Wanasiasa wameshindwa kuwa na tafsiri moja ya nani ni machinga?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
18,330
33,954
Mtu ana mtaji wa shilingi milioni tatu lakini anaitwa mmachinga Kwa kuwa anapanga bidhaa zake barabarani na Halipi Kodi!

Mwingine ana mtaji kama huo huo lakini kwa kuwa anauza bidhaa zake kwenye fremu, anaitwa mfanyabiashara na Anatozwa Kodi.

Hivi kigezo cha kuitwa mmachinga ni jinsi mtu anavyofanya biashara ama ni kiwango cha mtaji wake kibiashara na mauzo yake kwa siku?
 
kusema kweli hata sisi serikali mmetuchanganya sana na ndio maana hata sisi tumeamua kuwachanganya kwenye umeme! na mambo mengine!,kama wananchi kaeni mjitandabue ili tuwaelewe natujue nani ni machinga na nani si machinga!..
 
Kigezo cha mtu kuitwa machinga siyo namna ya ufanyaji wa biashara bali ni kiwango cha mtaji alichokiwekeza kwenye mtaji wake. Justifiably machinga anapaswa kuwa mtu yeyote mwenye mtaji ambao uko chini ya milioni 5 bila kujalisha namna na mahali anapofanyia biashara.

Ila kwakuwa serikali yetu inanjaa kielelezo cha machinga na biashara zake ni namna anavyoteseka katika utafutaji wake. Hata kama ana mtaji wa milioni 6 lakini akawa anauza karanga, mkaa, kuni kavu, mbolea za mafungu, majani ya nguruwe na ng'ombe, dagaa na samaki chanjani kwa kutumia wauzaji tofauti huyo watamuona mchovu na kumuweka nje ya mfumo wa kodi. Lakini kwa mtaji huohuo wa milioni 6 mtu akianzisha duka la vinywaji, TRA na halmashauri lazima watashughulika naye kulipa kodi.
Kiufupi, ukiichanganya serikali umetoboa.
 
kusema kweli hata sisi serikali mmetuchanganya sana na ndio maana hata sisi tumeamua kuwachanganya kwenye umeme! na mambo mengine!,kama wananchi kaeni mjitandabue ili tuwaelewe natujue nani ni machinga na nani si machinga!..
Dah😅
 
Back
Top Bottom