Uchaguzi 2020 Wanasheria, Tusaidieni. Je, kuna uwezekano wa Tundu Lissu kuenguliwa na NEC kugombea Urais kwa kutumia kigezo cha Uadilifu wa Mke wa Kaisari?

Sasa Paskali unaenda mbele na kurudi nyuma? Kwamba wewe ndio ulimshauri agombee urais halafu unakuja tena kuleta hoja za kuenguliwa kwake. Hujioni kama ni mnafiki fulani hivi mahiri ambaye unataka kuwa Mr. Nice upendwe na kila mtu?

Declaration yako kuwa "kwa sasa ni kada wa ccm", inalenga nini?
Hili jamaa linacheza na upepo,linajua kwa vyovyote kura zitaibwa na CCM kubaki madarakani,na huenda kukawa na rais kufumua baadhi ya idara na taasisi za serikali na teuzi mpya kuwepo,so linawinda kauteuzi.
 
"Innocent until proven guilty", hii haijalishi aina ya kesi: hata kama ana ni kesi za jinai.
Hebu jiulize, vipi unapomuengua halafu mahakama ikamuona hana hatia katika kesi zote, Je, utarudia uchaguzi kumrudishia haki yake uliyompoka?
 
1. "Huwezi kuwa mwanaharakati na mgombea urais kwa wakati mmoja, lazima uchague moja"
2. Huwezi kuwa mchambuzi huru wa mambo ya siasa ilhali wewe ni kada mtiifu wa chama cha siasa, wewe umechagua siasa, baki huko!
3. Hata katika andishi lako unajiumauma tu, huna tena mtririko wa hoja. Para moja inapinga para iliyofuata!!
Uchambuzi wako umesha Rest in Peace!
nimemsoma nimeshindwa kumuelewa
 
Nina mawili kwako comrade. Not a legal perspective but simply logical:

1. Ushauri kwako binafsi for your own well being:
Huu uzi wako umedhamiria kuwachochea wapinzani na usijeshangaa kuwa unaweza kuwa qualified huko baadaye na ICC kama "instigation to trigger partsan-driven hate and violence". Kwa hiyo usione ajabu kwa wewe kujikuta u miongoni mwa watakaoburuzwa ICC when sh..t hits the fan!

2. Matumizi ya lugha yenye staha kwa presidential candidate:
Hapa chini nime-quote jinsi ulivyomshambulia Tundu Lissu kwa kauli zake ulizoziita hazifai kwa mtu anayewania urais. Lakini inaonekana umejisahaulisha kidogo kuhusu kauli zinazotolewa na JPM huku akiwa rais ambazo actually nyingi ni worse kuliko za Lissu ambaye hata siyo rais. So, ushauri huu au hili karipio lako ungelielekeza kwa mwenyekiti wa chama chetu CCM kwanza kabla hujaanza kuwashambulia kina Lissu. Ondoa boriti lililoko ndani ya jicho lako badala ya kung'ang'ania kuondoa kibanzi kilichomo ndani ya jicho la mwingine.

Ni hayo tu, comrade!
Mkuu Magu kawanyanganya wanaccm wengi akili na wale wachache wenye akili wameamua kukaa kimya kuogopa visasi vya Magu.Waliobaki wamebaki wakisifu na kuabudu hata ujinga unaofanya na yesu wao
 
Huwa sichukulii poa hata mara moja hoja za Paschal Mayalla. Huenda ikawa kweli Mayalla anatuandaa kisaikolojia
 
Na kwa Ccm walivyo,ni bayana kabisa baadhi ya vyama wameweka wagombea kiti cha urais kwa msaada wa CCM.wengi wanetumwa na CCM ili kuzigawanya zaidi kura za uraisi.sababu wana kumbukumbu ya Ile hatari na balaa la UKAWA 2015.Watu km Membe,Lipumba na wengine wengi ni mapandikizi tu.wagombea halisi na washindani halisi Ni Mh.Magufuli na Mh.Tundu Antipas Mughwai Lissu pekee.
 
