Wanaume: Acheni kutoa lifti kwa wadada

BOB LUSE

JF-Expert Member
Jan 25, 2014
3,738
3,198
I Greet you all,

Naongelea wanaume walio katika mahusiano na wenza wao.Wanaume wenye vyombo vya usafiri kama baiskeli, bodaboda, bajaji na gari.

Wanaume wengi maisha yao ya mahusiano yanabadilika atakapojiingiza kwenye kutoa msaada wa usafiri kwa wadada, mara nyingi hizi lift zinaishia kuanzisha mahusiano au michepuko.

Wako wanaume wachache wenye nia njema wanapotoa msaada huo hawana budi kuendelea. Lakini kama wewe ni mdhaifu, weka kanuni kuwa hutasimama kupakia mwanamke kwenye chombo chako cha usafiri.

Badala yake saidia wanaume wenzio wanaoenda kutafuta maisha ili waje kuendesha vizuri familia zao. Kwa yeyote ambaye mahusiano yake au mchepuko wake aliupata katika mazingira kama haya karibu tujumuike.

Madhara ya lifti kama unayemchukua ni jirani na kwako unatakiwa umchukue kila siku, siku usipomchukua unaonyesha unaroho mbaya au umepata mwingine wa kumchukua au umemchoka, inaleta maswali.siku ukiwa na mwenza wako official unakosa amani kabisa.

Lets share wale wenye uzoefu na hii hali.
 
Siwezi kuacha kuwapa lift warembo!!! Sikumbuki kama niliwahi kutoa lift kwa mwanaume nisiemjua,na sidhani kama nitakuja kufanya hivyo!
mkuu una watosa WANA kwaajiri ya Mbunye! mweh!
 
Toa ulicho nacho wengine hela hawana washindwe hata kutoa lift????? Huu ni uchoyo.
Lifti nyingi zinaishia kupeleka wanaume wakose uaminifu kwenye mahusiano waliyonayo.madenti wengi wameishia kumegwa kwa lifti!
 
Ni nzuri ni kutoa mara moja moja ila usijenge mazoea na hao uwapao lift, si wanaume wala wanawake wenye tabia mbaya.
 
waambie wenyewe ndo wasiombe lifti..
ye akiomba na mi naomba tunakuwa tunaombana..!
kwani tatzo liko wapi..?
 
Aaaanh lift msitunyime jamani

Ila mwanaume ukiwa umeoa pakiza wanawake nyuma, sio wakae mbele ka vile mkeo
 
ni vizuri ukafanya ila tu isiwe kama ndiyo utaratibu .. ila kiukweli inaumiza kuona mpenzi wako au mume wako anampa vibinti lifti mara kwa mara mbaya zaidi unakuta jamaa hana limit wanajiachia kwenye gari tu mara miguu ipo juu ya dashboard au kakunja juu ya kiti ... aisee mi nimemwambia mr toa lifti ila nisimkute humo ndani ya gari na kama ni muhimu sana huyo mtu kupewa lifti wakati unakuja kunifuata aisee nipe taarifa in advance ili mkifika hapo nitengeneze tabasamu langu la plastic ili asijue kama nimemind na pia hakikisha anakaa siti ya nyuma si akae mbele eti anafika ndiyo anajifanya kunipisha , kama hutaki tatizo na mimi sababu akishuka nitahakikisha hapandi tena ha ha haha si uchoyo (abiria chunga mzigo wako).. inauma unakutana na demu kakuzidi mbali halafu anapewa lifti,.... au unakufukunyua unakuta we umeingia bahati mbaya mikato wa mademu wake wa zamani ni wa aina fulani halafu ndiyo kila ukikuta katoa lifti sampuli hizo hizo inauma sana aiseee ila yote ni wivu tu .. kiukweli na wivu ha ha haha nalinda mali zangu mniache ..... makurufu kutoa lifti hapa tumekubaliana kabisa na akitoa nisijue basi..
 
Makubwa haya

Dar! mkuu hapa umeongea neon ambalo kwa kweli huu ni mtego mkubwa sana tena sana, kwa mwanaume hata kama wewe utakuwa mjanja vipi utanaswa au kutoka kwako kwenda kwake au kutoka kwake kuja kwako. Hili ni jaribu kubwa kulishinda yataka moyo kweli kweli!!
 
Back
Top Bottom