Wanasheria, kama mkataba una mapunfufu ya aina hii, wakitupeleke mahakamani , wanaweza vipi kushinda kesi dhidi yetu?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,023
144,380
Kwa maelezo ya wanasheria mbalimbali, huu mkataba una mapungufu mengi mengine yanayoonekana kuondoa uhalali na hata maana ya mkataba wa pande mbili.

Kwa mfano, kwakuwa kwenye mkataba, Mama amesaini kwa niaba ya Serikali ya Dubai ambayo yeye hana mamlaka yoyote na wala serikali hiyo haijampa legal power yoyote ya kufanya hivyo kwa niaba yake, mpaka hapa, huu unastaili kuwa mkataba halali?

AU Serikali ya Dubai imempa Mama nguvu za kisheria(power of attorney) kufanya hivyo(kusaini kwa niaba)?

Kuwa na legal power ya aina hiyo ni kitu kisichowezekana, sasa hapa nini kilitokea kukawa na kitu kama hichi kwenye document kama hii?

Pili, kama Dubai sio nchi, mkataba huu una sifa za kuwa IGA?

Kama hauna hiyo sifa ya msingi, unaweza vipi kuwa legally binding?

Mpaka hapa, Waarabu hawa wanaweza kwenda mahakama ya usuluhisho(London) na document yenye map
uungufu kama haya na kushinda kesi?

Kwa maneno mengine,tukivunja mkataba huu, mahakama inaweza kusikiliza malalamiko ya Waarabu ili hali mkataba wenyewe unakosa sifa za kuwa mkataba?

Wanasheria tusaidieni hapa.
 
Masikini Tanganyika
masoudkipanya_1689221638827494.jpg
 
Hapa kuna Rostam walitaka kutupiga!! ashukuriwe Mungu wa mbinguni maana ameamua kuwaumbua!! yamezoea kutuibia! Tena Mungu aingilie kati wakafie mbali!
 
Back
Top Bottom