Kacheti ketu kale P ka UD hakawez kukupa majibu?
Maelezo ya Lissu pia hayawezi?

Maelezo ya wakili Mwanajf aliyeeleza humu hivi Karibun nayo hayafui dafu?

Au ulitaka kumbagaza kwa bandiko hili?

Hongera kwa ukada wa Abbas kwa ccm na hbari maelezo

Ukipinga hili tuletee bandiko la kuililia habari maelezo
 
Wanabodi,

Hili ni bandiko la swali la hoja za kisheria, wanasheria wetu humu, tusaidieni, kufuatia Tundu Lissu kuwa ni mtuhumiwa wa jinai ambayo akikutwa na hatia kutamuondolea sifa za kugombea urais, hivyo jee kuna uwezekano wa Tundu Lissu kuenguliwa na NEC kugombea urais kwa kutumia kigezo cha uadilifu wa mke wa Kaisari?.

Uandilifu wa mke wa Kaisari ni ile kutuhumiwa tuu, inamtosha Kaisari kutoa talaka bila any proof, mke wa Kaisari should be spotless, kule kutuhumiwa tuu ni doa!. Mgombea wa urais should also be spotless, as while as snow!, as clear as sky!. Hatuhitaji mtu mwenye makandokando ya jinai nyuma yake!.

Miongoni mwa sifa za kugombea urais ni pamoja na kutokuwa mjinai uliyakutwa na hatia.

Kwa vile TL anakabiliwa na kesi kadha za jinai ambazo zikikamilika na akikutwa na hatia, zitamuondolea sifa ya kugombea urais, hivyo akigombea na kushinda urais, kesi zake zote za jinai zinafutika, hivyo NEC kumpitisha TL kugombea urais ni kuingilia uhuru wa mahakama, contempt of the court, hivyo kanuni ya uandilifu wa mke wa Kaisari, itatumika kumuengua TL kugombea urais!, ili mahakama iwe huru kuendelea na kesi zake za jinai za uchochezi?.

Kufuatia possibility ya TL kutopitishwa na NEC, then mgombea wa pamoja wa upinzani ni Benard Membe, Tundu Lissu ni Pacemaker tuu wa Membe, his candidacy itaishia NEC kwa kuwekewa pingamizi ambalo litakubaliwa!.

Unapoamua kugombea urais, you have to choose in between kugombea urais au kuendelea kuwa mwanaharakati, you can't be both, mwanaharakati na mgombea urais. Ukichagua kuwa mgombea urais, uanaharakati unauweka pembeni, you speak, talk and behave like a president in waiting!, huwezi kusema hovyo, huwezi kutukana watu, huwezi kutoa tuhuma bila ushahidi, huwezi kuibagaza nchi yako kwenye media za mabeberu, halafu ukategemea utapitishwa tuu hivi hivi kugombea urais!.

Hata pingamizi la yumkini ya kuyumkinika kuhusiana na kesi za jinai zinazomkabili, japo Tanzania tunafuata mfumo wa haki wa common laws of England, "innocent until proven guilty", japo TL ni innocent, lakini anakabiliwa na kesi ambazo akikutwa na hatia, zitampotezea sifa za kuwa rais wa JMT, kwasababu kwa mujibu wa katiba yetu, mtuhumiwa wa jinai TL, akishinda urais, kesi zake zote za jinai zinapaswa kufutika, hivyo mtu akimjazia pingamizi based on this, pingamizi hilo linapita kwa urais kabisa!. Watanzania tunataka rais muadilifu, presidential material na sio rais mwanaharakati.

Angalizo hili ni muhimu sana kwa wana Chadema ambao wamehamasika sana na kupita kwa Tundu Lissu kuwa mgombea wa Chadema, hivyo angalizo hili litawasaidia washangilie kwa kiasi na kuweka akiba ya ushangiliaji wao, ili wasije wakapata psychological depression kutokana na too high expectations on TL, akienguliwa na NEC, kitakachofuata ni despair na psychological depression, ila kwa kila mwaka Chadema atakayelisoma bandiko hili, holi likitokea litakuwa na less impact, because they had some prior info. Wata despair tuu lakini hawatapata psychological depression.

