Mbeya: Hukumu kesi ya kupinga mkataba kuhitimisha mjadala wa DP World

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Leo, Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya inatarajiwa kutoa Uamuzi/Hukumu yake juu ya kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na wanaharakati wanaohoji uhalali wa Mkataba wa Ukodishwaji wa Bandari kati ya Tanzania na Dubai kupitia kampuni ya DP World.

Kuanzia Makao Makuu ya CCM Dodoma na Ofisi zake zote mikoani, CCM imeelekeza macho na masikio yake Mbeya. Amini nawaambia, kadiri ya mipango isiyo na viwango iliyopangwa na chama hiki tawala, Hukumu ya kesi ya Mbeya imebaki kama tumaini la mwisho kuhusiana na mkataba wa DP World.

CCM imepanga (huku ikiamini kuwa kesi hiyo itashindwa) kutumia Hukumu hiyo ya Mbeya kuwanyamazisha watanzania na kuishauri Serikali kuendelea na utekelezaji wa mkataba huo tata wa DP World. Nyaraka za madokezo ya kichama nilizoziona zinaonesha kuwa CCM inaisubiri kwa hamu hukumu ya leo.

Mipango hiyo ya CCM inaonesha kuwa Hukumu ya Mbeya itatumika kama fimbo na kizibo cha kuwachapa na kuwaziba wakosoaji wa mkataba huo wa DP World. Kwa maana nyingine, CCM inaamini kuwa suala la DP World linahitimishwa leo kupitia Hukumu ya Makahama Kuu ya Mbeya.

Nakitahadharisha na kukiambia chama changu, Hukumu ya Mbeya haitahitimisha jambo hili kwa wanaharakati kushinda au kushindwa kwenye kesi hiyo. Mwisho wa ukosoaji wa mkataba wa DP World ni kwa Serikali kuachana na mkataba huo tata kwakuwa watanzania wameukataa.

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)
 
Good observation. Tunajua CCM watashinda na huo ndio utakuwa mwisho wa mahakama Tanzania na majaji wake wa UPE
 
Mwambusi alidai field ya SHERIA Hasa practical yake ni harakati na maandamano barabarani, Si courtini pekee!!!
 
Hongera Mzee TUPATUPA, Nategemea kuwa RA atakuwa amepiga simu uko.
 
Back
Top Bottom