kupokea 1m@ unashindwa kata bima ys mwaka mzima?mko wapi kwani nyie
Wengi wakiwa na pesa wanajisahau, tena asimilia kubwa watu wanajisahau sana.
 
Unaonaje ungewahimiza wapiganie mabadiliko ya mfumo na uwajibikaji serikali ili na sisi tuwe na mifumo ya kustaafu kama Ulaya ambapo mtu akistaafu anaishi maisha ya raha? I mean hili jambo la kuhimiza kila mfanyakazi awe na kitega uchumi cha kumsitiri wakati wa kustaafu practically haliwezekani na siyo suluhisho la kudumu ila ni matokeo ya kuwa na uongozi mbovu. Tujaribu kutatua tatizo ni siyo kulizunguka.
Sahihi
 
Wengi wetu hatuelewi Kuwa ni wajibu wetu wazazi kutunza na kusomesha watoto lakini sio wajibu wa mtoto kutunza mzazi.Somesha huku na wewe ukiweka akiba Yako pamoja na miradi Yako ya kukupa mtindi wa kusogeza uzee.Huyo Mzee nyumba ya 300m inaonekana alikuwa vizuri kiuchumi ameshindwaje kuweka mazingira ya watoto Kuja kukopa kwake hata kama Wana kazi zao?.
Sahihi
 
Back
Top Bottom