Wanasheria wetu tusaidieni.

NB. Japo DPP hapaswi kuingiliwa na mamlaka yoyote, kama ni kweli Tanzania tunataka uchaguzi Mkuu ujao uwe huru na wa haki, na Tundu Lissu ndie mgombea pekee anayeweza kuleta challenge ya ukweli kwa mgombea wa CCM, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, then nashauri DPP aitwe, aombwe kufuta kwa noble, kesi zote za jinai zinazomkabili Tundu Lissu ili Tundu Lissu awe spotless, kusitokee sababu zozote za NEC kumuengua.

Ikitokea Lissu ni kweli ameenguliwa na NEC ili kutoingilia uhuru wa mahakama, sisi waelewa wote tutaelewa, lakini its very unfortunately kwa wafuasi wake na mashabiki wake, hawataelewa!, watadhani Lissu anaonewa na hata kudhani kuwa serikali ya CCM inamuhofia sana Tundu Lissu, na kumuona ni tishio hivyo wameitumia NEC kumuengua!. Kelele zao zitakuwa sio za kitoto!.

Kwa track record ya kazi nzuri ya JPM kwa Watanzania, CCM itashinda kwa ushindi wa kishindo mapema asubuhi, hivyo tusiwape sababu za kutupigia makelele, serikali sikivu ya CCM, ihakikishe Lissu anagombea ili kuuthibitishia ulimwengu uchaguzi Mkuu wa Tanzania ni uchaguzi huru na wa haki.

Background.
Kwa wasionijua, mimi ni Kaka yake na Tundu Lissu, nilimtangulia shuleni Ilboru, na ni mimi ndie mtu wa mwanzo kumshauri Lissu agombee urais
Uchaguzi 2020 - Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha uwezo zaidi ya Magufuli!

Declaration of Interest.
Mimi Pascal Mayalla, kwa sasa ni kada wa Chama cha Mapinduzi, CCM, kwa good track record ya JPM aliyoyafanya kipindi cha kwanza awamu yake hii ya tano, yanajieleza wazi, hivyo JPM hana mpinzani wala mshindani, ni clear sweet victory.

Miongoni mwa sisi wana CCM wapya, tunapenda kuona sio CCM inashinda tuu, bali CCM inashinda kwa haki katika uchaguzi Mkuu ulio huru na wa haki ndio maana tumetoa ushauri huu kwa chama chetu.

Ushindi Mtamu ni Ushindani ktk Uwanja sawa, Sio Ule wa Mezani! Magufuli, Kasi yako ni Ushindi wa Kishindo CCM. Ruhusu Ushindani wa Haki, Sawa na Wazi!

Na ndio maana tunapenda sana kusitokee jambo lolote la kusababisha Lissu asigombee, ili kupunguza kelele mbele ya safari.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali
THE MOST DANGEROUS POST AT THE MOST SENSITIVE TIME. Imagine haya unayoyataka ambayo yanaonekana yako planned kwani wewe pia ni mwanasheria, muonekano wako kwa upande hasi kwako utakuwaje, binafsi umejipangaje. Inawezekana wakati unaandika POST hii wewe uliishia kwa Lissu ukasahau kuwa anakundi kubwa zaidi ambalo limewekeza kwake na huenda liko tayari kwa lolote, kumbuka siku zote shabiki hasikii lolote kuhusu kipenzi chake.
 
LISU MTEULE??
Sikusema Lisu ni mteule, lakini sikatai Kuwa anaweza Kuwa mteule. Harald wewe unaweza Kuwa mteule. Ni Siri kubwa aijuaye ni Mungu tu. Usitumie nguvu Sana kumzimisha mtu, usijejikuta unapambana na Mungu. Achilia mambo yaende kiasili na sanasana omba Mungu wako audhihirishe ukweli. Usijisumbue Sana kuzuia mafuriko ya mto kwa kiganja chako Cha mkono.
 
