Uchaguzi 2020 Wanasheria, Tusaidieni. Je, kuna uwezekano wa Tundu Lissu kuenguliwa na NEC kugombea Urais kwa kutumia kigezo cha Uadilifu wa Mke wa Kaisari?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,879
114,528
Wanabodi,

Hili ni bandiko la swali la hoja za kisheria, wanasheria wetu humu, tusaidieni, kufuatia Tundu Lissu kufutwa ubunge kwa kosa la kukiuka maadili ya uongozi wa umma, na kosa hilo ni a disqualification ya kutogombea urais, na ukijumlisha na Lissu kuwa ni mtuhumiwa wa jinai lukuki mahakama mbalimbali, ambayo akikutwa na hatia kutamuondolea sifa za kugombea urais, hivyo jee kuna uwezekano wa Tundu Lissu kuenguliwa na NEC kugombea urais kwa kutumia kigezo cha uadilifu wa mke wa Kaisari?.

Uandilifu wa mke wa Kaisari ni ile kutuhumiwa tuu, inamtosha Kaisari kutoa talaka bila any proof, mke wa Kaisari should be spotless, kule kutuhumiwa tuu ni doa!. Mgombea wa urais should also be spotless, as white as snow!, as clear as stlill water in the glass or sky!. Hatuhitaji mtu mwenye makandokando ya jinai nyuma yake!.

Miongoni mwa sifa za kugombea urais ni pamoja na kutokuwa mjinai kwa kosa la kukiuka maadili ya uongozi wa umma ambapo alikutwa na hatia na kufutwa ubunge, hivyo kupoteza sifa za kugombea urais?.

Ukiondoa hilo kosa la ukiukwaji maadili ya uongozi wa umma ambalo ni direct disqualification kugombea urais, na kwa vile TL anakabiliwa na kesi kadha za jinai ambazo zikikamilika na akikutwa na hatia, zitamuondolea sifa ya kugombea urais, hivyo akigombea na kushinda urais, kesi zake zote za jinai zinafutika, hivyo NEC kumpitisha TL kugombea urais ni kuingilia uhuru wa mahakama, contempt of the court, hivyo kanuni ya uandilifu wa mke wa Kaisari, itatumika kumuengua TL kugombea urais!, ili mahakama iwe huru kuendelea na kesi zake za jinai za uchochezi?.

Kufuatia possibility ya TL kutopitishwa na NEC, then mgombea wa pamoja wa upinzani ni Benard Membe, Tundu Lissu ni Pacemaker tuu wa Membe, his candidacy itaishia NEC kwa kuwekewa pingamizi ambalo litakubaliwa!.

Unapoamua kugombea urais, you have to choose in between kugombea urais au kuendelea kuwa mwanaharakati, you can't be both, mwanaharakati na mgombea urais. Ukichagua kuwa mgombea urais, uanaharakati unauweka pembeni, you speak, talk and behave like a president in waiting!, huwezi kusema hovyo, huwezi kutukana watu, huwezi kutoa tuhuma bila ushahidi, huwezi kuibagaza nchi yako kwenye media za mabeberu, halafu ukategemea utapitishwa tuu hivi hivi kugombea urais!.

Hata pingamizi la yumkini ya kuyumkinika kuhusiana na kesi za jinai zinazomkabili, japo Tanzania tunafuata mfumo wa haki wa common laws of England, "innocent until proven guilty", japo TL ni innocent, lakini anakabiliwa na kesi ambazo akikutwa na hatia, zitampotezea sifa za kuwa rais wa JMT, kwasababu kwa mujibu wa katiba yetu, mtuhumiwa wa jinai TL, akishinda urais, kesi zake zote za jinai zinapaswa kufutika, hivyo mtu akimjazia pingamizi based on this, pingamizi hilo linapita kwa urais kabisa!. Watanzania tunataka rais muadilifu, presidential material na sio rais mwanaharakati.

Angalizo hili ni muhimu sana kwa wana Chadema ambao wamehamasika sana na kupita kwa Tundu Lissu kuwa mgombea wa Chadema, hivyo angalizo hili litawasaidia washangilie kwa kiasi na kuweka akiba ya ushangiliaji wao, ili wasije wakapata psychological depression kutokana na too high expectations on TL, akienguliwa na NEC, kitakachofuata ni despair na psychological depression, ila kwa kila mwaka Chadema atakayelisoma bandiko hili, holi likitokea litakuwa na less impact, because they had some prior info. Wata despair tuu lakini hawatapata psychological depression.

Wanasheria wetu tusaidieni.

NB. Japo DPP hapaswi kuingiliwa na mamlaka yoyote, kama ni kweli Tanzania tunataka uchaguzi Mkuu ujao uwe huru na wa haki, na Tundu Lissu ndie mgombea pekee anayeweza kuleta challenge ya ukweli kwa mgombea wa CCM, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, then nashauri DPP aitwe, aombwe kufuta kwa noble, kesi zote za jinai zinazomkabili Tundu Lissu ili Tundu Lissu awe spotless, kusitokee sababu zozote za NEC kumuengua.

