Wanaume: Acheni kutoa lifti kwa wadada

Wanaume: Acheni kutoa lifti kwa wadada

Aaaanh lift msitunyime jamani

Ila mwanaume ukiwa umeoa pakiza wanawake nyuma, sio wakae mbele ka vile mkeo
nyuma lifti hainogi.maswali hayajibiwi uzuri! lazima akae mbele ili reception ionekane.
 
Toa ulicho nacho wengine hela hawana washindwe hata kutoa lift????? Huu ni uchoyo.
Tatizo Wanawake Wengi Wanaopewa Hizo Lift, Wanataka Kupata Hiyo Nafasi Zaidi Ya Siku 1, Hii Ni Kutokana Na Matatizo Ya Kugombea Madaladala Kila Siku! HIVYO Kidume Kikimpatia Lift Tu Mtt Wa Kike Atajishau Hadi Kidume Kiingie Mtegoni, Kukiunganisha Na Hivyo Vimini Au Taiti Zenu Mnavyovaa!!! Mhhhh!! Kidume Lazima Kiingie Mtegoni, Mmekaa Ktk FOLENI Saa Zaidi Ya 2.30!!! Wee Labda Uwe Mtt Si Riziki, Lkn Rijali!!!!!
 
ndio maana sipati lift, jamaa muwe mnatupa kalift washikaji zenu....
 
ni vizuri ukafanya ila tu isiwe kama ndiyo utaratibu .. ila kiukweli inaumiza kuona mpenzi wako au mume wako anampa vibinti lifti mara kwa mara mbaya zaidi unakuta jamaa hana limit wanajiachia kwenye gari tu mara miguu ipo juu ya dashboard au kakunja juu ya kiti ... aisee mi nimemwambia mr toa lifti ila nisimkute humo ndani ya gari na kama ni muhimu sana huyo mtu kupewa lifti wakati unakuja kunifuata aisee nipe taarifa in advance ili mkifika hapo nitengeneze tabasamu langu la plastic ili asijue kama nimemind na pia hakikisha anakaa siti ya nyuma si akae mbele eti anafika ndiyo anajifanya kunipisha , kama hutaki tatizo na mimi sababu akishuka nitahakikisha hapandi tena ha ha haha si uchoyo (abiria chunga mzigo wako).. inauma unakutana na demu kakuzidi mbali halafu anapewa lifti,.... au unakufukunyua unakuta we umeingia bahati mbaya mikato wa mademu wake wa zamani ni wa aina fulani halafu ndiyo kila ukikuta katoa lifti sampuli hizo hizo inauma sana aiseee ila yote ni wivu tu .. kiukweli na wivu ha ha haha nalinda mali zangu mniache ..... makurufu kutoa lifti hapa tumekubaliana kabisa na akitoa nisijue basi..
kumbe una wivu namna hiyo miss chagga! mimi nimepiga tinted kama mwarabu,muomba lifti hawezi kujua kama kuna mtu au hamna.
mpe uhuru themeji aonje mema ya nchi.
 
ila inakera sana, kuna siku niliomba shemeji yako anipitie mahali, alivyokuja akawa na mdada alimpa lift amekaa mbele,
nikafungua nikakaa nyuma,
nikaona nakwazika nikamwambia apark napitia sokoni so atangulie,
mi huyo nikashuka nikapanda daladala tukakutana nyumbani.
Inakera haswaaa
 
Dar! mkuu hapa umeongea neon ambalo kwa kweli huu ni mtego mkubwa sana tena sana, kwa mwanaume hata kama wewe utakuwa mjanja vipi utanaswa au kutoka kwako kwenda kwake au kutoka kwake kuja kwako. Hili ni jaribu kubwa kulishinda yataka moyo kweli kweli!!
Hili jaribu limewaharibia wengi mahusiano yao.badala ya kuwa neema inakuwa tanzi
 
mimi kinachonifanya kutowapa wanaume wenzangu lift hata kama nniwafahamu ni kuwa siwaamini kabisa wanaume, unaweza ukampa lift na mwisho wa siku hata akakuua au kukujeruhi kisa anataka kukuibia.
MSIMAMO WANGU: SITAACHA KUWAPA LIFT WANAWAKE HATA SIKU MOJA.
inatokea mkuu anaanza kukuonea wivu na kukutangazia maneno yasiyofaa mtaani anaona anakujua sana! kuna mmoja nilikuwa namsaidia lifti jirani yangu.mbele nikawa nachukua pia mwanafunzi wa shule ya msingi msichana mdogo.yule jirani ninayemsaidia aliniharibia jina mtaani eti nagegeda yule kinda wa shule ya msingi.toka siku hiyo naepuka jinsia zote mpaka ulazima uwepo.
 
Kwani kumpa lift ndio mpaka uchepuke nae, ukimchekea ovyo atakuzoea kiboya,mpe lift kua serious, mambo ya kuanza kuulizana sijui wakaa wapi,wafanya kazi wapi, ohhh umependeza shabashi kwanini aache kukutega sasa, wee mpe lifti then vunga tena wa mpakiza seat za nyuma huko, wewe wadrive wafungulia mziki watulia kimyaaaaa. Akifika anaposhuka wamshusha waendelea na safari yako(HAPA MELENGA WENYE MAGARI)
akiomba namba na kesho umpitie kituoni ni jirani yako utagoma?!
 
Wananchosha wanawake wanapewa lift, wanakaa mbele na AC anawasha, mziki anaongeza sauti, nne anakunja, anavaa na nguo zetu zile ukikaa upaja nje, kumwagiwa tindikali kunahusika kwa kweli
mna miwivu kitu! kweli adui wa mwanamke ni mwanamke mwenzie!
 
Back
Top Bottom