Ukichagua kuwa mgombea urais, uanaharakati unauweka pembeni, you speak, talk and behave like a president in waiting!, huwezi kusema hovyo, huwezi kutukana watu, huwezi kutoa tuhuma bila ushahidi, huwezi kuibagaza nchi yako kwenye media za mabeberu, halafu ukategemea utapitishwa tuu hivi hivi kugombea urais!.

Mbona kama umeshahukumu?

Hapo amatoa na hukumu kabisa!na kama suala lipo mahakamani unalisemea la Nini sasa unataka kuifundisha kazi tume maana unatoa maelekezo ya Nini tume ikifamye juu ya Tundu Lisu!Paskali ni I bwana!
 
Wanabodi,

Hili ni bandiko la swali la hoja za kisheria, wanasheria wetu humu, tusaidieni, kufuatia Tundu Lissu kuwa ni mtuhumiwa wa jinai ambayo akikutwa na hatia kutamuondolea sifa za kugombea urais, hivyo jee kuna uwezekano wa Tundu Lissu kuenguliwa na NEC kugombea urais kwa kutumia kigezo cha uadilifu wa mke wa Kaisari?.

Uandilifu wa mke wa Kaisari ni ile kutuhumiwa tuu, inamtosha Kaisari kutoa talaka bila any proof, mke wa Kaisari should be spotless, kule kutuhumiwa tuu ni doa!. Mgombea wa urais should also be spotless, as while as snow!, as clear as sky!. Hatuhitaji mtu mwenye makandokando ya jinai nyuma yake!.

Miongoni mwa sifa za kugombea urais ni pamoja na kutokuwa mjinai uliyakutwa na hatia.

Kwa vile TL anakabiliwa na kesi kadha za jinai ambazo zikikamilika na akikutwa na hatia, zitamuondolea sifa ya kugombea urais, hivyo akigombea na kushinda urais, kesi zake zote za jinai zinafutika, hivyo NEC kumpitisha TL kugombea urais ni kuingilia uhuru wa mahakama, contempt of the court, hivyo kanuni ya uandilifu wa mke wa Kaisari, itatumika kumuengua TL kugombea urais!, ili mahakama iwe huru kuendelea na kesi zake za jinai za uchochezi?.

Kufuatia possibility ya TL kutopitishwa na NEC, then mgombea wa pamoja wa upinzani ni Benard Membe, Tundu Lissu ni Pacemaker tuu wa Membe, his candidacy itaishia NEC kwa kuwekewa pingamizi ambalo litakubaliwa!.

Unapoamua kugombea urais, you have to choose in between kugombea urais au kuendelea kuwa mwanaharakati, you can't be both, mwanaharakati na mgombea urais. Ukichagua kuwa mgombea urais, uanaharakati unauweka pembeni, you speak, talk and behave like a president in waiting!, huwezi kusema hovyo, huwezi kutukana watu, huwezi kutoa tuhuma bila ushahidi, huwezi kuibagaza nchi yako kwenye media za mabeberu, halafu ukategemea utapitishwa tuu hivi hivi kugombea urais!.

Hata pingamizi la yumkini ya kuyumkinika kuhusiana na kesi za jinai zinazomkabili, japo Tanzania tunafuata mfumo wa haki wa common laws of England, "innocent until proven guilty", japo TL ni innocent, lakini anakabiliwa na kesi ambazo akikutwa na hatia, zitampotezea sifa za kuwa rais wa JMT, kwasababu kwa mujibu wa katiba yetu, mtuhumiwa wa jinai TL, akishinda urais, kesi zake zote za jinai zinapaswa kufutika, hivyo mtu akimjazia pingamizi based on this, pingamizi hilo linapita kwa urais kabisa!. Watanzania tunataka rais muadilifu, presidential material na sio rais mwanaharakati.