Ikitokea Lissu ni kweli ameenguliwa na NEC ili kutoingilia uhuru wa mahakama, sisi waelewa wote tutaelewa, lakini its very unfortunately kwa wafuasi wake na mashabiki wake, hawataelewa!, watadhani Lissu anaonewa na hata kudhani kuwa serikali ya CCM inamuhofia sana Tundu Lissu, na kumuona ni tishio hivyo wameitumia NEC kumuengua!. Kelele zao zitakuwa sio za kitoto!.

Kwa track record ya kazi nzuri ya JPM kwa Watanzania, CCM itashinda kwa ushindi wa kishindo mapema asubuhi, hivyo tusiwape sababu za kutupigia makelele, serikali sikivu ya CCM, ihakikishe Lissu anagombea ili kuuthibitishia ulimwengu uchaguzi Mkuu wa Tanzania ni uchaguzi huru na wa haki.

Background.
Kwa wasionijua, mimi ni Kaka yake na Tundu Lissu, nilimtangulia shuleni Ilboru, na ni mimi ndie mtu wa mwanzo kumshauri Lissu agombee urais
Uchaguzi 2020 - Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha uwezo zaidi ya Magufuli!

Declaration of Interest.
Mimi Pascal Mayalla, kwa sasa ni kada wa Chama cha Mapinduzi, CCM, kwa good track record ya JPM aliyoyafanya kipindi cha kwanza awamu yake hii ya tano, yanajieleza wazi, hivyo JPM hana mpinzani wala mshindani, ni clear sweet victory.

Miongoni mwa sisi wana CCM wapya, tunapenda kuona sio CCM inashinda tuu, bali CCM inashinda kwa haki katika uchaguzi Mkuu ulio huru na wa haki ndio maana tumetoa ushauri huu kwa chama chetu.

Ushindi Mtamu ni Ushindani ktk Uwanja sawa, Sio Ule wa Mezani! Magufuli, Kasi yako ni Ushindi wa Kishindo CCM. Ruhusu Ushindani wa Haki, Sawa na Wazi!

Na ndio maana tunapenda sana kusitokee jambo lolote la kusababisha Lissu asigombee, ili kupunguza kelele mbele ya safari.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali
 
Ukichagua kuwa mgombea urais, uanaharakati unauweka pembeni, you speak, talk and behave like a president in waiting!, huwezi kusema hovyo, huwezi kutukana watu, huwezi kutoa tuhuma bila ushahidi, huwezi kuibagaza nchi yako kwenye media za mabeberu, halafu ukategemea utapitishwa tuu hivi hivi kugombea urais!.

Mbona kama umeshahukumu?
 
Ukichagua kuwa mgombea urais, uanaharakati unauweka pembeni, you speak, talk and behave like a president in waiting!, huwezi kusema hovyo, huwezi kutukana watu, huwezi kutoa tuhuma bila ushahidi, huwezi kuibagaza nchi yako kwenye media za mabeberu, halafu ukategemea utapitishwa tuu hivi hivi kugombea urais!.

Mbona kama umeshahukumu?
Huyu Ataelewa tu
 
1. "Huwezi kuwa mwanaharakati na mgombea urais kwa wakati mmoja, lazima uchague moja"
2. Huwezi kuwa mchambuzi huru wa mambo ya siasa ilhali wewe ni kada mtiifu wa chama cha siasa, wewe umechagua siasa, baki huko!
3. Hata katika andishi lako unajiumauma tu, huna tena mtririko wa hoja. Para moja inapinga para iliyofuata!!
Uchambuzi wako umesha Rest in Peace!
 
ili mahakama iwe huru kuendelea na kesi zake za jinai za uchochezi?.

Unapoamua kugombea urais, you have to choose in between kugombea urais au kuendelea kuwa mwanaharakati, you can't be both, mwanaharakati na mgombea urais. Ukichagua kuwa mgombea urais, uanaharakati unauweka pembeni, you speak, talk and behave like a president in waiting!, huwezi kusema hovyo, huwezi kutukana watu, huwezi kutoa tuhuma bila ushahidi, huwezi kuibagaza nchi yako kwenye media za mabeberu, halafu ukategemea utapitishwa tuu hivi hivi kugombea urais!.
Kwani anakabiliwa na kesi gani zisizokuwa za kisiasa?
Hivi Polisi si wanatakiwa wafanye uchunguzi wa kushambuliwa kwake miaka 3 iliyopita na kutowa ripoti?
Kusema hovyo na kutukana watu nikule kuyaweka wazi maovu ya viongozi wa CCM au Serikali yake?

Pamoja na hayo,
Tahadhari yako ina Mantik sana na ndio hasa Tegemeo la dhuluma wanalotarajia CCM kulitumia.
 
Back
Top Bottom