Hawa ndio wanasiasa ambao tayari wameshapitishwa kimkakati kuwa wabunge katika majimbo yao ya zamani, Kinachosubiriwa ni wao kutangazwa tu

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Sep 9, 2020
6,860
12,293
Habari za asubuhi wanaJF wenzangu?

Ndugu zangu... kama ilivyo ada, mimi huwa sipendi kuficha ficha mambo haswa yanayohusiana na maslahi ya taifa letu, hata kama mambo hayo kuna watu yatawagusa na kuwaumiza au kuua mipango yao, hiyo ni shauri yao, kikubwa mimi nafikisha ujumbe ili kila mtu aufahamu.

Mada yangu ya leo, ningependa niwazungumzie wanasiasa ambao wana uhakika wa 100 kwa 100 kuchukua majimbo ya ubunge aidha katika majimbo mapya watakayoenda 'kuzuga' watu kugombea, au kurudi kupewa kushikilia tena yale majimbo yao ya zamani ambayo waliyakosa au walishindwa kuyatetea katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Nitaweka baadhi ya sababu na picha hapo chini ili mtu mwenye akili aweze kufungua akili yake vizuri, afahamu na kuelewa kile nilichoandika. Najua kila alie katika mpango huo wa kupewa ubunge ana chawa wake katika mitandao kwa ajili ya kumtetea na kumpigania, lkn hilo halitoondoa uelewa wa wale wenye akili na uwezo wa kuelewa mambo kwa haraka. Yafuatayo ni majina ya wahusika na ufafanuzi wake hapo chini.

1. Freeman Mbowe.
Huyu ni mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo (chadema) baada ya kuonekana kuwa anaunga mkono misimamo mikali ya chama chake katika kupambana na serikali, na pia kuonesha kuunga mkono msimamo wa chama wa kutokushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa 2024, na ule mkuu wa 2025 mpaka itakapoundwa tume huru na katiba mpya, wazee wa chama tawala walikaa chini wakajadili jinsi ya kukituliza chama hicho kupitia mmiliki mkuu wa chama hicho, mwenye nguvu, uwezo na uthubutu wa kupindua meza ya misimamo yao bila kufanywa lolote, na mpuuzi yoyote. Na mtu huyo sio mungine bali ni mwenyekiti wa chama ambae yeye ndio alfa na umega wa chama hicho. Lolote asemalo ni sheria katika chama. Hata yule mzee wa 'kubwabwaja' anapofika mbele ya mwenyekiti wake hugeuka kama njiwa aliemwagiwa maji au kuku mwenye mdondo. Yani utamkuta kimyaa anaugulia maumivu rohoni tu.

Mhe. Amesha ahidiwa jimbo lake la zamani la Hai, hivyo amerudi mezani na kuipindua kutaka chama hicho kishiriki katika chaguzi zote aidha kwa kutaka au kutotaka. Watu wote kimyaa. Na mwamba anaenda kukabidhiwa kiti chake kiulaini, sijui kwa upande wa wengine kama kina Sugu, Msigwa, Lisu nk ambao hawakufanikiwa kufika ikulu kimya kimya kuonana na kina Kinana kama na wao watafanikiwa kushinda majimbo yaliobaki na uraisi kwa ujumla!

2. Zitto Kabwe.
Huyu haina haja ya kuandika mengi juu yake maana uelekeo wake unafahamika, yeye anachoangalia kwanza ni tumbo lake, mambo ya chama nk yatakuja baadae. Baada ya kuonekana kuwa hawezi kuwaongoza wapemba wenye misimamo thabiti akaamua aachie ngazi mwenyewe kabla huko mbele hajaja kuchezea bakora na kutolewa kibusha. Wapemba sio watu wa kuwachezea haswa linapokuja swala la masilahi ya chama na nchi yao kwa ujumla. Hivyo mwamba kwa kuliona hilo mapema kaamua akae pembeni ya chama ili kila atalofanya aonekane anafanya yeye binafsi kama mwanachama wa kawaida na sio msimamo wa chama.

Wapemba ni tofauti na Chadema ambapo mtu mmoja ndo anaamua mustakabali na uelekeo wa chama huku wengine wakiwa makondoo tu kwa kuogopa kushambuliwa na chawa wa mtoa maamuzi mitandaoni. Wapemba ukizingia mara moja, wao wanakuzingia mara elfu 1 mpaka unaomba poo.