Angalizo hili ni muhimu sana kwa wana Chadema ambao wamehamasika sana na kupita kwa Tundu Lissu kuwa mgombea wa Chadema, hivyo angalizo hili litawasaidia washangilie kwa kiasi na kuweka akiba ya ushangiliaji wao, ili wasije wakapata psychological depression kutokana na too high expectations on TL, akienguliwa na NEC, kitakachofuata ni despair na psychological depression, ila kwa kila mwaka Chadema atakayelisoma bandiko hili, holi likitokea litakuwa na less impact, because they had some prior info. Wata despair tuu lakini hawatapata psychological depression.

Wanasheria wetu tusaidieni.

NB. Japo DPP hapaswi kuingiliwa na mamlaka yoyote, kama ni kweli Tanzania tunataka uchaguzi Mkuu ujao uwe huru na wa haki, na Tundu Lissu ndie mgombea pekee anayeweza kuleta challenge ya ukweli kwa mgombea wa CCM, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, then nashauri DPP aitwe, aombwe kufuta kwa noble, kesi zote za jinai zinazomkabili Tundu Lissu ili Tundu Lissu awe spotless, kusitokee sababu zozote za NEC kumuengua.

Ikitokea Lissu ni kweli ameenguliwa na NEC ili kutoingilia uhuru wa mahakama, sisi waelewa wote tutaelewa, lakini its very unfortunately kwa wafuasi wake na mashabiki wake, hawataelewa!, watadhani Lissu anaonewa na hata kudhani kuwa serikali ya CCM inamuhofia sana Tundu Lissu, na kumuona ni tishio hivyo wameitumia NEC kumuengua!. Kelele zao zitakuwa sio za kitoto!.

Kwa track record ya kazi nzuri ya JPM kwa Watanzania, CCM itashinda kwa ushindi wa kishindo mapema asubuhi, hivyo tusiwape sababu za kutupigia makelele, serikali sikivu ya CCM, ihakikishe Lissu anagombea ili kuuthibitishia ulimwengu uchaguzi Mkuu wa Tanzania ni uchaguzi huru na wa haki.

Background.
Kwa wasionijua, mimi ni Kaka yake na Tundu Lissu, nilimtangulia shuleni Ilboru, na ni mimi ndie mtu wa mwanzo kumshauri Lissu agombee urais
Uchaguzi 2020 - Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha uwezo zaidi ya Magufuli!

Declaration of Interest.
Mimi Pascal Mayalla, kwa sasa ni kada wa Chama cha Mapinduzi, CCM, kwa good track record ya JPM aliyoyafanya kipindi cha kwanza awamu yake hii ya tano, yanajieleza wazi, hivyo JPM hana mpinzani wala mshindani, ni clear sweet victory.

Miongoni mwa sisi wana CCM wapya, tunapenda kuona sio CCM inashinda tuu, bali CCM inashinda kwa haki katika uchaguzi Mkuu ulio huru na wa haki ndio maana tumetoa ushauri huu kwa chama chetu.

Ushindi Mtamu ni Ushindani ktk Uwanja sawa, Sio Ule wa Mezani! Magufuli, Kasi yako ni Ushindi wa Kishindo CCM. Ruhusu Ushindani wa Haki, Sawa na Wazi!

Na ndio maana tunapenda sana kusitokee jambo lolote la kusababisha Lissu asigombee, ili kupunguza kelele mbele ya safari.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali
Paskali hujambo? Hebu jaribu kutumia japo akili ya kawaida tu, mwenye jukumu la kudhibitisha JINAI ni chombo gani? Kwanini unaleta MAHABA yako kwa JPM na CCM kwa kuanza kuongolea mambo ambayo bado hayajathibitishwa kisheria na chombo husika? Hakika WAJUMBE wa huko kawe waliona mbali sana, kama ungebahatika kwenda Bungeni bila shaka ungesumbua sana kwa hoja za kipuuzi kama akina Kibajaji, Msukuma, Nkamia na wapuuzi wenzio wengine wenye mawazo na akili za namna hii. CCM must go.
 
Back
Top Bottom