Suluhisho la mgogoro wa Machinga jijini Mwanza

Undava King

JF-Expert Member
Aug 11, 2017
3,205
5,333
Niseme kuwa imefikia wakati serikali ya mkoa na uongozi wa jiji waketi meza moja kulimaliza hili tatizo ambalo limekuwa na mvutano wa muda mrefu wa kimaslahi kati ya serikali na wamachinga juu ya wapi ni eneo sahihi la kufanyia biashara.

Twatambua kuwa jiji lina mipaka yake kwa maana ya kila manispaa ndani ya jiji ina njia zake na mapendekezo yake juu ya wapi wanahitaji machinga wahamishiwe ndani ya eneo lao la utawala.

Lakini unapodili na mfanyabiashara haina tofauti na kudili na mwanasiasa kwa kuwa wote hitaji lao ni WATU, hivyo basi ni vizuri kumpa mwenzako sikio juu ya malalamiko yake na ukatafuta njia nzuri ya kulitatua tatizo pasipo kuumizana pande zote mbili wakati mkihakikisha malengo na maslahi yenu yanapatikana ilivyokuwa imepangwa.

Kitendo cha kumwondoa mmachinga penye soko na kumpeleka eneo ambalo halina biashara au mzunguko wa pesa kwa mfanyabiashara huu kwake ni ukatili, lakini kwa upande wako kuna vingi sana umefanikiwa kuanzia makusanyo, mipango miji, mazingira n.k

Hivyo basi kuifanya isiwe ndefu haya hapa ni mapendekezo yangu katika hili:-

1. Jengeni Machinga complex katika mazingira yaleyale ila yawe ya kisasa na yenye kukidhi mahitaji na hadhi ya mahali husika mfano kuna haja gani ya kumhamisha mmachinga MAKOROBOI na kumpeleka relini huko voil au mkuyuni,

Wakati unaweza kubomoa majumba na mabanda mabovu mabovu yanayolizunguka eneo hilo la katikati ya jiji na ukasimamisha jengo kuu moja la ghorofa moja tu ambalo linawa-accomodate wamachinga wote wa eneo hilo kwa sasa na waliobaki wangeangaliziwa pahala pengine.

-Kwanza hii inaongeza thamani,mpangilio na mandhari ya jiji
-Pili ni njia rahisi ya kuepuka migogoro na machinga ikiwa kama suluhu ya muda mfupi.
-Tatu inakuepushia kuwa na miradi mingi White elepant mfano kumtoa mfanyabiashara katikati ya mji na kumjengea machinga complex sehemu isiyo rafiki kibiashara kwa muda husika matokeo yake hamna cha ROI zaidi ya kuishia kuwatimua kila wakionekana wamerudi barabarani na pale mlipowatimua mwanzo.

2. Maeneo ya kuwahamishia wafanyabiashara wadogo wadogo (katika plani ya muda mrefu) ifanyiwe tafiti za kina za kitaalamu zikiwahusisha pia wafanyabiashara wenyewe kwa kipindi kirefu katika kubaini fursa za kibiashara katika maeneo husika kabla ya kutoa maamuzi ya muda mfupi ya kushtukiza ambayo mara nyingi huwa yanakuwa na matokeo hasi.

3. "Machinga haitaji maghorofa" ila haimaanishi anahitaji mazingira duni na mabanda mabanda bali machinga anahitaji WATEJA na wateja wa machinga ni watanzania ambao utamaduni huo wa kukwea ngazi kupanda ghorofa ya sita kwenda kuchagua ndala au fulana hawana,

Hivyo basi ukisha-identify soko na eneo sahihi linalomfaa mmachinga jitahidi kujenga structure rafiki ndani ya Paa moja waache wafanye shughuli zao humo kwa amani na jengo lisizidi ghorofa moja kwa kuwa bado utawapa ugumu wa kufanya shughuli zao.

4. Turekebishe mifumo yetu ya uongozi wa jiji, kwani kukosekana kwa Coordination nzuri kati ya manispaa moja inayojinasibu ni jiji na manispaa nyingine inayojiita manispaa, utengeneza loop hole kubwa ya kuchelewesha maamuzi inayoruhusu wafanyabiashara wadogo wadogo kutoka manispaa moja kuweza kuhamia nyingine pasipo kizuizi na kuendeleza shughuli zao zilizozuiliwa mahali pengine pa utawala.

5. Bajeti kwa ajili ya shughuli hii itengwe na ichukuliwe serious katika utekelezaji na wahusika,hili mwisho wa siku mtanzania mfanyabiashara na serikali yake wote wanufaike na jasho lao.
 
njia ya kuzuiya machinga sio mwanza tu serikali kuwekeza kwenye kilimo chenye tija na masoko hili vijana lime wauze wanunue boda miziki mkubwa magali nk sio akili yote kuweka kwenye bwawa la umeme na leli na madalaja tungu tupate uhuru hakuna rais alie wai kuekeza kwenye kilimo
 
Back
Top Bottom