Lipumba, Mbatia, Cheyo, mzee wa ubwabwa nk, hao vyama vyao havina madhara yoyote kwa chama tawala, hivyo hapakuwa na umuhimu wa kuwapa jimbo lolote wala ahadi yoyote.

Mwenye macho haambiwi tazama, na mwenye masikio halazimishwi kusikia.

Ukiona kikaoni kuna Kinana, basi ujue dili limeshamalizika salama.

JK alituasa kuwa 'za kuambiwa changanya na zako'.
images (18).jpeg
images (19).jpeg
images (17).jpeg
Screenshot_20240321-081939.jpg
Screenshot_20240308-164447.jpg
 
Yaani tangia wakae bungeni bado wanalalamika kukoswa ubungwe awamu iliyopita utadhani ubunge ndo Kila kitu kwao
Wenzako wanafanya siasa ni biashara ya kuendesha maisha yao. Hivyo wakikosa ubunge inamaana biashara yao inakuwa imeyumba na pengine kufa kabisa.
 
Nusu mkate itaenda kutokea kwa namna nyingine ya kuwaumiza wapinzani hasa Chadema, labda nusu mkate itawanufaisha zaidi vyama vidogo dogo kama CUF, ACT na NCCR mageuzi.

Nusu mkate haina maana kama wapinzani watapewa tu kila jimbo wanalokubalika kirahisi, CCM sio chama cha wahubiri injili.

Nachoona kitachoenda kutokea, kama ikitokea Chadema wakashinda Tarime Mjini, basi Tarime Vijijini watashindwa hata kama walipata kura za kutosha..

Chadema wakishinda Moshi Mjini, basi Moshi Vijijini lazima wapigwe chini hata kama walipata kura za kutosha.

Hapa itakuja ile kasumba ya kusema Chadema ni chama kilichojisimika zaidi mijini ili kuudanganya umma, huku jamaa wakiwa wameshatimiza malengo yao.

Kama kelele za malalamiko zikizidi, watakuja tena waseme mbona pale mlishinda kwa tume hii mnayoilalamikia, kubalini mmeshindwa kihalali, biashara inaishia hapo.
 
Nusu mkate itaenda kutokea kwa namna nyingine ya kuwaumiza wapinzani hasa Chadema, labda nusu mkate itawanufaisha zaidi vyama vidogo dogo kama CUF, ACT na NCCR mageuzi.

Nusu mkate haina maana kama wapinzani watapewa tu kila jimbo wanalokubalika kirahisi, CCM sio chama cha wahubiri injili.

Nachoona kitachoenda kutokea, kama ikitokea Chadema wakashinda Tarime Mjini, basi Tarime Vijijini watashindwa hata kama walipata kura za kutosha..

Chadema wakishinda Moshi Mjini, basi Moshi Vijijini lazima wapigwe chini hata kama walipata kura za kutosha.

Hapa itakuja ile kasumba ya kusema Chadema ni chama kilichojisimika zaidi mijini ili kuudanganya umma, huku jamaa wakiwa wameshatimiza malengo yao.

Kama kelele za malalamiko zikizidi, watakuja tena waseme mbona pale mlishinda kwa tume hii mnayoilalamikia, kubalini mmeshindwa kihalali, biashara inaishia hapo.
Hiki ulichoandika ni mawazo yako tu mwenyewe ila mwenyekiti na team yake wameshaamua kushiriki n watashiriki tu. Labda nikuulize maswal matatu tu hapo chini

1. Unataka kusema wewe una maono kuliko mwenyekiti wa chama ambae amekubali chama chake kiingie kwenye chaguzi zote mbili na kutupilia mbali mapingamizi yote ya kupinga kushiriki chaguzi za serikali ya mitaa na ule mkuu wa 2025?

2. Kwani mwenyekiti hana washauri wa chama ambao hawakuliona hili uliloandika hapa?

3. Kama mwenyekiti ameamua kulazimisha chama kishiriki kwa masilahi ya tumbo lake mwenyewe, wewe unashauri nini kwa wafanya maamuzi wengine wa chama ambao hawakubaliani na msimamo wa mwenyekiti?
 
Back
Top Bottom