Tundu Lissu: Mama Lowassa ni mwalimu wangu miaka 41 iliyopita

Madumbikaya

JF-Expert Member
Jun 6, 2018
638
1,902
Tundu Lissu ameyasema hayo alipotembelea familia ya Lowassa kuhani msiba kuwa amefika kumpa pole mwalimu wake aliyemfundisha darasani miaka arobaini na moja iliyopita.

Tundu Lissu amesisitiza ukimtoa Mwalimu Nyerere kwa ushawishi anayefuata ni Edward Lowassa kwa ushawishi, hivyo Taifa limepoteza mtu aliyekuwa na ushawishi sana.

Akiwa msibani kwa Lowassa Rais mstaafu Jakaya Kikwete amekiri alishawishiwa na Lowassa kugombea urais mwaka 1995 akiwa ameambatana na Samwel Sitta na Rostam Aziz.

Aidha Paul Makanda akiwa msibani amekiri Lowassa ndio mwanasiasa ambaye walimtukana lakini hakuwahi kunyanyua mdomo kumjibu mtu yeyote yule hapa Tanzania.
 
Siasa unaa sana unaa mwingi. Hapo watu wanasaka political mailage hamna kingine
 
Mke wa Lowassa Mama Regina Lowassa kafundisha wengi waliosona Ilboru miaka ile ya wakina Lissu. Mnavyosikia English ya Lissu mwalimu wake wa kwanza wa English ni mama Regina Lowassa. Lakini kafundisha wengi ikiwa pamoja na mawakili kama Chipeta na Mpuya.

Tungependa kujua mwalimu wa mpendwa wetu Magufuli wa English alipokuwa form 1.
 
Mke wa Lowassa Mama Regina Lowassa kafundisha wengi waliosona Ilboru miaka ile ya wakina Lissu. Mnavyosikia English ya Lissu mwalimu wake wa kwanza wa English ni mama Regina Lowassa. Lakini kafundisha wengi ikiwa pamoja na mawakili kama Chipeta na Mpuya.
Kwahiyo Bwana Lissu hakuwa anajua au amesoma Kiinglishi hadi alipokwenda Ilboru? Basi sawa!!!
 
Back
Top Bottom