Ukitegemea watoto ulio lipia ada kubwa kwenye private schools kukutunza au ukitegemea mke ulio mvumilia siku zote eti ndo atakutunza au ukitegemea hiyo pession 33% yako na bima ya afya ulio pata baada ya kustaafu, hapo umechemsha mkuu.....
Maisha ya kustaafu yanahitaji cash flow or cash in hand sio assets au promises, mzee mstaafu jirani mwenye watoto 5 gradutes kati yao wawili wako wingereza watatu wameajiriwa serikalini, amekufa kifo cha kimasikini sana 'died like apauper' wakati mke wake ameenda kutembelea bint yake mkoani takribani miezi 3 sasa hayupo.....kweli meneja mstaafu ndo wakukosa sh 10,000 kuwayishwa dispensary, ndo wa kupewa chakula na wapangaji?????
Rai yangu if you are 45+ anza kujianda jinsi ya kustaafu kwa heshima uza baadhi ya mari zako utunze pesa sio sehemu moja never ever over trust your wife, hao wa dudu tukikua wana badilika na kuhamia kwa watoto wao. Kwa kweli nime umia sanaa mzee kajitahidi sanaa kutunza familia uwe first class nyumba yake ni 300m to 500m worthy ila bado maiti iko hospitali next of kin bado hawajafika hi ni siku ya pili.
Sitaki kuamini kile ulichokiandika kama msingi wa hoja yako kina ukweli,
Mosi umesema ana nyumba isyiopungua 300M to 500M, Umesema amesomesha watoto, Umetaja neno wapangaji. Na umesema siku mbili next of kin hawaonekani.
Hili siyo kosa la marehemu, kwangu mimi amefanya kila alichopaswa kufanya hapa duniani, kwa maana ya kuhakikisha anawapatia watoto wake elimu bora na yeye anakuwa na nyumba bora ya kuishi.
Jambo lingine umetaja mzee kukosa chakula na kupewa chakula na wapangaji, umesema mzee kukosa elfu ya kumwahisha hospitali, umetaja mke wake kuwa kwa binti yake kwa zaidi ya miezi mitatu.
Kama ana wapangaji sidhani kama angeweza kukosa elfu 10 ya kumwahisha hospitali, kwa sababu bado alikuwa na uwezo wa kumwita mpangaji mmoja na wakaingia makubaliano akamsaidia kiasi cha hela ili aende hospital.
MKE kwenda kwa binti hili ni janga hasa kwa jamii zetu waafrika na binafsi wazazi nilishawapa msimamo wangu kama nikuja kwangu kusalimia waje wote kwa maana ya baba na mama, siwezi kumwita mama alafu baba akabaki nyumbani peke yake. Vivyo hivyo kwa baba. Unless iwe ni issue ya ugonjwa.
Kwa meneja ambaye amestaafu, sijui alikuwa ni meneja wa taasisi au kampuni ipi lakini naamini hakosi pesheni kuanzia laki 4 kwenda juu kwa mwezi + nyumba za wapangaji anakosaje elfu 10?
ALAFU unatuambie tuuze mali tutunze pesa how? una miaka mingapi wewe? hebu fikisha huo umri uuze mali utunze pesa. Wazungu wanakwambia life begins at 60yrs. Hebu fikiria una miaka 45 uuze pengine nyumba za kupangisha ili utunze hela nadhani wewe utakuwa miongoni mwa wazee wapumbavu kuwahi kutokea.
Alafu kama kweli watoto wa huyo mzee wako serikalini kwa maana ya JMT ni mkoa upi ambao watashindwa kufika nyumbani kwa muda wa siku mbili? Labda hao wa UK wanaweza kuchelewa kwa maana ya flght schedule na flight cancelations tofauti na hapo naona kama ni chumvi.