Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 21,340
- 51,895
Kwema Wakuu!
Wanaoshauri timu moja itolewe wanajaribu kueleza na kumpa taarifa Rais kuwa hakubaliki. Au tuseme wanajaribu kumtisha Rais kuwa kwa hali ilivyo hakubaliki.
Katika lugha za kisaikolojia mtu akisema kuwa, hakuna haja ya kuchapisha fomu nyingi za kuwania Urais au nafasi fulani. Hiyo inatoa tafsiri kuwa kuna hofu na mashaka ya kutokukubalika. Au kuogopa dharura za hapa na pale.
Nafikiri, ushauri mzuri ni kuwaacha Watu wachukue fomu. Tena ingefaa Rais mwenyewe kwa kujiamini kabisa ndiye aseme Watu wajitokeze kuchukua fomu ili ajipime na aonyeshe kuwa yeye ni kiongozi wa Watu na anakubalika.
Hiyo kasumba mbaya ya Wazee wetu tena tunaowaheshimu ya kusema ati mgombea akiwa madarakani asipate upinzani mpaka aongoze awamu mbili ni kasumba ya kikatili, dhulma, ukandamizaji wa haki za raia wa nchi hii ambao wanahitaji kuwania nafasi hizo.
Na jambo lolote ambalo ni dhulma, ukandamizaji na ukatili Watibeli hatuvutiwi nalo. Huo utaratibu ni utaratibu wa kidhulma.
Ni haki fomu zitolewe nyingi wagombea wagombea na atakaye pendwa zaidi achaguliwe.
Ni kweli kuwa, fomu zikitolewa nyingi zitadhihirisha nani anawatu wengi.
Ni akili, kuwapa Watu uhuru wa kupima na kulinganisha viongozi.
Ni upendo kutoa Haki kwa kila mtu anayetaka kuwania nafasi hizo.
Nawatakia mwaka mpya mwema wote.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam